Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,792
- 31,804
Utangulizi
Nina rafiki yangu yeye ni Mkatoliki mara kwa mara hunipigia simu kuniuliza masuala ya Kiislam. Siku zilipopatikana taarifa kuwa masheikh wetu akina Mselem bin Ali wameletwa Dar es Salaam kutoka Zanzibar wako mahabusi Segerea akanipigia simu kutaka kujua kulikoni.
Katika maswali yake aliyoniuliza moja tu ndilo jibu lake lilimshtusha sana akaniuliza mara mbili mbili na jibu langu likawa ndiyo lilelile nilompa halibadiliki.
Alitaka kujua hadhi ya hawa masheikh katika jamii ya Kiislam wa Tanzania. Hapo nilimuomba ruhusa niliweke swali lake vyema. Nikamwambia, ''Sema hadhi yao katika ulimwengu mzima wa Kiislam.''
Niliamua kumpa jibu ambalo yeye kwake kama Mkatoliki atalielewa vizuri pasipo na shida wala shaka. Nilimwambia, ''Hadhi ya masheikh wetu waliotupwa rumande Segerea kwa tuhuma za ugaidi ni sawasawa na hadhi ambayo Mkatoliki yeyote duniani anampa Polycarp Pengo.''
''Hebu rudia tena jibu lako...'' Alisema.
Nami nikamwambia tena, ''Hadhi ya masheikh wetu waliotupwa rumande Segerea ni sawa na hadhi ambayo Mkatoliki yeyote duniani atampa Polycarp Pengo.''
Nilimsikia akisema,''Yesu wangu.''
=============
SHEIKH MSELLEM ALLY NA WENZAKE WATETEWA BUNGENI KWA MARA NYENGINE
Chanzo: Mwananchi
Mbunge wa CUF azua utata Bungeni
Mbunge wa Masoud Abdallah Salim leo amezua hali ya taharuki Bungeni pale alipokuwa akimuuliza waziri wa katiba na Sheria Dk Harison Mwakyembe kuhusu majukumu ya tume ya haki za Binadamu
Akiuliza swali la nyongeza Mbunge Salim amehoji kuhusu uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar ikiwa ulikuwa huru na haki ikiwa ni pamoja na watu mbalimbali kuchukuliwa hatua za kisheria pamoja na kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Aidha Mbunge huyo amehoji pia kuhusu baadhi ya wafungwa walio gerezani akielekeza shutuma dhidi ya mashekh wa jumuiya ya uamsho ambao hadi sasa wapo gerezani.
“Nataka kujua kuhusu lini mahabusu hawa kesi yao ya msingi itapatiwa ufumbuzi, kwani zipo taarifa kwamba wenzetu hawa wanafanyiwa vitendo vya ukatili gerezani.”Amesema Mbunge Masoud Abdallah Salim
Kufuatia hali hiyo Dk Mwakyembe amesema tayari wataalamu wa tume ya haki za binadamu inaandaa taarifa za utekelezaji wa haki za binadamu hivyo pindi taarifa hiyo itakapokamilika taarifa zitatolewa.
Sheikh Mselem bin Ally na Mwandishi kwenye madrasa yake Zanzibar