Shehe Mkuu wa Tanzania awakataza Waislamu kushiriki maandamano ya kisiasa

naomba kuuliza hivi kwa nini BALUKTA ilifutwa? Na je taasisi ya waislamu ni BAKWATA tu? Je na waislamu wengine wenye itikadi tofauti na hao wao wanasimamia wapi? Kwa upande wangu hao Viongozi wa BAKWATA siwaamini wameshindwa kuishinikiza ccm(serikali) iwape mahakama ya kadhi kama walivyoahidiwa afu bado wanaipigia debe! Wanaongoza waislamu kwa manufaa ya nani? No wonder ktk mgogoro wa msikiti wa ijumaa Arusha Bakwata wanasaidiwa na polisi kudhulumu baraza la wazee la msikiti,

waislamu huwa wanaboa sana, badala ya kuzungumzia masuala ya kitaifa wanazunguzia mambo ya kadhi ambayo hayana faida yoyote kwa maendeleo ya nchi!
 
Wacha kutuzuga hapa! wakati tulipowaambia kuwa Nyerere mwaka 1968 huko Iringa aliasisi BAKWATA ambayo huyu Mufti anaiongoza, baada ya kuivunja jumuiya tukufu ya Waislamu(EAMWA) mlikanusha kwa matusi na kejeli kwa kumtetea huyo Baba yenu wa Taifa! leo unashangaa nini Mufti kuitetea CCM?

Mufti na BAKWATA wanahaki kabisa kuitetea Serikali ya CCM kwasababu wao ni kitengo cha Serikali ndio maana Waislamu wengi hawamtambui huyu Mufti! Ubaguzi wa kidini mlianza wenyewe sasa jinamizi la ubaguzi litaendelea kuwatafuna!
mkuu leo umepata thanks yangu, maneno yako murua
 
Hivi kuna mtu anaona "Bomu" linalo tengenezwa Tanzania kama nionavo mimi?

Tanzania imesifiwa kuwa nchi ya amani duniani kote,natabiri,.....kwa jinsi tunavo endelea sasa,..mda si mrefu Tanzania itageuka kisiwa cha umwagaji damu duniani na itakuwa ngumu kumaliza vita tunayo ichochoea sasa,itakuwa rahisi kupata amani somalia,sudan etc kuliko kupata amani Tanzania!

Am sorry for the prophecy ila ndicho ninacho ona,...yatakuja mapigano ya kidini,kati ya walionacho na wasio nacho,....na hasira zote zilizotunzwa sasa ndani ya moyo wa kila mmoja zitatoka mda huo!

Namuomba Mungu either nisiwepo duniani,au nikiwepo nisiwe Tanzania!

Na chanzo cha kutoweka kwa amani Tanzania,iwe ni leo au miaka 50 ijayo ni Kikwete kwa kuwasha moto wa udini nchini!
 
Ni kweli maandamano yanayoendelea nchini sio dalili nzuri, ina maana lazima kuna chanzo. Kama mambo yangekuwa mazuri nchini wala Shehe asingewambia watu kuacha kuandamana maana wasingekuwa na haja ya kuandamana. Jambo la kujiuliza ni kwamba ni kwa nini waandamane sasa hivi? Kwa maana hiyo wahusika washughulikie chanzo cha maandamano, kama tatizo ni kupanda kwa gharama za maisha, watu wwwezeshwe na kuelimishwa kuhusu kufanya kazi kwa bidii. Miaka ya nyuma watu waliukuwa wakindamana kuunga mkono tamko fulani.
 
