Sharif Hamad adondosha chozi...!

Sharif Hamad adondosha chozi...!

Ukweli Hamad ni kifaa CCM wamekubali kuwa kuna vichwa hapa nchini havijafanyiwa repair yaani origino kabisa sio kichwa cha slaa kina viraka kibao UDINI,UKABILA,UBINAFSI NA................Zanzibar ni moja na wazanzibari ni wamoja daima ubabaishaji mwiko.

WE EL MADRASA pia eeeeeeeehhhhhhhhhhh nilikuwa sijui...
 
CCM B huyo hana lolote na kila kitu kilipangwa maana hata yeye alijua hilo...
 
Nilisikitika hata mie baada ya kutangazwa matokeo yale, japo ndio hivyo ilishatamkwa Dr. Ally M. Shein Ndio Rais Mteule wa Zanzibar.

Hamad alipoitwa alipongeza ushindi huo japo alitamka dhahiri mbinu chafu za baadhi ya watendaji wa tume ya uchaguzi ( ZEC )

Hakika kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwake, aliamua kukaza moyo na kutoa kauli ya mdomoni kuwa Dr. SHEIN ametawazwa kuwa Rais na alisisitiza kwamba ktk uchaguzi huo hakuna mshindi yaani kama ungelikuwa mpira wa miguu ni matokeo ya sare au suluhu baina ya CUF na CCM.

Pembeni ya hapo kwa wale tulomtathimini kwa undani Maalim hasa usoni, alikuwa si yule Maalim mcheshi, mchangamfu na anayejiamini.

Alifanya kila jambo kama amelazimishwa au inambidi afanye hivyo kwani hakukuwa na njia mbadala.

Hisia na Mtazamo halisi wa Hamad (Sharif) umejionesha zaidi ktk machozi yalokuwa yakimtoka kila alipokuwa akizungumza, yalimchuruzika kwa vipindi japo aliweza kujikaza kisabuni asiangue kilio kikubwa.

Pole sana Hamad kwa kuumia, mie niliyaona machozi yako yalonipa ujumbe fulani ktk maisha.

Du! watu kweli tunajua kuumba maneno, eti "machozi yalokuwa yakimtoka"! Kama vile na sisi hatukuona TV! Tusimsingizie ni mmoja kati ya wanasiasa wachache walioonyesha ukomavu mkubwa, apewe his due credit
 
Zanziba hakuna mshindi wala mshinda bali ni ushindi wa wazanzibar wote mwingine ni umbeya na upuuzi hakuna zaidi ya hili wazanzibar hatutaki uchokozi wala uchochezi.
 
Ndugu zangu, Maalim aliwahi kuwa waziri kiongozi na hivyo huwezi kusema ana furaha ya kuwa makamu wa rais. Nadhani kilichowaumiza ni mfumo mzima wa bara kuamua nani awe rais wa visiwani kwa kutumia nguvu za dola na uchakachuaji wa matokeo. Ni bara iliyopekeleka police wengi waliosababisha vurugu na mauaji 2001.
Hali hii ikiendelea kuna siku hicho kinachoitwa amani na wengi kitageuka maafa! Ukizoea kuwanyang'ana watu haki zao tambua kuwa iko siku nguvu ya umma itazidi nguvu ya mabomu
 
Machozi ya mamba hayo, mwanamapinduzi huwa hakubali kirahisi hivyo, lazima kuna ahadi kapewa ama ni huo u makamu rais. Nataka niwaambie wazanzibari kuwa kwa kukubali kuvunja upinzani mmeiangamiza Zanzibar. Katika maswala ya utawala nilipitia kauli ifuatayo "Where there's no conflict, there's no development." Mahali ambapo hakuna migongano hakuna maendeleo. Kinachotakiwa ni regulate migongano isifike mbali sana na kuleta madhara. Hii serikali ya umoja wa kitaifa itawazidishieni umaskini, maana sasa hakuna wa kumwambia serikali umekosea. Haya shauri yenu.

I like that..."crocodile tears"! Kwa hiyo Maalim katuzuga?
 
