Shehe Mkuu wa Tanzania awakataza Waislamu kushiriki maandamano ya kisiasa

Mwenyezi Mungu ndio ana-manage uislamu, hao ni viongozi wakitoa agizo ambalo alipingani na dini tunalifuata kama linapingana na dini tunalipotezea. Leo nimeamini kuwa wapenzi na wanachama wengi wa CHADEMA ni waikristu.

Basi wkristu watakuwa wapo hadi ndani ya uislam! Inauma!!
 
Mwenyezi Mungu ndio ana-manage uislamu, hao ni viongozi wakitoa agizo ambalo alipingani na dini tunalifuata kama linapingana na dini tunalipotezea. Leo nimeamini kuwa wapenzi na wanachama wengi wa CHADEMA ni waikristu.

Na wa cuf je?
 
wajumbe tupunguze ukali wa maneno lengo ni kutoa muongozo na si kutukanana ....nadhani kabla hatujaenda mbali lazima kwanza tupate Habari kwanini Mufti anapinga maandamano? kwanini Sasa na si wakati mwingine? yeye anasema kwa niaba ya nani? je anayewasemea wamekubaliana na jambo hilo? na pia madhara ya kauli zake kwa taifa
 
Research nyingi zinaonesha nchi nyingi zilizoendelea hasahasa europe watu wake hawana misingi ya kidini. They mostly rely on facts. Now i know why.
 
naomba kuuliza hivi kwa nini BALUKTA ilifutwa? Na je taasisi ya waislamu ni BAKWATA tu? Je na waislamu wengine wenye itikadi tofauti na hao wao wanasimamia wapi? Kwa upande wangu hao Viongozi wa BAKWATA siwaamini wameshindwa kuishinikiza ccm(serikali) iwape mahakama ya kadhi kama walivyoahidiwa afu bado wanaipigia debe! Wanaongoza waislamu kwa manufaa ya nani? No wonder ktk mgogoro wa msikiti wa ijumaa Arusha Bakwata wanasaidiwa na polisi kudhulumu baraza la wazee la msikiti,

BALUKTA ilifutwa kwa sababu viongozi wake wakuu hasa Shekh Yahya Husein walipenda fedha za ccm na serikali yake kuliko kazi za kidini.
 
Shehe mkuu wa Tanzania mufti shaaban bin Simba amesema ya kwamba Raisi kikwete anaandamwa kutokana na imani yake,ameyasema hayo wakati akizungumza na baraza la maulamaa lililowakutanisha mashehe mbalimbali,,alisema ,hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.

Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.

“Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja” alisema Mufti Simba.
 
Huku ndio kuwagawa watanzania kwa misingi ya kidini, nataka kujua atachukuliwa hatua gani na wahusika
 
Shame on you! You demonstrate your highest degree of phobia and intolerance aginst fellow human beings, just because they happen to take a different view or belief. Na anayesema kwamba kutokula kahawa na kashata ni kusoma basi huo ni upuuzi na nina hakika hata wewe elimu yako ni ya kubabaisha tu!

Acha hasira wewe! Unamkosoa mtu na wewe unaendelea kufanya makosa hayo hayo ya kutovumilia misimamo kinzani ya wenzio. Nani asiyejua kuwa wazee wa vibandiko ni mabingwa kwa vijiwe vya kahawa na kashata! Hiyo ni lugha ya kumbainisha mtu, hata kama huipendi.
 
Nashauri BAKWATA sasa iwe kitengo rasmi cha CCM kama UVCCM,UWT na Jumuiya ya Wazazi. Mbona CUF,NCCR wanaandamana hawaja walaani kuwa wanataka kuharibu amani? Halafu kwa nini kila kitu wao wanapenda KULAANI? Kwani hakukuwa na njia njingine ya kufikisha ujumbe wao bila kulaani???
 
Shehe mkuu wa Tanzania mufti shaaban bin Simba amesema ya kwamba Raisi kikwete anaandamwa kutokana na imani yake,ameyasema hayo wakati akizungumza na baraza la maulamaa lililowakutanisha mashehe mbalimbali,,alisema ,hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.

Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.

Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja alisema Mufti Simba.

Acheni kujishuku. Mnataka rais aharibu mambo, aongoze nchi hovyo, na asababishe maisha magumu kwa wananchi halafu wananchi wakae kimya eti kwa sababu ni muislam. Upuuzi gani huu!
 
Duh hii kali! Kama imefikia hatua ya kusema namna hii sijui tunaelekea wapi watz. Lakini huo udini unaosemwa juu ya Jk mbona hatujausikia au viongozi wao ndio wanauona pekee. Jamaa wana JF ni wapi JK kasemwa kwasababu ya dini yake tukumbushana tafadhali.

SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba, amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.

Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amewataka waumini hao wa Kiislamu kuvunja ukimya katika mambo mbalimbali yanayojitokeza nchini hususani yanayohusu mustakabali wa Taifa, na kuwataka mashehe na maimamu wa misikiti yote nchini kuwaasa waumini wa dini hiyo kuyapinga maandamano hayo kwa njia ya kistaabu ili amani idumishwe.

Bila kutaja chama au wanasiasa wanaoendesha maandamano hayo, Mufti Simba amesema , kimantiki maandamano hayo si halali kwa kuwa yanaonesha waziwazi kudhoofisha nguvu za Rais aliyepo madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani,” amesema Mufti Simba leo.

Aidha, amesema, hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.

Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.

“Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja” alisema Mufti Simba.

Amelaani mashambulizi ya baadhi ya Magharibi dhidi Libya, akisema kinaonesha ile ni vita dhidi ya Uislamu na siyo vinginevyo kwa kuwa ni kawaida ya nchi ya Marekani kuziandama nchi zenye Waislamu.

Kuhusu Mahakama ya Kadhi, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wake kwa kuwa ni moja ya nguzo muhimu ndani ya dini hiyo huku pia akiwataka maaskofu kuacha kuingilia kati suala hilo.

Ameshangazwa kuona Waislamu wanapotaka kufanyiwa jambo lolote kunajitokeza ugumu kulitekeleza tofauti na dini nyingine, jambo alilosema halipaswi kufanywa hivyo kwa kuwa ‘wote ni watoto wa baba mmoja.’

Source: Habari Leo
 
SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba, amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.

Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amewataka waumini hao wa Kiislamu kuvunja ukimya katika mambo mbalimbali yanayojitokeza nchini hususani yanayohusu mustakabali wa Taifa, na kuwataka mashehe na maimamu wa misikiti yote nchini kuwaasa waumini wa dini hiyo kuyapinga maandamano hayo kwa njia ya kistaabu ili amani idumishwe.

Bila kutaja chama au wanasiasa wanaoendesha maandamano hayo, Mufti Simba amesema , kimantiki maandamano hayo si halali kwa kuwa yanaonesha waziwazi kudhoofisha nguvu za Rais aliyepo madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani,” amesema Mufti Simba leo
 
Waislam kwa nini hawamtoi kwenye hicho cheo wampe Ramadhani Dau awe Mufti
 
Huyo mufti hata elimu ya dini hana

sasa which is which, tumwamini nani? wengine mnasema hana elimu dunia ana ya dini tu, na wengine mnasema hata ya dini hana. How did he climbed the radar na kuwa mufti?
 
Back
Top Bottom