Tetesi: Sharti Moja kubwa waliopewa viongozi waliofika Ikulu ni hili hapa

Unayo ongea ni ukweli kabisa bila hata kuambiwa kama unaakili utajua kabisa kuo ilo ndio game linalo enda kuchezwa acha nisema rip kwa chadema atae bisha atakua hajui kuchambua mambo yani ngoma inaenda kupingwa juu chin chadema lazima iminywe alafu vyama vingine vinapandishwa bai Bai ruzuku msishangae mboe kuunga juhud mda si mrefu sio mbowe tu hata baadh ya wabunge wengine watakao hofia kukosa kurud bungeni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna point unaimiss, iko hivi, Magufuli anajua UKAWA ukiwepo wapinzani wataachiana majimbo, hivyo upinzani kushinda itakuwa rahisi zaidi, sasa Magufuli alichofanya ni kuwaruhusu hao kina Mbatia na wenzake kusimamisha wagombea nchi nzima ili wao wapinzani wagawane kura hivyo CCM ishinde kirahisi, but sio kwamba hao kina Mbatia wataachiwa majimbo washinde kirahisi, NO. wanatumika tu.

Inshort Magufuli anaiogopa CDM, anaijua nguvu ya CDM ndio maana mwanzo walijitahidi kuleta propaganda za kumzuia Mbowe asichaguliwe mwenyekiti, wakashindwa, sasa ndio wamekuja na hili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
CDM ijiandae na iandae Wagombea wenye nvuto hasa make mwaka huu kuna vyama vitawezeshwa kusimika wagombea nchi nzima.
Kiuhakika, kukiondolea mzigo wa 'UKAWA" ni baraka kwa CHADEMA, sioni kwa nini walitegemee hilo ambalo ni mzigo mzito kwao.

Wanachotakiwa kufanya CHADEMA ni kuhakikisha wapo imara katika majimbo yote na hakuna hata nafasi moja watakayoacha kumweka mtu wao aigombee, akipambana na yeyote atakayewekwa kuwa kipingamizi kwao.
 
Pia kuna swala la wao kuanzia sasa kuto kusumbuliwa iwe na Wakuu wa wilaya au Mikoa au Polisi.Hivyo usitarajie kuona either Lipumba au Mbatia au Zitto Kabwe akisumbuliwa kuanzia sasa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu tunashukuru kwa hii habari, japo ingependeza kama ungeeita tetesi. Ni hivi, cdm ndio chama cha upinzani chenye wafuasi wengi na mvuto zaidi na hilo halina mjadala. Kwa sisi wenye mtazamo wa mbali tulisikitishwa na ule muungano wa Ukawa kwani athari zake tulizitarajia na sasa zinatokea, na tatizo lingine kubwa la Ukawa ilikuwa ni kumpokea Lowassa na kumpa nafasi adhimu. Ikumbukwe kuwa CHADEMA ndio chama cha siasa kilichofanya kazi ya siasa kuanzia 2010-2015 kwa asilimia kubwa kuliko chama chochote cha siasa ikiwemo ccm, na chenyewe ndio kilikuwa mbeleko ya hivyo vingine.

Nini kifanyike, cdm ikubali kuwa muungano wa vyama vya siasa haukuwa na wala hauna tija kwani kila chama kina mtazamo wake, na sasa isiingie kwenye malumbano yoyote na hivyo vyama vilivyokuwa ndani ya Ukawa, viwaache wafanye watakacho kwani cdm ndio yenye watu. Wao wapaze sauti wawezavyo kudai tume huru ya uchaguzi, na iwapo hakutakuwa na tume huru ya uchaguzi wachukue maamuzi magumu. Bila cdm hakuna mvuto wa siasa za ushindani, huo ndio ukweli. Ni swala la cdm kujua ukweli huu na wala wasipanic, hii hali ya siasa za kuchomekea ni kujaribu kuua nguvu ya cdm kwani Magufuli na ccm wanaijua ukweli, ni suala la muda tu na cdm itasimama vyema.
 
Chama dola, kutoka afrika.

Mwafrika si m bunifu kwa hiyo njia rahisi kwake ni kutumia madaraka vibaya ili mkono uende kinywani.

Mwafrika hataki kuuchosha ubongo ili kujipatia riziki yake
tapatalk_1583317069482.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
MURUSI,
Hili ni andiko lenye uzito; lenye ushawishi mkubwa kuaminiwa kuwa kweli.

CHADEMA hawapotezi chochote kwa kutokuwepo kwa UKAWA.

Inawabidi wajizatiti tu kishujaa kuikabili kazi kubwa iliyo mbele yao.

Kazi yao kubwa ni kufanya kazi na wananchi na kujihami na hujuma za kipuuzi zinazofanywa dhidi yao.
 
The golden question is;

Kwanini waachane na umoja wa Vyama vyao/ UKAWA?....

Who benefits from that arrangement and how?.

tukijaribu kupata majibu hapo labda ndo tunaweza pata picha kamili
Wazushi hao
 
Nyuma ya keyboard watu huwa na ujasiri sana. The real man isn't existent in real life except a hypothetical and hypocritical shadowy being gimmicking nyuma ya PC au simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo 'keyboard' ndizo silaha pekee walizonazo kwa sasa.

Ukitaka kujua walivyo majasiri hasa kuliko hao wa upande wa pili, zigawe zile bunduki zetu tulizowakabidhi waliozishika sasa hivi, ambao wewe ndio unaowaita 'realmen'.

Ukiweza kufanya hivyo, hapo utakuwa na haki ya kujua 'realman' ni yupi.
 
Back
Top Bottom