She is not my standard

She is not my standard

Ungekuwa unamfahamu, nadhani usingesema chochote, sasa hivi niko nje ya tz, huko mtaani anatangaa kwamba nkirud namuoa.....afu watu wote wanamjua tabia zake, nshafatwa na baadhi ya wamama watu wazima na kunionya niachane nae na wanasema inawezekana kaniendea kwa mganga, but hua mi siamini hivyo vitu.
kaka kama kweli huna lengo la kumuoa huyu binti, fanya jitihada uachane nae na utafte binti mwingine ambaye ni chaguo lako. vinginevyo atakuganda na utamuoa. nayaongea haya kwa uzoefu niliona kwa rafiki yangu. yaani maelezo yako ni sawa kabisa na yule binti alieolewa na mshikaji.

tulifuatwa mpaka na wamama watu wazima lakin jamaa aliahidi kumuacha lakin baadae arirudi akisema atamuacha wkati ukifika, just bcoz he had no replacement na akisikia ham ya ile kitu, alikuwa hana jinsi, mwishowe akampa mimba na kumuoa.

kama kweli unampenda,(naona husemi hilo lakin deep down kuna kitu umekipenda kwake) muoe lakin uhame mji. usiishi maeneo alikozoeleka otherwise utapigiwa saaaaana. muendeleze kishule mjenge familia, watu hubadilika bhana.
 
mkuu kama kweli huna lengo loloye na huyo binti ni bora ukafuta mawasiliano naye kabisa ili kuepusha usumbufu na kama umekwisha kuonywa na watu wazima sikiliza ushauri wao kisha fanya maamuzi. Kumbuka ndoa mkataba wa kudumu na hivyo ukifanya uchaguzi mbaya wawezajutia baadae
 
Watu tunaropokaga tu ndio maana wengi tunaishi maisha ya kuhama vituo na hatuna amani moyoni hatuna muda kujitazama.kutafakari.tunataka nini
 
hhahhahhaha, nimefurah though inahuzunisha jaman! you made a mistake at the first starting point... kaka hata malaya kuna mda huwa anapenda kwa dhati... either umbadilishe tabia then muoe but ukishindwa achana naye isije ikakucost mbaleni....
 
Sasa ndugu kama Humpendi kwa maana ya kutaka kuishi nae huyu binti hana sababu ya msingi ya kung'ang'ania kuishi na wewe. Kwa profile yake uliyoiweka si jambo la kushangaza. mabinti zetu wengi huamini NDOA ni kipimo cha mwisho cha mapenzi. Mwanaume akitangaza NDOA basi amedhihirisha kuwa ana mapenzi yaliyofikia kiwango husika.

Kwa hali halisi, kuna wengi walio kwenye ndoa wakijuta kuharakisha maamuzi yao, na kuna waliogundua makosa waliyoyafanya wameamua kuachana. laba kama wewe ni mkatoliki, au dini yako inaamini katika ndoa moja tu, kwa maisha ya sasa hivi, watu huoana au kuishi pamoja na watu zaidi ya mmoja kwa kipindi chote cha maisha yao. kwa hesabu za "probability" . makisio ya binadamu mmoja kukutana na binadamu mwengine wakatamaniana yameongezeka, kutokana na uongezekaji wa "mobility". leo hii uko nje, kesho utaenda mkoa flani n.k, binti yuko karne ya 19 wewe uko ya 21.yeye anatafuta kutulia baada ya makosa mengi aliyofanya ya kutembea na kundi la marafiki zako, wewe unatafuta ambaye hajatembea na kundi la marafiki.kimantiki wote mna ndoto za alinacha.

Watu wachache walioana na walio na elimu au uelewa chini sana ya wa kwao wakafanikiwa kukaa pamoja. kwani itafikia muda mtaishiwa vya kuongea, au mtashindwa kujenga hoja za kutatua migogoro yenu zenye kushabihiana uelewa.

Lakini binadamu wako tofauti, ukionacho wewe hakifai wengine wanakitafuta kuchwa, wewe hupendi msichana asiyejua sana, wengine wamewachoka wenza wao machi-know. wewe hupendi kuja ishi na binti anayewaza ngono tu, wengine hutamani wasomi wao wenye digirii tano kama wao wawaze hiyo ngono japo mara 2 kwa mwaka.

unaweza kumpata huyo msomi, asiyewaza ngono masaa yote ukaishia kuleta thredi nyengine hapa baada ya miaka mitano, kuwa waifu ananinyima unyumba namtamani hausigeli n.k.

