Shehena ya kwanza ya mabomba ya gesi Mtwara yawasili

Shehena ya kwanza ya mabomba ya gesi Mtwara yawasili

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,356
Shehena ya kwanza ya mabomba ya mradi wa gesi Mtwara imepokelewa bandarini leo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Waziri Mkuu amesema kuwa anashangaa kuona baadhi ya watu kwa makusudi kabisa wanapotosha ukweli wa mambo kuhusu mradi wa gesi Mtwara. Amesema lengo la serikali ni kuhamasisha uchumi wa gesi ili kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umaskini.

Aidha Waziri Mkuu ameishukuru serikali ya watu wa China kwa kuiwezesha serikali ya Tanzania kupata mkopo wa riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa gesi Mtwara. Ametoa wito kwa wananchi, wanasiasa, wanahabari na mashirika ya dini na yale yasiyo ya kiserikali na wanaharakati wote kuungana na serikali katika kufanikisha kukamilika kwa mradi huu.

Awali akizungumza kuhusu mradi huo Waziri wa Nidhati na Madini Sospeter Muhongo amesema kuwa sasa serikali imeanza safari ya maendeleo. Alisema sehemu ya kwanza ilikuwa ni kugundua rasilimali zilizopo kwenye ardhi yetu na kwamba sehemu ya pili ni kuanza kuzivuna hizo rasilimali.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC amesema shehena hiyo ni awamu ya kwanza tuu na kwamba zitakuja jumla ya meli nyingine kumi na mbili zenye shehena kama hiyo. Meli iliyowasili ina mabomba karibia 3,400.

[video=youtube_share;q4936Ej_8NY]http://youtu.be/q4936Ej_8NY[/video]

------------------------------------------
bomba.jpg
 
kwan bado msimamo wao wa kusafirisha gesi kwenda dar upo palepale? watanzania tuwaunge mkono wana mtwra tuseme NO GESI KWENDA DAR.UFISADI BONGO YATOSHA SASA.
 
kwan bado msimamo wao wa kusafirisha gesi kwenda dar upo palepale? watanzania tuwaunge mkono wana mtwra tuseme NO GESI KWENDA DAR.UFISADI BONGO YATOSHA SASA.

Huo ubwege wenu fanyeni wenyewe. Mi nasubiri gesi nipike kande. Madai yenye msingi mmeyaacha mnaleta upuuzi wa kanda hapa. Tena mi nataka wapindwe kweli kweli kama Pinda alivyoelekeza na Sugu kutolea ufafanuzi
 
Serikali dhalimu ndivyo ilivyo. Hawataki kusikia maoni ya Watanzania popote pale. Wameshapokea mabilioni ya rushwa toka kwa Wachina sasa wanataka kulazimisha huu mradi kwa nguvu zote.

kwan bado msimamo wao wa kusafirisha gesi kwenda dar upo palepale? watanzania tuwaunge mkono wana mtwra tuseme NO GESI KWENDA DAR.UFISADI BONGO YATOSHA SASA.
 
Huu ni ufisadi wa mchana. Kulikuwa na haja gani ujembe mzito hivi kwenda kupokea mabomba? Ni kutafuta ulaji ili wajilipe posho tu. Waendelee kuiba tu siku yao yaja naam imeshafika nayo yafanya haraka kama nini!
 
Mkuu EMT
Bado ninaamini wana Mtwara tunalakufanya
Ili yale tunayoyapigania yatekelezwe, nimeangalia hapo na nimesikitika sana,
Serikali ya Ni ya ajabu sana,
Ni uchumi wa aina gani wanaotaka kuujenga Mtwara? Hadi sasa naona ni Jengo la bank kuu tuu ndiyo linajengwa,
Hakuna hata moja walilo ahidi na ambalo wameanza hata kulitekeleza..
Kumbuka mkataba uliosainiwa (ule wa symbion) uliweka huu uzi https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...d-symbion-to-build-power-plant-in-mtwara.html

It is not known when the Mtwara power plant will be completed or how it will be financed. Symbion Power Tanzania,

hapa sasa lazima tuongeze mashaka kibao na tujue kuwa tunaibiwa..
Hata watanzania wasio wanamtwara yawapasa waungane na wanamtwara kwa sababu madeni yanayotengenezwa
Kutokana na huu Mradi hawatalipa wanamtwara wenyewe,

Ninaamini sana katika maendeleo ya Mtwara
 
Last edited by a moderator:
Pia mbona hamuulizi kwa nini hiyo shehena haikushushwa Mtwara moja kwa moja? Si kuna bandari kule? Why Dar?

Si mabomba yote yanashushwa Dar, mengine yanashushwa Mtwara na hata jana kwenye taarifa ya habari imeelezwa kabisa eneo ambalo yatawekwa kule Mtwara
 
Serikali dhalimu ndivyo ilivyo. Hawataki kusikia maoni ya Watanzania popote pale. Wameshapokea mabilioni ya rushwa toka kwa Wachina sasa wanataka kulazimisha huu mradi kwa nguvu zote.