Hamad alilia jamani! Au watu wengine huangalia midomo na mikono tu? Na kama watu mnakumbuka vizuri ni kwamba yule mchukua picha wa TBC Au ni Televisheni gani alijitahidi kuchezea kdogo rangi ikawa kama kahawia ili kupoteza uhalisia bt mie nilijaaliwa kutazama usoni kwa hamadi na hali nkiyasikiza maneno yake alokuwa akiyatoa...

Alilia Sheik... Alililia Hamadi jamani tuelewane.. SAWA SAWAA!
 
hakutokwa na machozi ila aliongea kwa uchungu sana kuilaumu tume ya uchaguzi,hapa alidhihirisha kubali yaishe au kosa vyotevyote au aliye juu mpandie hukohuko
hakujililia yeye bali umati uliokuwa nje ya hoteli ya bwawani, je wadhani angelikataa matokeo ya ZEC nini kingalitokea pale??? yaani kuishi nchi hizi:A S angry:
 
Hisia na Mtazamo halisi wa Hamad (Sharif) umejionesha zaidi ktk machozi yalokuwa yakimtoka kila alipokuwa akizungumza, yalimchuruzika kwa vipindi japo aliweza kujikaza kisabuni asiangue kilio kikubwa.

Pole sana Hamad kwa kuumia, mie niliyaona machozi yako yalonipa ujumbe fulani ktk maisha.
Pia huwa yapo machozi ya furaha, Umakamo wa Kwanza wa Rais, sii haba!, ni mwendo wa ving'ora!.
 
hakujililia yeye bali umati uliokuwa nje ya hoteli ya bwawani, je wadhani angelikataa matokeo ya ZEC nini kingalitokea pale??? yaani kuishi nchi hizi:A S angry:
Ndio maana nimeshauri, Dr.Slaa awepo kesho pale karimjee wakati wa kutangazwa kwa matokeo.
 
Machozi ya mamba hayo, mwanamapinduzi huwa hakubali kirahisi hivyo, lazima kuna ahadi kapewa ama ni huo u makamu rais. Nataka niwaambie wazanzibari kuwa kwa kukubali kuvunja upinzani mmeiangamiza Zanzibar. Katika maswala ya utawala nilipitia kauli ifuatayo "Where there's no conflict, there's no development." Mahali ambapo hakuna migongano hakuna maendeleo. Kinachotakiwa ni regulate migongano isifike mbali sana na kuleta madhara. Hii serikali ya umoja wa kitaifa itawazidishieni umaskini, maana sasa hakuna wa kumwambia serikali umekosea. Haya shauri yenu.
Migongano si ya nguvu bali hoja. Naamini hivyo ndivyo itakavyokuwa kwani vyama hivi japo vyote vinataka maendeleo ya Wazanzibari, mikakati yao ni tofauti. Maendeleo yatakayotokana na maridhiano ni kuaminiana na kuweza kufanya kazi pamoja. Kisera itakuwa ni maridhiano tu (compromis). kwenye maswala wanayotofautiana
 
Hakuna sehemu Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa Shein ameshinda ,hebu rudieni kikamilifu hiyo hotuba ya Maalim Seif na muisikilize kwa kituo ,punguzeni peresha mnaposikiliza maneno ya Seif ,kuna onyo flani aliwaambia kuwa wasicheze na utulivu ulioonyeshwa anytime kunaweza kukazuka fujo jipya ,hivyo kila mtu atunze mwenendo wake kwa maana hakuna kubezana.
 
tatizo ni kwamba Hamad hakusoma alama za kijiografia ya siasa za visiwani yeye
kafanyika chambo tu we tangu lini paka na wakala chakula pamoja?
wapi uliona mbuzi na simba wanacheza pamoja na kuruka kwa furaha?
akauza uzaliwa wake wa asili kwa kukubari muafaka wa kinafiki, na kuwakumbatia
majangili kifuani pake ndiyo ajue sasa kuwa hawa ccm hawafai hata kwa dawa
 
Ukweli Hamad ni kifaa CCM wamekubali kuwa kuna vichwa hapa nchini havijafanyiwa repair yaani origino kabisa sio kichwa cha slaa kina viraka kibao UDINI,UKABILA,UBINAFSI NA................Zanzibar ni moja na wazanzibari ni wamoja daima ubabaishaji mwiko.