Shekh pole sana,lakin katk dunia ya sasa ambayo watu wanajionea uozo unaoendelea kufanyika ni ngum sana kuwakataza wasishrik ktk maandamano,halaf shekhe wangu umepotoka,nani kakwambia kuwa lengo la maandamano ni kuvuruga aman na kuwagawa wa tz?
 
mimi siwezi kuchangia hii thread mpaka mtu atuwekee cv ya mufti hapa. naomba kujuwa elimu pls.
 
namheshimu sana mufti na naomba ndugu waislamu mnisamehe kama nitakuwa nimewaudhi. nimemsikia mufti akilaani maandamano ya chadema na akawataka maimamu nchi nzima walaani pia. anasema uchaguzi umekwisha watu wakubali matokeo. si siku nyingi zimepita alisema viongozi wa dini wasijihusishe na siasa. je, haya anayozungumza si siasa? chadema wanapinga matokeo? mbona mauaji ya arusha alifurahia? namwonea huruma ccm wanamtumia. ila najiuliza, je, rais ajaye akiwa mkristo atakuwa anamtetea pia? mnisamehe lakini n
Viongozi wetu wa dini Mashehe na Maaskofu wameanza kupoteza uhalali wa kukubalika ktk jamii kwa vitendo vya kujihusisha ktk siasa na kuwa na upendeleo kwa vyama vya kisiasa. Ni vyema wakawa wazi kuhusu itikadi zao za kisiasa kuliko kumuingiza MUNGU ktk mambo ya kisiasa na kujifanya wao ndio mawakala wa MUNGU humu Duniani, wote tuna akili na MUNGU kampa kila mtu uwezo wa kumtambua yeye na kumuabudu na kumtumikia, hakuna aliye bora kwa MUNGU kuliko mwenzake hivyo viongozi hawa wa dini wasituchanganye. Watu wengi wanauelewa mkubwa wa siasa na uchumi kuliko viongozi wetu wa dini hizi mbili hivyo wasijifanye kutoa miongozo ya kuwaamulia waumini wao CHAMA gani wafuate au itikadi gani ya kisiasa wafuate, wao sio MAWAKALA WA MUNGU wasitake kutuaminisha kwamba kauli zao ni kauli za MUNGU.
Uwanja huu wa kisiasa tuachiwe tuamue wenyewe kwa utashi wetu maana kama shida tunapata sisi, ugumu wa maisha wetu, UFISADI unatuumiza sisi, kushuka kwa elimu kunatusumbua sisi na watoto wetu, ukosefu wa ajira unatubana sisi hapo DINI inaingia wapi?

Kama wao ni majasiri na wanaguswa na shida zetu kwanini wasiwaumbue MAFISADI na VIONGOZI wabovu makanisani na misikitini kwa kuwakemea ikibidi kwa majina, Maana viongozi na MAFISADI si ni waumini wao? Wao ni kupokea misaada na sadaka tu kwa MAFISADI na VIONGOZI MAMLUKI. HARAMBEE za ujenzi wa kanisa na misikiti wanawafuata na kuwaomba wawe wageni rasmi au wanawaomba misaada bila haya. PENYE MAHITAJI YA FEDHA WAO NDIO WANAWAKIMBILIA MAFISADI WACHANGIE MAKANISA NA MISIKITI. Kama wao ni MAWAKALA wa MUNGU hawaonyeshwi kwenye maombi yao kuwa FEDHA HIZO NI CHAFU/HARAMU? MUNGU apokei SADAKA chafu na haramu.

Watuache na maamuzi yetu na wasituchagulie itikadi gani ya kufuata
 
Mkuu wa dini nafikiri haelewi au amesahau au washauri wake wamemshauri vibaya. Hivi kweli hajui kuwa ndani ya wanasiasa wamo waislamu? Hivi anaweza kuwazuia Kikwete, Makamba, Mzee Mwinyi, Shein, Lipumba, Seif kushiriki maandamano ya wanasiasa?! mbona hawa siasa ni part and parcel ya maisha yao? Au alikuwa na maana gani? Hivi hajui kwamba yule anayekwenda kuswali msikitini ndiyo huyo huyo mwanasiasa? wanasiasa hawatakiwa kuwa waislamu? Hapa Sheik Mkuu kapotoka ama kapotoshwa.
 
SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba, amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.

Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amewataka waumini hao wa Kiislamu kuvunja ukimya katika mambo mbalimbali yanayojitokeza nchini hususani yanayohusu mustakabali wa Taifa, na kuwataka mashehe na maimamu wa misikiti yote nchini kuwaasa waumini wa dini hiyo kuyapinga maandamano hayo kwa njia ya kistaabu ili amani idumishwe.

Bila kutaja chama au wanasiasa wanaoendesha maandamano hayo, Mufti Simba amesema , kimantiki maandamano hayo si halali kwa kuwa yanaonesha waziwazi kudhoofisha nguvu za Rais aliyepo madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake.

"Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani," amesema Mufti Simba leo

Swadakta Sheikh tumekusikia na kukukubali kwani sote ni wapenda AMANI
 
Speaker,
Ni kweli Tanzania inaelekea katika umwagaji damu mkubwa kama watanzania hawatakua makini. Na chanzo kikuu cha udini huu ni Baba yenu wa taifa na Kanisa Katoliki. Binafsi namuunga mkono mufti katika suala la Chadema na mahakama ya kadhi but katika swala la Libya nadhani msimamo wake sio sahihi. Hata hivyo huyo ni Mufti wa serikali na hivyo sishangai anayoyasema ila ukweli unajulikana Chadema wanasukumwa na Kanisa Katoliki nahilo linatokana na kwamba Kanisa linahofia kukosa mapochopocho ya kuwa karibu na serikali. Udini aliuanzisha Nyerere sasa ndio unaiva tuombe mungu usitumbuke tu
 
Sipendi bakwata kama nisifoipenda chadema na huo ndo ukweli mwenye kauli twende kazi

Hayo ni matatizo yako sasa. Sisi hatumo....... maana bakwata na chadema wapi na wapi. linganisha vitu vinavyo shabihiana.
 
Edom Mwasamya na Aziza Masoud
SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa bin Shabani Simba amelaani maandamano yanayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akisema yanalenga kuvuruga amani ya nchi.

Akizungumza katika mkutano wa Masheikh na Maimamu jijini Dar es Salaam jana, Mufti Simba alisema lengo la maandamano hayo yanayoendelea ni kuharibu amani ya nchi... “Wanasiasa wanataka kuivuruga nchi kwa visingizio kuwa wanataka kulinda amani, hivyo Waislamu tumeamua kuvunja ukimya uliodumu kwa muda mrefu na kuamua kukemea vitendo hivyo.”
Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolieleza taifa katika hotuba yake ya Februari mwaka huu kuwa chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.

Kauli hiyo ya Rais Kikwete, iliungwa mkono na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira ambaye alikionya Chadema akisema kisije kuilaumu Serikali itakapokosa uvumulivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.

Simba alisema kuwa mafunzo ya dini ya Kiislamu yanawapa jukumu la kutunza amani popote walipo, hivyo wameamua kukemea vitendo hivyo kwa kuwa vinahatarisha usalama wa amani iliyopo. Alisisitiza kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na walioshindwa hawana budi kusubiri kipindi kijacho badala ya kuchochea vurugu kwa kufanya maandamano nchi nzima kwa kisingizio cha kutafuta amani.

Wakati huo huo; Mufti Simba ameyashutumu mataifa ya magharibi akisema mashambulizi yake dhidi ya Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi yana lengo la kupiga vita Uislamu.

“Hakuna kiongozi aliyesaidia Uislamu duniani kama Gaddafi, sasa wameleta chokochoko ya kuwashawishi watu kuandamana na baadaye unaibuka Umoja wa Mataifa wanavamia na kudai wanawatetea wananchi,” alisema Simba.

