FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,777
Mosi mchango wa waislamu kupigania uhuru wa Tanganyika ni uongo uliojaa chuki za udini na ukanda.Ukweli ni kwamba uhuru wa Tanganyika ulipatikana kwasababu wazee wetu wote bila kujali dini,makabila au ukanda walishirikiana hadi mkoloni akasalimu amri akatuachia nchi yetu Tanganyika.
Pili uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa na sehemu moja ndogo sana "Kariakoo' huku watanganyika wa sehemu nyingine wakiwa wamelala.Ukweli ni kwamba uhuru wa Tanaganyika ulipiganiwa na watu wa sehemu mbali mbali kuanzia Upareni,Iringa,Meru,Tabora,Kigoma .........
Histohisia ya Mohamed Said imejikita katika kuwabagua watanganyika wa dini ngingine hasa wakristo na kuwaenzi waislamu hata kama mchango wenyewe hauna mashiko lakini Sheikh wa Kariakoo ataukuza bila sababu za msingi.
Bibie unataka niendeleeeeeee mbona utachoka na kushangaaaaaa.
Umesema yako lakini bado hujaonesha hata nukuu moja ambayo wewe unaona kuwa ni ya chuki.
Kuandika fulani ni muongo ni rahisi sana lakini kuleta badala ya huo uongo wake, ukweli ni huu, ni rahisi zaidi kama unao huo ukweli. Lakini kama wewe ndiye usemae uongo ukamwambia mwenzako wewe muongo na yeye ndiye asemae ukweli, inakuwa ni kazi ngumu sana wewe kuuleta ukweli
Kwa kuwa umesema "Mosi mchango wa waislamu kupigania uhuru wa Tanganyika ni uongo uliojaa chuki za udini na ukanda." sasa tunaomba tuelezee ukweli wako.
Jee, Mshume Kiyate hakuwapo ni uongo? Jee Abdul Waheed Sykes hakuwapo ni uongo? Jee, Sheikh Hassan Bin Ameir hakuwepo ni uongo?