tatizo lenu wazanzibar unafiki tu, hakuna zanzibar moja bali kuna pemba moja na unguja moja
 
tatizo lenu wazanzibar unafiki tu, hakuna zanzibar moja bali kuna pemba moja na unguja moja

Na Huo ndio Ukweli haya ya kujiita Uzanzibar ni Unafiki tu, siri zenu ziko moyoni, ni kheri sie twaweza kujiita Watanzania kwani kiasi twajitambua hasa na Utanganyika wetu upo lakini kwa mbali sanaa! Nyie wenzetu mnaendelea kurithisha kizazi hadi kizazi, hatujisifu bali sie tumejitahidi japo nasi tunayo yetu ya chinichini.
Mjaribu kurekebisha na kuwa na upendo wa kweli la sivyo huo ufukao utawaka siku moja.
 
Nadhani kwa Sharrif Hamad haya ni machozi ya furaha maana kama ni kwa uchungu huko nyuma angelia sana pale uchaguzi ulipotokea kwenye watu kufa na kuwa wakimbizi. Na vilevile halii kwa sababu ya umakamu, la hasha! ni kwasababu anaona ametoa mchango mkubwa sana kuwaletea amani wazanzibar wote na kuafanya wawe wamoja na hicho ni kitu cha thamani sana kwake.
 
na habari iliopo ndani ya nyumba CCM hawamtaki awe Makamo wa Rais na wamekitaka chama cha CUF kupeleka majina matatu na wao wachague moja, huenda mzee Duni au Jussa akawa Makamo wa Rais
 
Zanziba hakuna mshindi wala mshinda bali ni ushindi wa wazanzibar wote mwingine ni umbeya na upuuzi hakuna zaidi ya hili wazanzibar hatutaki uchokozi wala uchochezi.

Ingekuwa hivyo basi wangeapishwa marais wawili zanzibar. Ninachojua CCM wameshinda zanzibar na ndio maana ameapishwa Dr. Shein, na siyo Maalim Seif, kuwa rais wa baraza la mapinduzi zanzibar. Haya mengine kuwa hakuna mshindi zanzibar ni maneno ya kufarijiana tu.
 
Yeah nakubaliana nanyi nyote kuwa hakuna mshindi na Seif kumwaga chozi, what i think kwmamba alifahamu dhuluma na hila aliyofanyiwa ila kwa maslahi ya taifa akaamua bora yayesheeeeee cha kufahamu kuwa this time amekubali yayeshee kwa kuwa tu anajua kuwa anaenda kuwa makamu wa kwanza wa raisi wa SMZ labda anaamini ataweza ku impose yale anayotamani yafanyike ZNZ
 
Hamad alilia jamani! Au watu wengine huangalia midomo na mikono tu? Na kama watu mnakumbuka vizuri ni kwamba yule mchukua picha wa TBC Au ni Televisheni gani alijitahidi kuchezea kdogo rangi ikawa kama kahawia ili kupoteza uhalisia bt mie nilijaaliwa kutazama usoni kwa hamadi na hali nkiyasikiza maneno yake alokuwa akiyatoa...

Alilia Sheik... Alililia Hamadi jamani tuelewane.. SAWA SAWAA!

Haijalishi kuwa alilia au hakulia ukweli ni kuwa hatimaye alikubali kile alichokuwa akikikataa katika chaguzi zote kwa kudai kuwa kura zimeibwa. Na ukweli mwingine ni kuwa Maalim Seifu na chama cha CUF wameshindwa kuupata urais wa zanzibar na ni CCM ndiyo chama tawala zanzibar.

Hii imethibitisha kuwa kumbe ule uliokuwa ukiitwa kuwa ni mpasuko zanzibar ilikuwa ni uzushi tu wa Maalim Seif Sharif Hamad na chama chake cha CUF. Mkapa alikuwa sahihi aliposema kwenye kampeni ya CCM ya Jangwani kuwa siku zote wao walitaka serikali ya umoja wa kitaifa zanzibar lakini kwa sharti kuwa lazima itawaliwe na CCM.
 
Back
Top Bottom