Ushauri: chambua hili kwa kuangalia unaloweza kufanya ndani ya uwezo wako, STOP being delusional. Huyo unayemuona changudoa, labda ametembea na watu wachache kuliko huyo sista duu usiyemjua vizuri. Mtazame binti kama binadamu, ana vipi vizuri ana vipi vibaya,mtazame past ngono, pia kama hujafika 35. jipe muda, kua kidogo, mawazo yako yatabadilika kidogo utakapokaribia hiyo threshold.utafanya uamuzi mzuri zaidi, ukijipa muda.
 
kwahyo kama hajapata pa kutulia ndo afanye hvyo?

ngoja nijaribu hiyo theory yako
embu jaribu uone kama ni kweli demu akipata sehemu anapata anachokitaka, anagegedwa vizuri wala awezi toka
 
wasomi wa Tanzania hii mnatupa taabu sana. yaani wewe na degree mbili zote bado hujitambui?

She is not your standard! it's okay but why are dating her? it might be craziness!! <<< just thinking >>>
 
Sasa ndugu kama Humpendi kwa maana ya kutaka kuishi nae huyu binti hana sababu ya msingi ya kung'ang'ania kuishi na wewe. Kwa profile yake uliyoiweka si jambo la kushangaza. mabinti zetu wengi huamini NDOA ni kipimo cha mwisho cha mapenzi. Mwanaume akitangaza NDOA basi amedhihirisha kuwa ana mapenzi yaliyofikia kiwango husika.

Kwa hali halisi, kuna wengi walio kwenye ndoa wakijuta kuharakisha maamuzi yao, na kuna waliogundua makosa waliyoyafanya wameamua kuachana. laba kama wewe ni mkatoliki, au dini yako inaamini katika ndoa moja tu, kwa maisha ya sasa hivi, watu huoana au kuishi pamoja na watu zaidi ya mmoja kwa kipindi chote cha maisha yao. kwa hesabu za "probability" . makisio ya binadamu mmoja kukutana na binadamu mwengine wakatamaniana yameongezeka, kutokana na uongezekaji wa "mobility". leo hii uko nje, kesho utaenda mkoa flani n.k, binti yuko karne ya 19 wewe uko ya 21.yeye anatafuta kutulia baada ya makosa mengi aliyofanya ya kutembea na kundi la marafiki zako, wewe unatafuta ambaye hajatembea na kundi la marafiki.kimantiki wote mna ndoto za alinacha.

Watu wachache walioana na walio na elimu au uelewa chini sana ya wa kwao wakafanikiwa kukaa pamoja. kwani itafikia muda mtaishiwa vya kuongea, au mtashindwa kujenga hoja za kutatua migogoro yenu zenye kushabihiana uelewa.

Lakini binadamu wako tofauti, ukionacho wewe hakifai wengine wanakitafuta kuchwa, wewe hupendi msichana asiyejua sana, wengine wamewachoka wenza wao machi-know. wewe hupendi kuja ishi na binti anayewaza ngono tu, wengine hutamani wasomi wao wenye digirii tano kama wao wawaze hiyo ngono japo mara 2 kwa mwaka.

unaweza kumpata huyo msomi, asiyewaza ngono masaa yote ukaishia kuleta thredi nyengine hapa baada ya miaka mitano, kuwa waifu ananinyima unyumba namtamani hausigeli n.k.

Ushauri: chambua hili kwa kuangalia unaloweza kufanya ndani ya uwezo wako, STOP being delusional. Huyo unayemuona changudoa, labda ametembea na watu wachache kuliko huyo sista duu usiyemjua vizuri. Mtazame binti kama binadamu, ana vipi vizuri ana vipi vibaya,mtazame past ngono, pia kama hujafika 35. jipe muda, kua kidogo, mawazo yako yatabadilika kidogo utakapokaribia hiyo threshold.utafanya uamuzi mzuri zaidi, ukijipa muda.

