Shehe Mkuu wa Tanzania awakataza Waislamu kushiriki maandamano ya kisiasa

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Namheshimu sana mufti na naomba ndugu waislamu mnisamehe kama nitakuwa nimewaudhi. nimemsikia mufti akilaani maandamano ya CHADEMA na akawataka maimamu nchi nzima walaani pia.

Anasema uchaguzi umekwisha watu wakubali matokeo. Si siku nyingi zimepita alisema viongozi wa dini wasijihusishe na siasa. Je, haya anayozungumza si siasa? CHADEMA wanapinga matokeo? Mbona mauaji ya Arusha alifurahia?

Namwonea huruma, CCM wanamtumia. Ila najiuliza, je, rais ajaye akiwa mkristo atakuwa anamtetea pia? Mnisamehe lakini
 
Hivi mpaka leo mkuu ulikuwa hujui kuwa bakwata ni kitengo cha ccm na mwasisi wake ni Mwal. Nyerere?
Halafu bahati nzuri kwa ccm na mbaya kwa waisilamu, huyu shehe ana elimu ya kidini tu, elimu dunia kama waiitavyo, ni hakuna kitu. Sii ajabu ukiambawa kwa uaminifu kabisa hajui madhara ya kauli yake hiyo aliyoitoa.
Yeye tu kaambiwa sema hivi na bila kutafakari kasema kama alivyoagizwa.
.
 
Mufti anatumiwa. Hakuna muislamu muelewa asiyejua hali halisi ya tz kwa sasa. Bei ya sukari ju, wote tunaathirika,muslims and christians respectively. Tatizo ni elimu dunia ndogo aliyokuwa nayo. Waislamu umefika wakati viongozi wa dini yetu wawe pia na elimu dunia ya kuchambua mambo plus elimu ya dini pia.
 
mufti wa Tanzania alitakiwa kuwa sheikh Gorogosi msomi hodari, mungu amlaze mahali pema peponi huyu aliyepo mhhhh sisemi
 
yeye anapata gari bure,diesel bure,nyumba bure ulinzi bure,posho bila jasho asitupotezee muda huyu mzee hana wala elimu yenye upeo wa kileo.bakwata ni tawi la ccm kama vile uvccm.
 
naomba kuuliza hivi kwa nini BALUKTA ilifutwa? Na je taasisi ya waislamu ni BAKWATA tu? Je na waislamu wengine wenye itikadi tofauti na hao wao wanasimamia wapi? Kwa upande wangu hao Viongozi wa BAKWATA siwaamini wameshindwa kuishinikiza ccm(serikali) iwape mahakama ya kadhi kama walivyoahidiwa afu bado wanaipigia debe! Wanaongoza waislamu kwa manufaa ya nani? No wonder ktk mgogoro wa msikiti wa ijumaa Arusha Bakwata wanasaidiwa na polisi kudhulumu baraza la wazee la msikiti,
 
waislam ambao tunajua shida za nchi hii hayo anayosema yanaingilia sikio moja na kutokea jingine, Hatuna mda wa kutekeleza mawazo yake finyu.
 
Sipendi bakwata kama nisifoipenda chadema na huo ndo ukweli mwenye kauli twende kazi
 
Elungata unataka kauli gani nawe umesema huo ndo ukweli wako? We lala tu, tumekusoma kabla hujaandika.
 
namheshimu sana mufti na naomba ndugu waislamu mnisamehe kama nitakuwa nimewaudhi. nimemsikia mufti akilaani maandamano ya chadema na akawataka maimamu nchi nzima walaani pia. anasema uchaguzi umekwisha watu wakubali matokeo. si siku nyingi zimepita alisema viongozi wa dini wasijihusishe na siasa. je, haya anayozungumza si siasa? chadema wanapinga matokeo? mbona mauaji ya arusha alifurahia? namwonea huruma ccm wanamtumia. ila najiuliza, je, rais ajaye akiwa mkristo atakuwa anamtetea pia? mnisamehe lakini n

Wacha kutuzuga hapa! wakati tulipowaambia kuwa Nyerere mwaka 1968 huko Iringa aliasisi BAKWATA ambayo huyu Mufti anaiongoza, baada ya kuivunja jumuiya tukufu ya Waislamu(EAMWA) mlikanusha kwa matusi na kejeli kwa kumtetea huyo Baba yenu wa Taifa! leo unashangaa nini Mufti kuitetea CCM?

Mufti na BAKWATA wanahaki kabisa kuitetea Serikali ya CCM kwasababu wao ni kitengo cha Serikali ndio maana Waislamu wengi hawamtambui huyu Mufti! Ubaguzi wa kidini mlianza wenyewe sasa jinamizi la ubaguzi litaendelea kuwatafuna!
 
Elungata unataka kauli gani nawe umesema huo ndo ukweli wako? We lala tu, tumekusoma kabla hujaandika.

nilale we unajua niko wapi saa hii?ila nashukuru umenisoma but am spoiling for a fight with someone ,so if you dont want stay out of da way
 
SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba, amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.

Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kinondoni jijini Dar es Salaam.


Amewataka waumini hao wa Kiislamu kuvunja ukimya katika mambo mbalimbali yanayojitokeza nchini hususani yanayohusu mustakabali wa Taifa, na kuwataka mashehe na maimamu wa misikiti yote nchini kuwaasa waumini wa dini hiyo kuyapinga maandamano hayo kwa njia ya kistaabu ili amani idumishwe.


Bila kutaja chama au wanasiasa wanaoendesha maandamano hayo, Mufti Simba amesema , kimantiki maandamano hayo si halali kwa kuwa yanaonesha waziwazi kudhoofisha nguvu za Rais aliyepo madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake.


"Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani," amesema Mufti Simba leo.


Aidha, amesema, hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.


Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.


"Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja" alisema Mufti Simba.


Amelaani mashambulizi ya baadhi ya Magharibi dhidi Libya, akisema kinaonesha ile ni vita dhidi ya Uislamu na siyo vinginevyo kwa kuwa ni kawaida ya nchi ya Marekani kuziandama nchi zenye Waislamu.


Kuhusu Mahakama ya Kadhi, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wake kwa kuwa ni moja ya nguzo muhimu ndani ya dini hiyo huku pia akiwataka maaskofu kuacha kuingilia kati suala hilo.


Ameshangazwa kuona Waislamu wanapotaka kufanyiwa jambo lolote kunajitokeza ugumu kulitekeleza tofauti na dini nyingine, jambo alilosema halipaswi kufanywa hivyo kwa kuwa ‘wote ni watoto wa baba mmoja.'


Source: Habari Leo
 
Sasa hizo ndio siasa za udini ambazo madhara yake ni makubwa kuliko maandamano anayoyapinga kiongozi huyu. Mimi siamini kabisa kwamba raisi wetu ati anaandamwa kutokana na imani ya dini yake. Namuomba mheshimiwa raisi atoe tamko lakupinga upotoshaji huu wawazi. Amani itabomolewa na matabaka yaliyopo na matumizi mabaya ya raslimali za taifa.
 
Cjaickia wakuu,kakataza khudhuria maandamano ya Cdm tu,au pamoja na ya vyama vingine?
 
Back
Top Bottom