Sheikh Ponda Issa Ponda amkubali Rais Magufuli

Kwa Magufuli kila goti litapigwa.

Chadema wote watakusanyika na kusujudu na kutubu .
Umemsujudia unataka wengine wasujudu kwa kamungu kako.alafu unatangaza ujinga wa kiwango.IMEANDIKWA MSUJUDIE BWANA MUNGU WAKO UMUABUDU YEYE PEKE YAKE.
 
Hivi kati ya Magufuli na Sheikh Ponda nani kamkubali mwingine. Kwa uelewa wangu mheshimiwa raisi kamuunga mkono mpambanaji Sheikh Ponda na kawaumbua wanafk bakwata na wanaowaunga mkono. Wasisi wetu ni juu ya utekelezaji wa tamko hilo.
Basi tuseme kuwa wamekubaliana. JPM alimkubali Ponda na Ponda kamkubali JPM. Hapo tunasema ngoma draw
 
Umemsujudia unataka wengine wasujudu kwa kamungu kako.alafu unatangaza ujinga wa kiwango.IMEANDIKWA MSUJUDIE BWANA MUNGU WAKO UMUABUDU YEYE PEKE YAKE.
Duh! Hapa ndipo mnaponiachaga hoi. Kwani kupiga magoti ni kusujudu? Kwa Waislam kusujudu ni pale wanapoweka paji la Uso wao Ardhini. Sijajua kwa upande mwingine. Ila kule shuleni pia kulikuwa na adhabu ya kupiga magoti kuonesha unyenyekevu. Ina maana pale tulikuwa tunasujudu?
 
Ndio, kusujudu maana yake kunyenyekea. Endeleeni kukufuru sababu ya njaa. Ipo siku kipaumbele hakitakuwa tumbo, utaona taabu na shida nyingi sana
 
Kwani lini shehe Ponda alimkataa Magufuli,hapo ni kwamba Ponda anamtia moyo Magufuli kama Rais kuhakikisha dhulma inatoweka nchini.
 
Ponda ni mpenda haki, so kakutana na mpenda haki mwenzie...wapenda haki siku zote huwelewana na huwezi kuta wamegombana,safi sana,

Magufuli waabheja sanaa
Ponda waabheja nkoi
 
Iwapo serikali itakuwa Inatoa Fedha Kugharimia Maswala ya Kidini, Na Kiimani Basi Ni Vizuri yakifanyika Kwa Wote. Ingawa ingekuwa Siasa haihusiki ni Jambo zuri tu, Lakini Je Utaanza na Kuishia wapi katika Kutumia Fedha za kodi za Kila mwananchi kugharimia shughuli za dini au imani? Lengo hasa la Kufanya Hivyo Ni nini?

==========

SIKU moja baada ya Rais John Magufuli kuahidi kusaidia kurudisha mali ambazo Waislamu wamenyang’anywa au kurubuniwa,

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameibuka na kusema anamuunga mkono Rais katika hatua hiyo huku akimtaka kukaa na jumuiya yao ili washauriane juu ya mahitaji yao ya msingi.

Sheikh Ponda, ambaye alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Nipashe jana, alisema Rais Magufuli ameonyesha moyo wa kusaidia dini hiyo kwa kitendo chake cha kutoa fedha za kusaidia wanaokwenda hija.

Alimshauri Rais sasa kukaa na jumuiya yao ili asaidie maeneo ya kipaumbele kama elimu na afya, baada ya kutoa mchango kwa watu wanaokwenda kuhiji.

“Jana (juzi) nimeona ametoa hela kusaidia wanaoenda hija, lakini ukweli ni kwamba Jumuiya ya Waislamu ina mambo ambayo ni vipaumbele, mambo kama ya afya na elimu ambayo itakuwa vizuri tukae tuone ni namna gani atakavyotusaidia,” alisema Ponda.

Alipoulizwa kama haoni kwamba Rais anasimamia mambo hayo mawili kwa ngazi ya taifa, Ponda alijibu; “Ukiangalia wenzetu Wakristo wana hospitali na shule, na sisi pia tunayataka hayo mambo kwa hiyo ingekuwa vizuri kama tukishauriana naye ili aone namna ambavyo ataweza kutusaidia.”

Akizungumza kwenye Baraza la Idd El Fitr, juzi jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema anafahamu kwamba wapo baadhi ya watu wenye mali ambao huwatumia viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kuwarubuni kwa kuingia nao mikataba mibovu na hatimaye mali za baraza hilo hupotea.

“Mtu anakuja na kuwadanganya danganya katika kiwanja chenu eti atajenga kituo cha mafuta, ambako mngejenga msikiti. Kwani kituo cha mafuta na msikiti wapi na wapi, kipi bora?" alihoji Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliitaka Bakwata kutumia wanasheria wake kuhakikisha mali hizo zinarudishwa na kuwaonya wasiingie mikataba mibovu ambayo inasababisha migogoro.

“Serikali inapenda kuona mali za waislamu zinarudi mikononi mwa waislamu na mali za wakristo zinarudi mikononi mwa wakristo,” alisema Rais Magufuli.

Kutokana na kauli hiyo, Sheikh Ponda, ambaye amekumbana na misukosuko mingi na vyombo vya dola katika miaka ya karibuni, alisema: “Kauli ya Rais inaonyesha namna anavyojali wananchi, suala hili limeniponza kuwa na kesi mahakamani kwa miaka miwili mpaka nikashinda na sasa Rais amekuja na kauli hii, kwa kweli tutaamunga mkono.”

Chanzo: Nipashe
 
Mwanazuoni wa kiislam na mwanaharakati wa muda mrefu kupigania mali za waislam Sheikh Ponda Issa Ponda amemshukuru Mh. Rais John Pombe Magufuli kwa ahadi yake ya kusaidia kurejeshwa mali za waislam.
 
Eti watu walimsifu JK na membe wanajua diplomasia na kumponda huyu hajui anakurupuka. Walidhan kuchekacheka hovyohovyo ndio diplomasia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom