Uso Kwa Macho na Bingwa wa Kutafsiri Qur'an Sheikh Mselem bin Ali

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273
USO KWA MACHO NA BINGWA WA KUTAFSIRI QUR'AN SHEIKH MSELEM BIN ALI

Leo katika uzinduzi wa kitabu cha Sheikh Ponda Issa Ponda, ''Juhudi na Changamoto,'' Peacock Hotel nilibahatika kukutana na Sheikh Mselem bin Ali mwisho wa shughuli.

Miaka 10 imepita toka tuonane Zanzibar na sikuweza kumuona kwa kuwa alikuwa rumande kwa muda wote huo.

Kedhia ya Sheikh Mselem na wenzake ni kisa maarufu nchini Tanzania na kitaelezwa kwa miaka mingi sana.

Nilimfuata kumsalimia na nikachukua nafasi hiyo kumpa pole na kufahamisha kuwa juu ya tabu na dhiki walizopitia lakini umma wa Uislam Tanzania wamenufaika kupita kiasi kwa yale waliyowafika wao.

Nakumbuka alasiri moja niko Zanzibar mwaka wa 2012 nikaenda kwenye madrasa yake kumsalimia nikiwa nimeongozana na wenyeji wangu.

Sheikh alifurahi sana kuniona na baada kusalimiana nikamfahamisha kuwa nilikuwa na hamu kuja kumsalimia kwani mimi na watu wengi mtaani kwangu ni wasikilizaji wakubwa wa kipindi chake cha tafsiri ya Quran kiichikuwa kinarushwa na Radio Imaan, Morogoro.

Nikaendelea kumweleza kuwa ifikapo asubuhi majira kama ya saa tatu asubuhi kinapoanza kipindi chake radio zote za mtaani kwangu zinahama zilipokuwa zinakuja kujumika kwenye stesheni moja tu Radio Imaan kumsikiliza Sheikh Mselem bin Ali.

Nikahitimisha kuwa kumwambia kuwa nimesoma mengi kutoka kwake.

Ufundi mkubwa wa Sheikh Mselem bin Ali ni namna anavyoitafsiri Qur'an na akaitia katika maisha ya watu ya kila siku kwa lugha nyepesi sana na ya kuvutia ikawa msikilizaji anajenga picha katika matukio yaliyotokea na anayafahamu.

Ikiwa ni jambo la kutatiza atafanya rejea katika visa katika historia ya Uislam na vipi Waislam waliweza kuvuka salama.

Sheikh Mselem bin Ali kipindi chake kilivutia watu wengi pale alipokuwa wakati mwingine akieleza historia ya Zanzibar kama ilivyokuwa akifananisha na matatizo yaliyokuwapo katika jamii ya Wazanzibari.

Mtindo huu uliwavutia wasikilizaji wengi.

Siku ile Sheikh Mselem anakamatwa asubuhi yake kama kawaida nilikuwa namsikiliza katika kipindi chake cha Tafsir ya Qur'an.

Sheikh Mselem alikuwa akiwakumbusha viongozi na wanasiasa kuwa wapandapo katika majukwaa kuzungumza na wananchi wasisahau kumtanguliza Allah ili Allah aweke mkono wake kwao.

Siku ya pili ndiyo tukapata taarifa kuwa Sheikh Mselem na wenzake wamekamatwa Zanzibar.

PICHA: Picha ya Kwanza leo Sheikh Mselem bin Ali Peacock Hotel katika uzinduzi wa kitabu cha Sheikh Ponda, ''Juhudi na Changamoto.''

Picha ya pili mtoto wa Sheikh Mselem, Shaib bin Ali Mselem akipokea nishani kutoka kwa Sheikh Ahmada Kidege kwa niaba ya baba yake aliyotunukiwa na Waislam kwa ajili ya utumishi wake.

Wakati ule Sheikh Mselem alikuwa mahabusi akikabiliwa na kesi ya ugaidi.

Haukupita muda Sheikh Ahmada Kidege na yeye akakamatwa na kuwekwa mahabusu kwa miaka miwili kwa kesi ya ugaidi.

Picha ya tatu Mwandishi na Sheikh Mselem bin Ali Zanzibar, 2010.




Mwandishi na Sheikh Mselem bin Ali
 
Namkubali sana jinsi anvyojua na kuchambua vizuri Qu'ran kipindi yupo jela nilikua naomba sana dua aachiwe .
 
Back
Top Bottom