Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 21 Mei, 2024 amefanya kikao na Watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
866
547
WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI WA WIZARA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 21 Mei, 2024 amefanya kikao na Watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Akiongea na wafanyakazi hao wa Wizara yake, Waziri Tax ametoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kila mtumishi kwa nafasi yake atekeleze majukumu yake kwa wakati na kwa kujali muda na matokeo chanya na yenye tija kwa Wizara na Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akatumia fursa hiyo ya kuongea na Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi kwa kuipongeza Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Wizara ya Ulinzi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa tija.

Dkt. Stergomena Tax ametoa wito na maagizo kwa wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na JKT kufanya kazi kwa utendaji unaozingatia muda na matokeo na akasisitiza wafanyakazi kufanya kazi bila kusubiri kusukumwa.

Pia, Waziri Tax aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kufanya kazi kwa weledi na kufanya uchambuzi wa kina ili kuifanya Wizara ya Ulinzi kuendelea kuwa bora katika utendaji wake wa kazi na akasisitiza umuhimu wa Uandishi wa kiuchambuzi.

Vilevile Waziri wa Ulinzi akatoa wito kwa wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na JKT kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa hili ni takwa na haki ya kila Mwananchi kushiriki kikamilifu.

Awali akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na JKT ili aongee na Watumishi wa Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe alimshukuru Waziri Tax kwa utaratibu wake aliojiwekea wa kukutana na kuongea na watumishi ambapo alisema katika kikao cha kwanza yapo maelekezo aliyoyatoa na mengi yamefanyiwa kazi hadi kufikia sasa.

Wakati huohuo Waziri wa Ulinzi amekabidhiwa Vikombe vya Ushindi wa Michezo ya Mei Mosi kwa mwaka 2024 na Afisa Michezo wa Wizara Bi. Lisamarie Robert, ambapo Wizara ya Ulinzi iliibuka mshindi wa pili wa jumla, baada ya kushinda Kikombe cha mshindi wa kwanza mpira wa pete, Mshindi wa kwanza mchezo wa Vishale (Darts) na mshindi wa pili riadha na mshindi wa tatu mchezo wa bao.

"Nawapongeza Viongozi wa Michezo na Wanamichezo kwa kufanikiwa kupata ushindi wa pili wa jumla na kutuletea Vikombe Saba kwa Michezo ya Mei Mosi Taifa" alisema Waziri Tax.

Waziri Tax akaongeza na kuisisitiza umuhimu wa michezo katika sehemu za kazi na katika jamii kwa jinsi ambayo ushiriki katika michezo unavyosaidia kutunza afya za wafanyakazi kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza hiyo kasisitiza wafanyakazi waendelee kujitokeza kwa wingi kufanya mazoezi.
 
Attachments

 • 20240522_060115_InSave_1.jpg
  20240522_060115_InSave_1.jpg
  64.1 KB · Views: 5
 • 20240522_060115_InSave_0.jpg
  20240522_060115_InSave_0.jpg
  77.9 KB · Views: 4
 • 20240522_060115_InSave_6.jpg
  20240522_060115_InSave_6.jpg
  56.4 KB · Views: 4
 • 20240522_060115_InSave_8.jpg
  20240522_060115_InSave_8.jpg
  64.8 KB · Views: 5
 • 20240522_060115_InSave_7.jpg
  20240522_060115_InSave_7.jpg
  90.5 KB · Views: 4
 • 20240522_060115_InSave_5.jpg
  20240522_060115_InSave_5.jpg
  111.3 KB · Views: 6
 • 20240522_060115_InSave_3.jpg
  20240522_060115_InSave_3.jpg
  89.2 KB · Views: 4
 • 20240522_060115_InSave_4.jpg
  20240522_060115_InSave_4.jpg
  106.8 KB · Views: 4
 • 20240522_060115_InSave_2.jpg
  20240522_060115_InSave_2.jpg
  120.6 KB · Views: 4
Hakuna lolote Wala hakuna jipya.

Jeshi gani la ulinzi limeshindwa kuwakamata Kigogo2014 na Mange Kimambi?
 
WAZIRI WA ULINZI NA JKT AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI WA WIZARA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 21 Mei, 2024 amefanya kikao na Watumishi wa Wizara ya Ulinzi na JKT katika Ukumbi wa Mabele jijini Dodoma.

Akiongea na wafanyakazi hao wa Wizara yake, Waziri Tax ametoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kila mtumishi kwa nafasi yake atekeleze majukumu yake kwa wakati na kwa kujali muda na matokeo chanya na yenye tija kwa Wizara na Taifa kwa ujumla.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa akatumia fursa hiyo ya kuongea na Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi kwa kuipongeza Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Wizara ya Ulinzi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa tija.

Dkt. Stergomena Tax ametoa wito na maagizo kwa wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na JKT kufanya kazi kwa utendaji unaozingatia muda na matokeo na akasisitiza wafanyakazi kufanya kazi bila kusubiri kusukumwa.

Pia, Waziri Tax aliwataka wafanyakazi wa Wizara yake kufanya kazi kwa weledi na kufanya uchambuzi wa kina ili kuifanya Wizara ya Ulinzi kuendelea kuwa bora katika utendaji wake wa kazi na akasisitiza umuhimu wa Uandishi wa kiuchambuzi.

Vilevile Waziri wa Ulinzi akatoa wito kwa wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na JKT kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa hili ni takwa na haki ya kila Mwananchi kushiriki kikamilifu.

Awali akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na JKT ili aongee na Watumishi wa Wizara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na JKT Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe alimshukuru Waziri Tax kwa utaratibu wake aliojiwekea wa kukutana na kuongea na watumishi ambapo alisema katika kikao cha kwanza yapo maelekezo aliyoyatoa na mengi yamefanyiwa kazi hadi kufikia sasa.

Wakati huohuo Waziri wa Ulinzi amekabidhiwa Vikombe vya Ushindi wa Michezo ya Mei Mosi kwa mwaka 2024 na Afisa Michezo wa Wizara Bi. Lisamarie Robert, ambapo Wizara ya Ulinzi iliibuka mshindi wa pili wa jumla, baada ya kushinda Kikombe cha mshindi wa kwanza mpira wa pete, Mshindi wa kwanza mchezo wa Vishale (Darts) na mshindi wa pili riadha na mshindi wa tatu mchezo wa bao.

"Nawapongeza Viongozi wa Michezo na Wanamichezo kwa kufanikiwa kupata ushindi wa pili wa jumla na kutuletea Vikombe Saba kwa Michezo ya Mei Mosi Taifa" alisema Waziri Tax.

Waziri Tax akaongeza na kuisisitiza umuhimu wa michezo katika sehemu za kazi na katika jamii kwa jinsi ambayo ushiriki katika michezo unavyosaidia kutunza afya za wafanyakazi kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza hiyo kasisitiza wafanyakazi waendelee kujitokeza kwa wingi kufanya mazoezi.
Kuna jipya,au ni kula shushu na posho tu, watumishi wa umma, huwa hawafanyi zaidi ya kile kilichowapa ajira, hawafikirii kuboresha kidogo hata taratibu za kupokea wageni, kuja na mawazo chanya jinsi ya kuborsha, wao ni kusubili salary tu
 
Back
Top Bottom