Shame on you US Embassy TZ.

--------

Kuhusu huyo Binti mwenye miaka 16 aliyenyimwa haki yake ya kuwa na familia yake, anaweza kumwandikia barua Senator Hillary Clinton, akalalamika, au mtu yeyote anaweza kuiandika, kwa niaba yake, na kisha kuitisha Press Conference, awaalike BBC na other International news media reps, kisha tusikie majibu yake. Kama hakuna atakayewajibishwa huko Ubalozini, sijui.

Never underestimate the power of the media, the Fourth Estate!


./Mwana wa Haki
mmh mkuu uliyosema ni sawa lakini hapo mwisho naona ni soo,huoni kama yanaweza kuchimbuliwa mengine,maana nnachokumbuka ni kwamba babaake ana student visa,sasa family yooote imfuate huko??lakini poa nadhani kuna mahali kuna tatizo mpaka akanyimwa hiyo visa[/QUOTE]

Babukijana

Sheria ya Uhamiaji ya Marekani HAIKATAZI mwanafunzi mwenye familia kuishi na familia yake akiwa masomoni, ilhali ana uwezo.

Mimi nilisoma Marekani, naielewa vema sheria hiyo.

./Mwana wa Haki
 
Naomba nisaidie kitu kimoja huyo binti ana miaka 16 na kama sikosei atakuwa anasoma sekondary, Hivyo alikuwa anataka visa ya aina gani hasa?? kwa mtazamo wangu kama alikuwa anataka for long stay bas waliona kabisa anataka kusoma Us na kutumia mwanya wa baba mtu! Kama ilikuwa ni visit tuu bas sidhani baba mtu anaweza kumleta binti yake kwa sababu yeye mwenyewe ni mwanafunzi! jaribu kutufafanulia zaidi japo sio mtaalam sna wa Visa nitakusaidia kwa upeo wangu! Pole sna jipe moyo.

Hapa haitakiwi utaalamu wowote.

Mtoto yuko shule na ubalozi haitaki imnyime haki ya mtoto kwenda shule. Jamani hiyo si ndiyo haki?????? Tena haki ya mtoto ya elimu???.

Jinsi umejieleza ndivyo ilivyo na huyo baba yake alipokuwa anajaza fomu kuna namna alijieleza mtoto anamwacha na nani. Sasa yanapokuja tena kumuita mtoto USa, ubalozi wao wanarudi kwenye kumbukumbu zao na kutafakari pia.

Ieleweke pia maofisa wa ubalozi ni wasomi hawakurupuki mzee, pia wanajua ukiwa mwanafunzi unaegharamiwa na serikali ya Tz kuna kiasi amejieleza na kusaini fomu kama mkataba kwa hiyo hizo hela ni kwamba hazitoshi akiongezeka mtu wa pili au wa tatu. Pia wanajua mwanafunzi wa full time studies hana muda wa kufanya kazi. Full stop.

jamaa antaka kuwadanganya na ubalozi kwa asilimia mia wanao uhakika kwani atakuwa alisaidi fomu fulani kuhusu familia.
 
Naijua US imigration policy kwa foreign incommers tangu nikiwa kijana. Nimejilisha YAMINI kwamba marekani is the last choice for me period.

Mnaopapatikia kwenda nendeni lakini mjue kwamba mnakwenda kujidhalilisha hasa kuanzia kwenye maombi ya visa na takataka zinginezo.

Wabongo susieni misaada yao mpaka watakapobadili sera zao za kinyama.
 
Mimi sioni umuhimu wowote mtu kulalamika kuwa amenyimwa viza ya kwenda Marekani. Viza ya Marekani sio haki ya mtu. Na hata kama mtu umenyimwa sasa sijui utafanya nini. Labda uende mahakamani kudai hiyo viza na sijui utaenda mahakama gani?
 
Katika balozi zote hapa nchini US na Canada sio wasumbufu kama kwa mfano UK.Mara moja moja lazima kunatokea an unfortunate incident lakini wengi wanawasifu US kwa kuwa makini ukikamilisha vitu vyote.
 
Kama student visa ya mzazi/wazazi wake imekaribia kuisha inaweza pia ikawa ni sababu mojawapo ya kumnyima huyu mtoto visa. wakijua kwamba hakuna sababu ya mtoto kwenda kama wazazi karibu wanamaliza muda wao....hayo ni mawazo yangu
 
kama jamaa kasema akimaliza kusoma anarudi, ubalozi lazima ushangae mbona anahamisha familia yake yote kule? je huko ni kurudi? au kuhamia?

mtoto ana miaka 16, anatakiwa abaki TZ asome na amalizie shule yake....
kama baba yake analipiwa na serikali atawezaje kumudu gharama za familia....
baba yake wakati anaomba visa lazima atakuwa ameandika sponsor wake watamfadhili nini na nini, halafu sasa hivi inapokuja kuleta watoto ubalozi wanaangalia tu yule baba alivyojaza. ubalozi sio wajinga


je huyo mtoto angefika kule marekani angeendelea na shule wakati baba yake anasoma???
 
Back
Top Bottom