Uhuru wa Tanganyika uliletwa na watanganyika wenyewe haukuletwa kwa misingi ya kidini!
Yaezekana hayo maneno yako ikawa ni "kweli"!?
Lakini tatizo ilikua ni pale wakti wa zile harakati za ule "uhuru"...yule Nyerere na wafuasi wake aka viongozi/wanasiasa...hawakuona dhiki asilan kuzitumia dini,khasa Uislam/Waislam ili kufanza harakati zile misikitini,kwenye baadhi ya Taasisi za Kiiislam na kwingineko...ambako hata yule Julius Nyerere mwenyewe akihudhuria na dini ya Kiislam/Masheikh wakitumika ili kufanikisha harakati zile!?
Sasa,mara baada ya kupatika ule "uhuru"...ndipo ati ghafula yule Nyerere anatoa makucha yake na ati kukemea "udini"!? Ebo!
Hii topic ni ndefu mno,na nafikiri Bwana mleta mada ana maandiko kadhaa yenye kujitosheleza kwayo!?
Kwa kifupi,tatizo la yule Nyerere na takriban Wanasiasa/viongozi woote wa Kiafrika,ni yakua yale wanayo-preach siyo yaliyo ndani ya mioyo yao!?...huu ni unafiki ulokubuhu!
Kwanini yeye Nyerere hakuona umuhimu wa kuweka ile "mipaka" ya kutenganisha imani/dini na serikali au shughuli za kiserikali,katika kipindi kile muhimu mno, cha awali ya harakati za kuleta uhuru!?
Haiwezekani yakua hali hiyo ya kutenganisha/kutafautisha serikali na imani/dini za Watanganyika...kama yeye Nyerere angaliweza kuitimiza/kuijenga mapema ndani ya mioyo/fikra za Watanganyika/Waislam...labda ingemuepushia kuonekana mnafiki kwao!?
Yaani Watanganyika/Waislam,wamejikhis kutumika na kua-betrayed...taken for granted!?
Kwanini iwe huo "udini" wa Waislam, yeye Nyerere na wafuasi wake...wauone/waushtukie tu baada ya kupatikana ule uhuru!?
Wakati masuala yaleyale ya "udini",mbona yeye Nyerere hakuyapinga/kukemea,na alifaidika nayo mno kwenye harakati zile!?...hii kufaidika,ni Nyerere mwenyewe kwa mdomo wake,amesema mara kadhaa!?
Yaani Mkuu,mie najaribu kukupa ile slightly different perspective or Muslim's point of view, if you like!?
Najaribu kutumia empathy na kuwafahamu ndugu zetu Waislam,ambao nafikiri weye unadai ati haweshi kulalama,au!?
Kwa kifupi,hata kama yeye Nyerere hakua na nia ya kuleta nchi yenye misingi ya kidini....lakini impression aliyotoa tangia awali ni yakua, hapakuwapo na khitilaf amma utengano,baina ya dini/imani na serikali/shughuli za kiserikali!?
Je yule Nyerere alifanza vile kwa makusudi au bila ya kufahamu athari zake!?...je kwanini hakuona ni muhimu kufifilisha/kukemea zile harakati za "mchanganyo" wa dini/imani na zile shughuli/harakati za kuleta uhuru wa Tanganyika, tangia ile awali ya kuundwa kwa TANU!?
Nakhis hiyo nayo ni topic nyangine kabisaa,au!?
Ahsanta sana!