Share intaneti na rafiki yako kwa Bluetooth

Share intaneti na rafiki yako kwa Bluetooth

Tumia intaneti kwa mfumo wa Bluetooth

Umeshawahi kutumia intaneti kwa mfumo wa Bluetooth kupitia simu yako ? Najua wengi tunaotumia simu kwenye mambo mengi tu ila wengi hatujui tunaweza share intaneti kwa kutumia Bluetooth.

Watu wengi tunatumia njia ya hotspot kuweza ku share intaneti kwenye vifaa vingine lakini sio lazima unaweza tumia Bluetooth kuweza kushare intaneti kwenye kifaa kingine kama vile simu , kompyuta pamoja na tablet.

Kwenye simu zetu Kuna kitu kinaitwa Bluetooth tethering, ni njia moja wapo ya kutumia mfumo wa wireless kuweza kusambaza upendo wa intaneti kwenye vifaa vingine kupitia Bluetooth.

Tusema una bando Kuna mtu anahitaji kushare na wewe kidogo sio lazima uwashe hotspot unaweza tumia tu Bluetooth kuweza kushare intaneti na wengine.

Wala uhitaji password kuweza kuunganisha kwenye ivyo vifaa unafanyaje ku share intaneti kwa kutumia Bluetooth kupitia simu yako [emoji116]
• ingia setting kwenye simu yako
• Kisha hotspot & tethering
• utagusa kwenye Bluetooth tethering
• hakikisha data Iko Kisha kwenye simu nyingine inahitajika kupata intaneti awashe tu Bluetooth ikishakua connected anaweza tumia intaneti bila password

Pia unaweza tumia njia hii kuunganisha na kompyuta yako kuweza kushare intaneti kwenye kompyuta kama upendi watu uwatajie password ya hotspot yako.

Umeshawahi kutumia hii njia au ndo unasikia Leo tuachie maoni yako ? View attachment 2643734
hii natumiaga sana ku connect na pc through usb iyo kwa simu nmeijua leo thanks
 
Kwa wale wanaotumia WI-FI tufanyaje ?

Pembeni yako kuna Mtu anatumia Wifi , Alafu Wewe hujui Password yake ....
Unataka Upate internet , vipi hii njia inatumika ?
 
Kwa wale wanaotumia WI-FI tufanyaje ?

Pembeni yako kuna Mtu anatumia Wifi , Alafu Wewe hujui Password yake ....
Unataka Upate internet , vipi hii njia inatumika ?
Kuna kitu wanaita wifi map
Wenye ujuzi zaidi watakuja kueleza zaidi
 
Kwenye taasisi kama college,ambako Wi-Fi inaweza kutumika,hivi huwezi kutumia pasipo kutumia password zao?Mwenye maujanja,atujuze.
 
Kwa wale wanaotumia WI-FI tufanyaje ?

Pembeni yako kuna Mtu anatumia Wifi , Alafu Wewe hujui Password yake ....
Unataka Upate internet , vipi hii njia inatumika ?
Chukua simu yake utajua utatumia lugha gani kumshawishi akupe simu afu nenda sehemu ya Wifi yake na simu yako nenda sehemu ya wifi kisha scan QR Code ya WiFi yake hapo utajoin bila kujua wala kuhitaji password sema mwenye network anaweza kustukia na akablock au kuchange password hapo itakubidi kuscan tena..
 
Back
Top Bottom