Alisema maandamano yaliyofanywa na wananchi wa Libya yamesababishwa na shinikizo la nchi za magharibi kwani kulikuwa hakuna sababu ya watu hao kudai kwamba hawamtaki kiongozi huyo akisema amefanya mazuri mengi kwa taifa hilo.
Alisema Waislamu wote wa Tanzania wanalaani kitendo kilichofanywa na Marekani na washirika wake na kusema Masheikh, kupitia mihadhara wataendelea kukemea kitendo kilichofanywa na nchi hizo.

“Kwa niaba ya Waislamu wote wa Tanzania nalaani kitendo hicho. Siyo cha kistaarabu, hasa ikizingatiwa kuwa mashambulizi yanayofanywa na majeshi hayo yameua watu wengi kuliko wale aliowaua Ghaddaf,” alisema.
Alisema ni wazi kabisa kuwa uvamizi uliofanywa na nchi hizo hauna baraka za Umoja wa Mataifa, bali ni matakwa ya mataifa hayo ambayo yamelenga kuhakikisha Uislamu haupati nafasi duniani.

Alisema kama kweli lengo la nchi hizo lilikuwa ni kulinda usalama wa Libya na raia wake, wangetumia njia za kidemokrasia katika kutatua tatizo hilo na wala si kwa kuivamia.
 
Mbona hakemei Ufisadi uliosababisha nchi yetu kuwa taabani hana upeo au uwezo wake ni kutumwa aseme tu . maana ukiwa hakimu usikie pande zote na ujue kilichosababisha... Unaweza kutumwa na mjinga na wewe ukaonekana mjinga! na hofu na uwezo wake!!! amepewa uwezo wa kulaani na nani? kisiasa au kidini??? nitakaye muudhi anisamehe nauliza tu ila msema kweli ni mpenzi wa Mungu...
 
Hii inanikumbusha yale maandamano ya kidongo chekundu enzi za mkapa!!halafu ina maana kikwete alichaguliwa na waislam tu?mie naona kama huyu jamaa ndio anachochea udini kwa kauli hii hilo suala ilitakiwa iachiwe serikali yenyewe itatue eti wakristo wamepanga nchi isitawalike na wale mafisai waliojiuzuru kila lowasa, Mramba na wengineo ni waislamu?

Mimi sioni kabisa cha kwamba Kikwete anaonewa sijui wenzangu mnaonaje ila mie naona kama huu ndio udini wenyewe sasa umeanza kuzungumzwa misikitini eti wasihudhurie maandamano yeyote ina maana hata maandamano ya CUF wasiende?

Ustaadh hapa amekurupuka sana nadhani hata JK mwenyewe akiisoma hii atashangaa sana halafu haya maneno yanaweza yakawa ndio moto wenyewe sasa kwamba amechochea kuni maana sidhani kama wakristo nao watakaa kimya kwa hili kwasababu hii ni kashfa kwamba wakristo ndio wanaochafua serikali iliyopo madarakani je kuna ukweli hapo?

Yaani kwamba kisa serikali yake tu ionekane haifanyi kazi mie hiyo kitu nakataa kabisa kina lowasa sio waislamu kina pinda sio waislamu ila mbona wanakosea na wanawajibishwa hapa tatizo lipo kwenye system nzima ni ya kifisadi haijalishi huyu mkristo wala muislamu!!hawawajibiki ipasavyo!

Hakuna udini hapo!

Nimekukubali mzee,
problem is the system,fix system and everything is fixed...Hakuna cha uislamu wala ukristo hapo,njaa tu inasumbua...wadau wametoa mifano mingi,serikali siyo Rais peke yake watu wanapoiandama serikali maana yake Rais na cabinet yake wote hakuna kitu........cabinet ina waislamu na wakristo...lakini kubwa hayo maandamano yanachodai ni sahihi au siyo sahihi??yanaleta fujo au uvunjaji wa amani??kama hayo yote hayapo iweje mtu aanze kubabaika na yeye ana Polisi na Jeshi jamani???mtu yeyote mwenye akili timamu atumie akili yake kufikiri!!
 