Thanks bro..
Huyu angekua anauweza kubadilika nisingepost huu uzi hapa, tatizo ni kutokubadilika kwake, utamwonya atakusikia but ukiondoka nae kaanza.
kuna siku nlimwachia vunguo za kwangu nkasafiri mkoa wa karib but sikumwambia nakuja lini, suku ya kurudi nkafika kwangu nkakuta kumefungwa, nkampigia simu, akanambia yuko kwangu anaangalia TV, mh..kucheki milango imefungwa...nkampigia tena na kumwomba anipatie funguo zangu kwani niko kwangu na milango imefungwa. kumbe alikua mahali anapata bia.
 
kaka kama kweli huna lengo la kumuoa huyu binti, fanya jitihada uachane nae na utafte binti mwingine ambaye ni chaguo lako. vinginevyo atakuganda na utamuoa. nayaongea haya kwa uzoefu niliona kwa rafiki yangu. yaani maelezo yako ni sawa kabisa na yule binti alieolewa na mshikaji.

tulifuatwa mpaka na wamama watu wazima lakin jamaa aliahidi kumuacha lakin baadae arirudi akisema atamuacha wkati ukifika, just bcoz he had no replacement na akisikia ham ya ile kitu, alikuwa hana jinsi, mwishowe akampa mimba na kumuoa.

kama kweli unampenda,(naona husemi hilo lakin deep down kuna kitu umekipenda kwake) muoe lakin uhame mji. usiishi maeneo alikozoeleka otherwise utapigiwa saaaaana. muendeleze kishule mjenge familia, watu hubadilika bhana.

aksante mkuu..niko kwenye wakat mgu, lakini nimepata suluhisho ambalo litaniweka huru
 
Lakin huoni kama ww ndo uliyekosea toka mwanzo? ulijua kabisa kwamba hujamsimamisha ww, ulijua kwamba elimu yake ni Form 4 na ww una degree 2. Haya muoe sasa maana yeye kakupenda na kama Vp muendeleze kielimu ili asiwaze ngono.

Hata mimi nakuunga mkono mya kwa mya, kwakuwa mpaka hapo hoja za huyo ndugu hazina mashiko zaidi ya kuzingatia huu ushauri uliompa.
 
Huwa najuta kwa makosa kama hayo, but amini nilisemalo mimi, binti hana wazo lolote zaidi ya penzi, alikua kicheche kama asemavyo yeye, but anakiri nimembadilisha sana, lakini lengo langu halikua kumwoa, kwani ntaangaliaje washkaji ambao woote wamepita? hebu fikiria kama wewe ndio mimi..
Hao washkaji utawaangalia kama unavyojiangalia wewe kwakuwa walichokuwa wanafanya na wewe ndio hicho hicho ulikuwa unafanya, sasa bahati nzuri katika wote kakuchagua wewe. Sasa unamkataa aende kwa nani atakayekuwa na mawazo tofauti ya uliyo nayo wewe? muoe atakuwa mke bora sana kwako huyo kwakuwa inaonesha kakupenda kweli
 
Nawe punguza kubana, kakuona umekaa empty tena kihasara hasara ndio maana binti akaamua achangamkie fursa. Degree 2 bado hujaoa tu? By the way, akiamua kukukoleza na mahaba ya dhati hata hizo degree utasahau, nini tofauti ya elimu kwenye mapenzi bwana!
 
Wewe Endelea Tu Kuwa Nae Mpaka Siku Atakapo Kunywa Tetrovote. Nawewe Ukaolewe Jela. Manake Nakushangaa. Huyo Demu Anaonekana Wazi Bado Ni Idiot. Na Heading Yako Ina Majibu Yako.
 
ukiwaza harakaharaka unaweza ukawa sahihi mkuu, lakini kumbuka vijana tunapitia mambo mengi ya hatari, lakini mwisho wa siku inabidi utulie na ufanye maamuzi kwa ajili ya viumbe(watoto) ambavyo ukikosea tu vitateseka kwenye hii dunia kwa sababu ya makosa yako(baba). ukiangalia katika hili nadhani hakuna haja ya kuoa mahali ambako unapajua si sahihi. aksante kwa mchango wako.
 
Wewe Endelea Tu Kuwa Nae Mpaka Siku Atakapo Kunywa Tetrovote. Nawewe Ukaolewe Jela. Manake Nakushangaa. Huyo Demu Anaonekana Wazi Bado Ni Idiot. Na Heading Yako Ina Majibu Yako.

Tatizo ni moja tu bro, Hapa nlikua natafuta au njia sahihi ya kutekeleza heading yangu bila kumuumiza yeyote, maamuz binafsi wakati mwingine yanaweza yasiwe sahihi, hivyo nlitaka nipate na wenzangu mnashaurije? vile vile itawasaidia wengine ambao wana tatizo kama langu ...aksante
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom