Mohamed R
JF-Expert Member
- Mar 28, 2013
- 2,232
- 426
Huo ubwege wenu fanyeni wenyewe. Mi nasubiri gesi nipike kande. Madai yenye msingi mmeyaacha mnaleta upuuzi wa kanda hapa. Tena mi nataka wapindwe kweli kweli kama Pinda alivyoelekeza na Sugu kutolea ufafanuzi
Hiyo ingetokea lakini sio chini ya serikali ya Chichiem. Kumbuka tuliambiwa mkongo wa taifa ukikamilika gharama za mawasiliano zitashuka na yatapatikana kiurahisi zaidi. Kama mtu mzima na mfuatiliaji wa mambo jibu unalo mwenyewe.
Nakuthibitishia kuwa hata hiyo gesi ikifika DAR na kuanza kutumika kama Uniti ya Umeme itashuka, au Mitungi ya gesi ikashuka bei nitafute nitakulipa kwa gharama za mwezi mzima wa mwanzo wa huduma ya umeme na gesi utakayotumia.
Lau ahadi na maneno mazuri yanayosemwa yangekuwa yanatekelezwa leo tungekuwa na Tanzania yenye maendeleo na furaha mara kadhaa zaidi ya leo hii.