Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,888
Theopista Nsanzugwanko
Daily News; Friday,February 22, 2008 @06:04
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, amewasili katika ofisi yake mpya na kuahidi kutokomeza ufisadi bila kumuonea huruma mfanyakazi ye yote wa wizara hiyo atakayejaribu kuweka doa katika wizara hiyo.
Pia waziri huyo aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikikiano ili kuhakikisha wanarudisha imani kwa wananchi, na akasema hatamvumilia mtu ye yote mkorofi ambaye atasababisha aibu katika wizara hiyo.
Akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo katika chuo cha Utalii Dar es Salaam leo, Mwangunga aliwataka wafanyakazi kukabiliana na changamoto za kuhifadhi na kuzifanyia biashara raslimali za taifa ili kukuza uchumi na si kwa nia ya kujinufaisha wao binafsi.
Nilipoteuliwa kuwa waziri wa wizara hii kuna watu walionipa pole kutokana na unyeti wake huku wakidai kuwa imejaa mafisadi, lakini napenda kuwahakikishia kuwa yote yaliyopita tuyaache na kuanza upya kwa kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano kwani sitamvumilia mtu yeyote atakayejaribu kuleta ukorofi kwa nia ya kuitia doa wizara, alisema.
Aliwataka wafanyakazi kufanya kazi zao kwa kuzingatia misingi minne ikiwamo kujitoa mhanga katika kazi, kuipenda kazi na kuwa wabunifu ili kukabiliana na utandawazi, kuwa na bidii ya kazi na uadilifu kutokana unyeti uliopo katika wizara hiyo.
Aliwataka wafanyakazi wa idara ya misitu kubadilika kutokana na malalamiko mengi wanayopata kutoka kwa wananchi kwa kukataa hongo kutoka kwa wafanyabiashara ambazo zinawaondolea heshima pale wanapogundulika kudhulumu raslimali za taifa.
Waziri Mangunga aliwataka wafanyakazi kushirikiana katika idara zote ili kuweza kufanya kzi kwa ufanisi na kukusanya mapato zaidi kitendo kitakachowafanya kuwa kifua mbele kwa Rais hivyo kuongezewa fungu katika bajeti yao.
Awali, Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ezekiel Maige, aliwaomba wafanyakazi hao kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuweza kukabiliana na changamoto zilizopo za kupambana na ufisadi na kurejesha imani kwa wananachi kwa kuhakikisha rasilimali za taifa zinatumika ipasavyo.