siasa zitatumaliza! tuwe waangalifu,
ila udini hauna nafasi penye haki,
huwezi ukachonganisha watu kwenye mambo ya udini kama kuna haki, mwisho wa siku ukiona umeonewa utaenda mahakamani na kupata haki yako, ila kwa hali ya sasa hivi ambapo mahakama zinatawaliwa na rushwa , hakuna haki yoyote, litakalo baki ni watu kuingia mtaani na kuumizana kwa kutimia siasa au dini kama visingizio.....lakini waanzilishi wa fujo hizo wenyewe wapo wanakula kuku na kutizama tukichinjana kwenye TV
 
Shehe ana uhuru wa kusema ila hana uwezo wa kuinyamazisha CHADEMA isiendelee kuwaamsha waliolala kwenye dimbwi la usingizi mzito wa kujua haki zao. Mara kadhaa mashehe wamekuwa wakitoa matamko ya kupinga makanisa yasijiingize kwenye mambo ya siasa je haya matamko wanayotoa sio siasa? Viongozi wa waislam lazima wajenge namna ya kuishi maisha ya kawaida na ikiwezekana kutoonyesha ni vyama gani na ni viongozi wa dini gani wanawaunga mkono. Hii itawasaidia sana kuishi maisha ya kawaida hata pale itakapotokea nchi hii kushikwa na kiongozi ambaye sio wa dini yao au chama wanachokiunga mkono. Ni dhahiri sasa hivi inaeleweka wazi kuwa kwa kuwa rais kikwete ni muumini wao, basi hawawezi kuona ubaya wowote unaofanywa na ccm na hata kama upo ubaya. kulaani nchi za magharibi ni kujipasua kichwa kwani toka miaka hiyo kama laana yao wanayotoa kwa nchi za magharibi ingekuwa inasaidia nafikiri nchi hizo zingeshatoweka kwenye dunia hii.

Ushauri wangu kwa hawa wanaotoa matamko, tena mengine yakiwa yamepitwa na wakati nafikiri hayawezi kusaidia kwa sasa kwani CHADEMA itaendelea kufanya shughuli zao za kuelimika wananchi wale watako kubali watafumbuka wale wenye "usisi" watabaki kutoa matamko wengine wakipiga hatua.
 
siasa zitatumaliza! tuwe waangalifu,
ila udini hauna nafasi penye haki,
huwezi ukachonganisha watu kwenye mambo ya udini kama kuna haki, mwisho wa siku ukiona umeonewa utaenda mahakamani na kupata haki yako, ila kwa hali ya sasa hivi ambapo mahakama zinatawaliwa na rushwa , hakuna haki yoyote, litakalo baki ni watu kuingia mtaani na kuumizana kwa kutimia siasa au dini kama visingizio.....lakini waanzilishi wa fujo hizo wenyewe wapo wanakula kuku na kutizama tukichinjana kwenye TV

karibu sana Stratex.

Vipiumeshaconect, ODU zote zinaonekana, DAC je. haya sasa anza configuration usisahau kuset Freq na power.
 
Kikwete kachaguliwa na waislamu asilimia kubwa, hao wadini nyingine waliomchagua hawafiki hata 20% ya kura alizopata.

Kaka tunaomba ushahidi wa Takwimu,usiongee kama unatapika bwana!! we vipi??na ile asilimia 80% ya awamu ya kwanza ilikuwa toka kwa waislamu pia??acha uzushi.
 
......mmmmhhhh,kazi ipo!! JK au Salva asiporekebisha baadhi ya statements za Mufti tutaamini Mufti ametumwa na JK au Ikulu. Mfano wa statements ni kama 'kuandamwa kwa Jk ni kutokana na dini yake'.

Pia tusiposikia kundi linaloaminika na waislam wengi wakimpinga mufti wao, tutaamini ni stand ya waislam wote.
 
Back
Top Bottom