Tetesi: Sharti Moja kubwa waliopewa viongozi waliofika Ikulu ni hili hapa

MURUSI

JF-Expert Member
Jun 25, 2013
4,482
8,694
Kuna jamaa ninae muamini kabisa na ni kiongozi kutoka moja ya Chama ambacho viongozi wao alikuwa ikulu Jana amenieleza ukiachana na mambo ya auchaguzi kuwa huru na wa haki kuna Shariti moja wamepewa na anaamini ni wote,
Shariti kuu walilo pewa ni kuachana kitu kinacho itwa UKAWA, yaani ili kuwe na unafuu kwa hivyo vyama waachane na miungano hasa na CHADEMA.

Walisisitiziwa hasa kwenye Suala la kuachiana majimba ya Ubunge na Udiwani, kila Chama kisimamishe wagombea nchi nzima kwa Udiwani na Ubunge.

Wamehakikishiwa msaada wa kuwawezesha kusimika wagombea nchi nzima, haijawekwa wazi ni aina gani ya msaada watakao pewa.

Kwa NCCR Mageuzi tiyari kazi isha anza na Mbatia atazunguka nchi nzima kwa Kazi hiyo na muda wowote Lipumba naye ataanza na kufuatiwa na ACT Wazalendo.

Ndo maana jana tukaona Mbatia anasema ataweka wagombea nchi nzima na pia Lipunba alisha weka wazi hilo na muda si mrefu ACT nao wataweka wazi hilo.


Hivyo swala la kwamba wamezungumzia Uchaguzi huru na wa haki ni kijisehemu tu.

Hao ndo wapinzani wetu wakiongzozwa na Zitto Zuber Kabwe.

CHADEMA ijiandae na iandae Wagombea wenye nvuto hasa make mwaka huu kuna vyama vitawezeshwa kusimika wagombea nchi nzima.

Mjumbe hauwawi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu inaonekana Magu anakihofia sasa ni kitu gani hakuna anaye jua, alicho niambia kwa sasa wanaadaa ratiba zao za kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kuandaa wagombea wa Udiwani na Ubunge
The golden question is;

Kwanini waachane na umoja wa Vyama vyao/ UKAWA?....

Who benefits from that arrangement and how?.

tukijaribu kupata majibu hapo labda ndo tunaweza pata picha kamili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MURUSI,

Mjumbe kweli hautauawa ila nimetafuta emoji ya dole la kati nimekosa ulitakiwa ukawaonyeshe wote waliokubaliana watu wengine mpaka leo hawajulikani waliko, wengine ni vilema na zimebaki siku ndio wakubaliane hivi.
 
Yaani ukiwafuata wanasiasa unaweza wehuka, hawajielewi yaani hapo katonge kidogo tu misimamo yao yote wameiweka pembeni.

Nani atamkosoa aliyemadarakani?

Mbona wanajirahisi hivyo kwa maslahi mapana ya Taifa?

Wameonjeshwa maziwa, wamesahau mbio zao za kuanzisha upinzani!

Shame on them if it happens to be true


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ndo kazi inayotakiwa kufanywa na vyama vyote vya siasa mwaka huu.

Usitufanye wajinga we popoma mkubwa
 
Back
Top Bottom