Shehe Mkuu wa Tanzania awakataza Waislamu kushiriki maandamano ya kisiasa

Dini zisipotoshe watu,matatizo yetu watanzania yapo palepale! Yameongezeka kutokana na uongozi mbovu usio na focus kuleta maendeleo kwa wote.

Sielewi tunapoelekea,kama hio mahakama ya kadhi italeta maendeleo tutaiona; ila wafanyayo chadema ndio hayo hata bei ya sukari ikapunguzwa. Watanzania tuamue wenyewe, kusuka ama kunyoa!!
 
namheshimu sana mufti na naomba ndugu waislamu mnisamehe kama nitakuwa nimewaudhi. nimemsikia mufti akilaani maandamano ya chadema na akawataka maimamu nchi nzima walaani pia. anasema uchaguzi umekwisha watu wakubali matokeo. si siku nyingi zimepita alisema viongozi wa dini wasijihusishe na siasa. je, haya anayozungumza si siasa? chadema wanapinga matokeo? mbona mauaji ya arusha alifurahia? namwonea huruma ccm wanamtumia. ila najiuliza, je, rais ajaye akiwa mkristo atakuwa anamtetea pia? mnisamehe lakini n

Mbona samahani nyingi? Au kwa kuwa unajua kwamba umewakwaza? Mwache atoe maoni yake kama viongozi wengine wa dini wanavyofanya. Tumewasikia hapa akina Cardinal wakikemea na kutoa maoni yao lakini hatukuona chochote zaidi ya maoni ya kumpongeza kwamba yuko focused na aheshimiwe. Why? Kwa sababu ni Cardinal au kwa sababu alikisemea chama fulani? Unataka tuamini pale Mwadhama alipokosoa chama tawala (tena kwa usahihi) alifanya hivyo kwa sababu rais aliyepo ni muislamu na kwamba ingekuwa vinginevyo asingekosoa? Give us a break man!
 
mufti wa Tanzania alitakiwa kuwa sheikh Gorogosi msomi hodari, mungu amlaze mahali pema peponi huyu aliyepo mhhhh sisemi

Huwezi kuwapangia waislamu nani awe mufti wao! Mbona Gorogosi alipokuwa hai hukuwahi kumsifia kwa lolote? Unafiki tuuuu!
 
Kauli ya kujidhalilisha mno kutoka kwa kiongozi, ambaye haikutegemewa kabisa atamke hivi!

Hivi anadhani waislamu wote wanapelekwa kutibiwa nje kama yeye anavyofanyiwa na familia yake?

Nitawashangaa waislamu kama wataipokea kauli hii na kuifanyia kazi!

Mtu yeyote makini anajua wazi kwamba hakuna kitu chochote cha dini ndani ya Maandamano ya CHADEMA, sasa udini wa huyu shehe mkuu unazaliwa na nini?

Hii ni mbinu ya Mkubwa, ameamua kumtumia kiongozi huyu, au kumnunua kwa kumwahidi pepo ili aende kinyume na maagizo ya dini!

Ni ajabu kuwa Watanzania tunaishi nchi moja, lakini tunasikilizia kitofauti makali ya maisha just due to religious differences!..
.my hairs~!~!!
 
Aidha, amesema, hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.

Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.

"Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja" alisema Mufti Simba.

Amelaani mashambulizi ya baadhi ya Magharibi dhidi Libya, akisema kinaonesha ile ni vita dhidi ya Uislamu na siyo vinginevyo kwa kuwa ni kawaida ya nchi ya Marekani kuziandama nchi zenye Waislamu.

Source: Habari Leo
Retarded
 
Whether mnataka or hamataki lakini huyo ndiye mufti wenu anayeamua masuala yenu wazee wa kahawa na kashata. Mtu kama wewe na mkwere mwenzio kutomwita Nyerere Baba wa Taifa hakumpunguzii hadhi yake. Mmechelewa na daima Nyerere atabaki kuwa Baba wa Taifa. Kama aliwaundia BAKWATA ni umbumbu wenu wa kuendekeza ubwaubwa badala ya elimu. Sasa tulieni muendelee kunyolewa na ccm ambayo kila inapotaka kuwatumia lazima iandae pilau, kahawa na kashata. Shekhe mkuu wenu naye ni mwanachama hai wa ccm. Kwa hiyo sishangai.

Shame on you! You demonstrate your highest degree of phobia and intolerance aginst fellow human beings, just because they happen to take a different view or belief. Na anayesema kwamba kutokula kahawa na kashata ni kusoma basi huo ni upuuzi na nina hakika hata wewe elimu yako ni ya kubabaisha tu!
 
Ni vizuri kuwaachia Waislam wenyewe wachague la kufanya... Kwani ni watu wazima na wanajua kuchambua mbivu na mbichi.. 'ASIWAPANGIE'
 
mufti makamba jk tambwe lipumba hamad wote sawa tu huo ndo udini anaosema jk sometime elimu inasaidia pia angalia matamko ya wakatoliki na ya mufti coz am not sure kama ni ya waislam wote mbona hatoi tamko kuhusu hali ya mfumko wa bei au anahudumiwa na serikari hizi propaganda zinatupeleka wapi ccm wanatupeleka wapi waislam pamoja na jk inabidi watoe tamko kali kukanusha vinginevyo hali itakuwa mbaya ccm kweli kinakufa
 
Ni vizuri kuwaachia Waislam wenyewe wachague la kufanya... Kwani ni watu wazima na wanajua kuchambua mbivu na mbichi.. 'ASIWAPANGIE'

good, huyo Simba asitafute kuwagawa watz, kila mtu atumie akili yake kujua hayo maandamano yana faida au la!
 
Ni Serikali ya JK iliyomlipia Mufti usafiri na matibabu hivi karibuni kwenye hospital moja nchini India?Nipo sahihi au nimechanganya mambo?
 
NAMSIKITIKIA SANA MUFTI, PASI NA KUONEA HURUMA RAIA WANAOUAWA HUKO LIBYA, YE ANALILIA MISAADA? Hapo ishu kubwa kwake ni misaada, hawez kufikir zaid ya hapo
 
kwa nini..?!! kwa sababu hawataki kuandamana..?!!.. tuandamane ili iweje..?!: yatokee kama yaliotokea arusha..? wewe ndio uache unafiki..

."You fools!" (Jesus) Luke 11:40 , "You blind fools!" (Jesus) Mat 23:17 "How foolish you are" (Jesus) Luke 24:25

Polisi ndio waliofyatua Risasi na kuua raia kule Arusha wala si CDM! Mbona kanda ya ziwa hakuna damu ilyomwagika? Mtaiona IKULU chungu mwaka huu mpaka JK atakosa muda wa kwenda kubembea kule majuu!
 
hivi kati ya huyu na yule wa Bakwata wanatofauti gani?

maana last time I checked wengi hawamkubali..kwa maana Shia, bokhora, kadiani na wengineo

wao wanadai hawakumchagua hivyo hawawakilishi lakini waislama wenyewe wanajuana
 
AMECHELEWA SANA KUSEMA BINAFSI NILILITEGEMEA HILO, Ametoa kauli isiyo na hoja yoyote ndani yake. Wadau kumbukeni huyu mzee anakiwango cha chin kielimu so kunauwezekano kuchangia kwa uelewa mdogo alionao!
 
SHEHE Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaaban bin Simba, amewataka Waislamu wote nchini kutoshiriki katika maandamano ya wanasiasa yanaoendelea nchini kwa vile yanalenga kuleta uvunjifu wa amani.

Mufti Simba ametoa agizo hilo alipozungumza na Baraza la Maulamaa lililowashirikisha mashehe na maimamu mbalimbali wa Tanzania katika Msikiti wa Farouk uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Amewataka waumini hao wa Kiislamu kuvunja ukimya katika mambo mbalimbali yanayojitokeza nchini hususani yanayohusu mustakabali wa Taifa, na kuwataka mashehe na maimamu wa misikiti yote nchini kuwaasa waumini wa dini hiyo kuyapinga maandamano hayo kwa njia ya kistaabu ili amani idumishwe.

Bila kutaja chama au wanasiasa wanaoendesha maandamano hayo, Mufti Simba amesema , kimantiki maandamano hayo si halali kwa kuwa yanaonesha waziwazi kudhoofisha nguvu za Rais aliyepo madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Sisemi ni wanasiasa wa wapi wanaochochea maandamano hayo kwa kuwa kila mmoja anajionea mwenyewe, wao badala ya kutetea amani wanageuka na kuwa wavurugaji wakubwa wa amani,” amesema Mufti Simba leo.

