Shamra shamra za mkutano wa CCM zimeanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shamra shamra za mkutano wa CCM zimeanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Precise Pangolin, Jun 9, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Wanabodi nipo mbagala maeneo ya kizuiani ile kampeni jaza uwanja imeanza gari lenye vipaaza sauti linasumbua wananchi Wana lalamika huu ni muda wa kazi wao hamasisha jangwani mbona mbona Hawawi watulivu Kama wenzao chadema watu Wana waonyesha vidole viwili . Wengine wanasema Chama tawala kinatakiwa kutekeleza ahadi zake wala sio kwenda kukusanya watu jangwani huu ni muda wa vitendo na wala siyo maneno
   
 2. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ili ueleweke vizuri sema AHADI ZAKE
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwa wale wanao fahamu hesabu ndogo ndogo signature yangu itatafaslika vizuri
   
 4. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Mtu atakaye kwenda jangwani atakuwa mwanawazimu mkubwa, kwani ccm ni chanzo cha umaskini tulio nao hapa tz (poverty generator)
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hicho ndio nini?
   
 6. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Huo ubwabwa wao nani atakula? Watu wananjaa sana na shida tupu kwa hyo lazma waende tu lakini mapenz yao yako chadema
   
 7. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,315
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Usijekuta anayeandika hiki ni University graduate.
   
 8. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Waacheni wafu wawazike wafu wao. Siku ya kufa kwa nyani miti yote hutereza ! Watahangaika weeee! Mwishowe watajajua kuwa Watanganyika TUMEWACHOKA & HATUWATAKI TENA !
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  mbona hawapiti mbezi na msasani??

  wanajua huko kuna ma yakhe wengi ndo maana
   
 10. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  siku ya kufa nyani nyani mwenyewe ndio huteleza na siyo miti bhana kwani siku zote huishi na kucheza kwenye hiyo hiyo miti.
   
 11. m

  mbezibeach 2 Senior Member

  #11
  Jun 9, 2012
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naona ndio wameku-release asubuhi hii...wamekutumia usiku kucha halafu..very sory.
   
 12. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  CCM aiwezi kuwa chanzo cha umaskini hapa Tanzani sababu Vijana wengi wa Tanzania awapendi kufanya kazi,wengi uishia kuvuta bangi na kukaa kwenye vijiwe.kwa hiyo wewe unategemea CDM hiki chukua madaraka itafanya kuwagawia pesa,watu wanaoshinda vijiweni ili kuinua Hali nzuri za Wananchi.Mkuu kuwa great thinker acha ukilaza.
   
 13. Z

  Zhu Senior Member

  #13
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania ni mskini kwa sababu ya CCM. Na vijana matajari hapa Moshi ni kwa sababu ya CDM
   
 14. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Ccm wazee wa kucopy na kupaste cdm ilianza vua gamba vaa gwanda ccm ikaja na vua gamba na gwanda vaa uzalendo na "ufisadi".cdm wakaamua kufanya mkutano jangwani uwanja uliokua unakimbiwa na vyama vya siasa ccm nao hao..cdm wameuita jangwan chadema square sikilizen sasa kama magamba hayajaja na jina
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,168
  Trophy Points: 280
  Niko maeneo ya Kimbiji, mabasi ya mekodiwa yanaenda vijijini kuchukua raia.
  CCM bila majeshi ya kukodi ni aibu kubwa Jangwani
   
 16. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Leaderssssssssssssssss powersssssssssssssssssssssssssss
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jun 9, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

  Bila shaka hapo utakuwa umeridhika na ahadi ya serikali ya ccm!

  ​kwa hisani ya mtu wa Tanganyika
   
 18. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkutano wa leo wa CCM ni karata yao nzuri ya kujichimbia kaburi endapo hawatakuwa na majibu yatayowaingia wananchi juu ya mustakabali mzima wa maisha na taifa kwa ujumla.

  Yangu macho, nasubiri saa sita tulitoahidiwa tuanze kuona nini kinajiri uwanjani.
   
 19. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280

  una undugu na Lusinde nini!?
  Naona wote mnayapenda haya maneno ''kujamba'' na ''uharo'' sana.
   
 20. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Elimu za dot com ndo faida ya kuwa na CCM kwa miaka 50
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...