Nafikiri wamesaikiliza maoni ya wengi wenye akili. Mimi maoni yangu ni kwamba hiyo gesi ni ya Tanzania na mtu yeyote anayeamini kuwa hiyo gesi ni ya Mtwara ni mpuuzi, hiyo moja. Mbili, lazima ije Dar kwani ndio kwenye matumizi (soko) na maendeleo ya watu wa Mtwara hayatakuja pasipo wenyewe kuamsha kichwa na kuacha tamaduni za kale.

Yule Mhindi kashika adabu yake
 
Pia mbona hamuulizi kwa nini hiyo shehena haikushushwa Mtwara moja kwa moja? Si kuna bandari kule? Why Dar?
Nimekuwa ninajiuliza kwa nini kuna nguvu nyingi sana ya publicity, wanapokea mabomba, wanazindiua ujenzi ambao haujaanza n.k.?
 
Mbona hamuulizi kwa nini korosho zinaletwa dar badala ya kubaki Mtwara?
Baadhi ya watanzania wamekuwa na uelewa mdogo sana. Poroja nyingi, hawaelewi kuwa hawaelewi. Shida tupu. Na wengi wana vidigirii vipya badala ya kufanya upembuzi yakinifu na kutumia "tools of analysisi" wamekuwa wazushi na wafitini huenda bila kujua. Mungu uturehemu na uwasamehe. Mabomba ya Gesi ni ya Watanzania. Tumekopa na tutalipa. La msingi ni kuuliza yana gharama gani na yatalipwa vipi? GESI ITATOKA TUU,
 
Mimi nasubir kuona mwisho wa mradi huu, nadhaka yangu ni kutofaidika siyo wana mtwara tu bali watanzania wote. Refer migodi ya madini na mali asili zingine!
 
Hakuna sababu ya kufanya uhayawani wa kuingia gharama kubwa kujenga bomba la gharama kubwa wakati gharama hizo zingeweza kuepukwa kwa kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha umeme Mtwara ambacho kinaweza kabisa kusaidia katika kuwa na umeme wa uhakika nchini na ule wa ziada kuuzwa nchi za jirani. Hii pia ingesaidia katika kuzalisha ajira chungu nzima na kuweza kuinua viwango vya maisha vya wana Mtwara wengi ambao hali zao za kimaisha ni duni mno. Wana Mtwara nao ni Watanzania wanastahili kupata maendeleo ya kuridhisha kama ilivyo katika baadhi ya mikoa michache. Kunyanyua viwango vya maisha vya Wanamtwara ni kunyanyua viwango vya maisha vya Watanzania.

Nafikiri wamesaikiliza maoni ya wengi wenye akili. Mimi maoni yangu ni kwamba hiyo gesi ni ya Tanzania na mtu yeyote anayeamini kuwa hiyo gesi ni ya Mtwara ni mpuuzi, hiyo moja. Mbili, lazima ije Dar kwani ndio kwenye matumizi (soko) na maendeleo ya watu wa Mtwara hayatakuja pasipo wenyewe kuamsha kichwa na kuacha tamaduni za kale.

Yule Mhindi kashika adabu yake
 
Nafikiri wamesaikiliza maoni ya wengi wenye akili. Mimi maoni yangu ni kwamba hiyo gesi ni ya Tanzania na mtu yeyote anayeamini kuwa hiyo gesi ni ya Mtwara ni mpuuzi, hiyo moja. Mbili, lazima ije Dar kwani ndio kwenye matumizi (soko) na maendeleo ya watu wa Mtwara hayatakuja pasipo wenyewe kuamsha kichwa na kuacha tamaduni za kale.

Yule Mhindi kashika adabu yake

We Mwana Mtoka Pabaya nimeshakusoma wala hauna akili..usijione kuwa Unaakili,
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri wamesaikiliza maoni ya wengi wenye akili. Mimi maoni yangu ni kwamba hiyo gesi ni ya Tanzania na mtu yeyote anayeamini kuwa hiyo gesi ni ya Mtwara ni mpuuzi, hiyo moja. Mbili, lazima ije Dar kwani ndio kwenye matumizi (soko) na maendeleo ya watu wa Mtwara hayatakuja pasipo wenyewe kuamsha kichwa na kuacha tamaduni za kale.

Yule Mhindi kashika adabu yake

Na yeyote anayeamini gesi ni ya Tanzania wakati iko mtwara na maslahi ya Mtwara hayaangaliwi ni MPUUZI.
 
kwa mantiki hii tutarajie kushuhudia makubwa zaidi ktk fezi mpya ya sakata la gesi-mtwara.god 4bid.
 
Back
Top Bottom