Aidha, amesema, hivi sasa Rais Jakaya Kikwete anaandamwa kutokana na imani ya dini yake huku waumini na viongozi wa Kiislamu wakibaki kimya bila ya kuyazungumzia masuala yanayojitokeza likiwemo hilo.

Amesema, tofauti na uongozi wa marais wanaokuwa na imani ya Kiislamu, marais wanaokuwa na imani ya Kikristo huwa hawaandamwi kiasi hicho na hivyo kuleta tafsiri kuwa imani ya dini ndiyo chanzo cha yote yanayofanywa rais aandamwe.

“Misikiti iungurume na wala isikae kimya, ukimya ufe na yalaani mabaya yote hayo pamoja na dini ya Kiislamu kufanywa tabaka la chini, tuamke na tushikamane kwa pamoja” alisema Mufti Simba.

Amelaani mashambulizi ya baadhi ya Magharibi dhidi Libya, akisema kinaonesha ile ni vita dhidi ya Uislamu na siyo vinginevyo kwa kuwa ni kawaida ya nchi ya Marekani kuziandama nchi zenye Waislamu.

Kuhusu Mahakama ya Kadhi, ameiomba Serikali kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wake kwa kuwa ni moja ya nguzo muhimu ndani ya dini hiyo huku pia akiwataka maaskofu kuacha kuingilia kati suala hilo.

Ameshangazwa kuona Waislamu wanapotaka kufanyiwa jambo lolote kunajitokeza ugumu kulitekeleza tofauti na dini nyingine, jambo alilosema halipaswi kufanywa hivyo kwa kuwa ‘wote ni watoto wa baba mmoja.’

Source: Habari Leo


Hakika JK amefanikiwa kuigawa nchi hii katika makundi, baada ya kuwagawa wanachama wa CCM katika makundi (wanamtandao, etc) sasa amefanikiwa kuigawa nchi katika misingi ya dini! Amefanikiwa kumrubuni hata MUFTI aamini upuuzi huu???!!

Kwa mtu yeyote mwenye sound mind atajiuliza, wale waliokua wanasema JK ni chaguo la Mungu hawakujua kuwa yeye mwislamu? ...sasa ndio wamejua kuwa kumbe ni muislamu na kuanza kumbagua? Haingii akilini...

Facts are on the ground kwamba yeye nchi imemshinda sio kutokana na dini yake bali kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi period! Bei ya unga kutoka Sh.600/- per kg mwaka 2005 hadi Sh. 1,500/- mwaka 2011; sukari kutoka Sh. 500/- per kg (mwaka 2005) had Sh. 2000/- per kg (2011); etc...Siamini kama ugumu wa maisha unawabana wakristo peke yao na wenzao waislamu hawauumii!!!
 
Kwani huyu muft simba ndo mume wa yule sofia simba?(mropokaji) nijulishen jamani.
 
Hapa suala la udini lisitumike kutugawa.ccm kina wakristo na waislamu cdm kuna wakristo na waislam,CCM TUMEKICHOKA.
 
Sasa hizo ndio siasa za udini ambazo madhara yake ni makubwa kuliko maandamano anayoyapinga kiongozi huyu. Mimi siamini kabisa kwamba raisi wetu ati anaandamwa kutokana na imani ya dini yake. Namuomba mheshimiwa raisi atoe tamko lakupinga upotoshaji huu wawazi. Amani itabomolewa na matabaka yaliyopo na matumizi mabaya ya raslimali za taifa.

Kiwete ni kweli inabidi apinge huu upuuzi vinginevyo atakuwa anauunga mkono ujinga wa huyu Mufti, hivi wakristu wakiwa na akili mbaya kama hizi nao wawaambie wakristo waandamane hii nchi itakalika? Rais kikwete kama kweli si mdini kemea huu upuuzi, hawa watu wanataka kutupeleka kubaya sasa, huyu Mufti nilijua ana busara kumbe nae kama wenzake tu. Hivi yeye hajui kama wakristo wakiamua kuweka rais wao hii nchi haitakaa itawaliwe na muislamu? Yaani nimesoma hii habari nikitetemeka, tunakokwenda sio kuzuri, viongozi mmelianzisha, hasa kikwete, naomba mlimalize wenyewe, mlifikiri ni dogo.
 
Back
Top Bottom