Mohamed Said
Hivi leo sheikh Jongo amekuwa sio sheikh kwasababu amekwenda kinyume na mitazamo yako??? Nadhani wewe sheikh una nafasi kubwa sana ya kumuona sheikh Jongo na kumuelimisha; nina uhakika sheikh Jongo haingii JF sasa huoni hili darsa litakuwa limepotea bure?? siku zote Bakwata imekuwa ndio taka la lawana lakini inashangaza sana kuona hadi leo mmeshindwa kuunda taasisi yenye nguvu ambayo itasimamia haki za waislamu; sheikh siku zinakwenda kilio hiki umekianza miaka mingi sana sasa nadhani huu ni wakti mauafaka wa kupata majibu ya kilio chako; maana hata ikija Chadema madarakani (Mungu aupushe mbali balaa hilo) yatakuwa ni yaleyale maana zamani tulikuwa tunasikia tunaonewa kwasababu hatuna raisi muislamu sasa mmebadili maneno tu lakini mdundo ni uleule. Nakutakia afya njema Mola aendelee kukupa wingi hakima na bausara na pale penye mapungufu ayaondoe. Amen
Chama,
Kuna baadhi ya mambo umepatia na mengine kwa uoni wangu umekosea.
Sijapatapo kusema Jongo kaacha kuwa sheikh.
Kuhusu kumuelimisha Sheikh Jongo ndiyo huku nimeeleza historia ya masheikh
waliojipendekeza na nini ulikuwa mwisho wao na hao niliowataja ni baadhi tu.
Haya yote niliyoandika yashamfikia wala usiwe na wasiwasi kuhusu hilo.
Ama kuhusu ''kilio'' hakuna anaelia.
Nimeandika historia ya Waislam katika Tanganyika na leo wale waliokuwa na
fikra kuwa hii ni nchi ya Kikristo wamebadili fikra zao.
Nadhani unalikumbuka sakata na sensa na kwa nini Waislam waligoma kushiriki
Wanachojua ni kuwa Tanganyika si nchi ya Kikristo ila Wakristo wamehodhi
fursa kwa wingi takriban fursa zote.
Haya ndiyo majibu ya juhudi zangu.
Namshukuru sana Allah kwa haya.
Hilo la kuunda taasisi yenye ''nguvu'' sijui una maana gani unaposema ''nguvu.''
Waislam tunazo taasisi nyingi zilizodhahiri na zisizo dhahiri na ndiyo maana hadi
leo unashuhudia Uislam una nguvu nchini kila kukicha umma unasonga mbele juu
ya vikwazo tulivyowekewa.
Wala hujasikia Waislam wanatoka kwenye dini yao kwa ajili ya shida.
Hilo la rais Muislam na sisi kubadili ''mdundo''sijui umelitoa wapi.
Nakushukuru kwa dua.
Amin kwa sote.