Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea!!!!!!!!!
CattleRustler,
Hakika utamu unakolea...
Kwa maana uongo umetoweka na kweli imedhihiri:
Gazeti la An-nuur linalotoka kila siku ya Ijumaa
ukurasa wa mbele limeandika kwa wino ulikoza
kibwagizo hiki:
''Sheikh Jongo ajifunze hawana shukrani hawa
Labda uritadi kama ilivyosema Qur'an
Asome kutoka kwa Suleiman Takadir.''
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
Waliokuwa Katika Picha Hii na Ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU
(Wengine Hawapo)
[*=center]Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
[*=center]Nassoro Kalumbanya (Simba)
[*=center]Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
[*=center]Mtoro Ally (Muhonda)
[*=center]John Rupia (Misheni Kota)
[*=center]Julius Nyerere (Minaki Sekondari)
[*=center]Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
[*=center]Jumbe Tambaza (Upanga)
[*=center]Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
[*=center]Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
[*=center]Mshume Kiyate (Tandamti)
[*=center]Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
[*=center]Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
[*=center]Rajab Simba (Kiungani)
[*=center]Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
[*=center]Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
[*=center]Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
[*=center]Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
[*=center]Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo)
​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Wazee hawa walifukuzwa TANU mithili ya mbwa na wao ka ustaarabu wa watu wa pwani hawakufanya tabu walijirudia majumbani mwao na na hawakutia mguu tena pale ofisi ya TANU Mtaa wa Lumumba. Mmoja baada ya mwingine walikufa na si Nyerere wala TANU ilikuwa na habarinao. Walikuwa sawa na ganda la muwa au mgomba baada ya ndizi kukatwa.
Nakuwekea hapa chini kisa chao:
''Tarehe 11 Machi, 1963, Kamati Kuu ya TANU iliyokutana Dar es Salaam ilipiga kura kuvunja kamati ya wajumbe kumi na moja ya Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake
Idd Tulio. Wazee walikusanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na wakasomewa uamuzi wa Kamati Kuu ya kulivunja Baraza la Wazee. Taarifa ilisema wazee hao ni kero kwa sababu ''dini na siasa vilikuwa vitu viwili tofauti na hawa wazee walikuwa wanachanganya dini na siasa.'' Hiki kilikuwa chombo cha ushauri ambacho wajumbe wake wote walikuwa Waislam; chombo kilichokuwa ndani ya TANU ambacho kilimuunga mkono
Nyerere na TANU tangu siku za mwanzo kabisa, kwanza chini ya uongozi wa
Sheikh Suleiman Takadir na kisha chini ya
Idd Tulio baada ya kufukuzwa kwa
Sheikh Takadir kutoka TANU. Wakati haya yote yakitendeka Kanisa ambalo wakati wa kudai uhuru lilijiweka mbali na halikutoa msaada wowote sasa likawa linanyemelea kujiingiza katika siasa likiwa na agenda yake: kuwaweka viongozi Wakristo katika nafasi za uongozi na kuutoa nje ya uongozi Waislam ambao Kanisa liliwaona hawana elimu. Jumuiya za Kiislam kama Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na EAMWS zilikuwa sasa zinapigwa vita na serikali ya
Nyerere kama vyombo ambavyo havikuwa na umuhimu wowote katika Tanganyika mpya. Katika kumuhakikishia utiifu wao juu yake, Waislam walijitahidi mwisho wa uwezo wao kuziweka taasisi zao kando na chuki za kidini dhidi ya Wakristo. Juhudi hizi hazikuthaminiwa. Serikali ilifanya juhudi za siri kuhakikisha kuwa jumuiya zote za Waislam zinapigwa marufuku.Huu ndiyo ukawa mwanzo wa kampeni za kufuta historia ya Uislam katika TANU na mwisho wa Waislam kuwa na sauti katika siasa baada ya uhuru kupatikana. Baada ya kupatikana kwa uhuru, ile nguvu ya Waislam iliyotumika kupambana na Waingereza kuleta uhuru, ikaonekana haina maana yoyote na haifai kitu tena. Kuvunjwa kwa Baraza la Wazee ndiyo ilikuwa kishiko cha mwisho cha Waislam katika TANU. Baada ya hapo Kanisa lililokuwa pembeni wakati wa kudai uhuru sasa likajitokeza waziwazi kuwapiga vita Waislam katika TANU.''