Shambulio la Lissu kupigwa risasi: Polepole aibua mapya

Shambulio la Lissu kupigwa risasi: Polepole aibua mapya

Hujui maana ya shahidi.Pole mwenye dereva anamuamini dereva wake amesema siku akirudi atarudi na dereva wake na siku ya kuhijiwa atahojiwa na dereva wake akiwa kama wakili wake.

Polisi ifanye kazi yake siyo kurukaruka akma maharage yanayochemka
Hahahahahah bavicha kweli vichwa maji.Yani lisu asimame kama wakili wa dereva hahahahahah wakati yy mwenyewe na dereva wake wanatakiwa kuhojiwa.Polepole anajua mengi na ndio hoja ya mcng.mleteni dereva
 
Kwa kauli moja; wameamua kuficha camera kwa kuwa CDM imemficha dereva. Wanadai wakimwaga mboga wao wanamwaga ugari
 
Unawezaje Fanya uchunguz bila kuwahoji wahusika waliokuwepo?au unataka polisi wapige ramli?ttz bavicha lisu na dereva mmewafanya innocent.

Kwa hiyo Lissu alijipiga Risasi?Very stupid argument.Subirini Lissu akirudi atarudi na dereva wake hayo mengine mnajishuku tu?Hata Imran Kombe mlisema mlidhani jambazi baada ya Mkewe kukomaa ndipo mkajidai kwamba Polisi walimfananisha.Ukiwa mwanachama wa Chama Cha Mauaji lazime uwe unaweweseka kila unaposikia Lissu.Poleni sana.
 
kama dereva mmemficha mnashindwaje kuiba kamera za cctv
jibun swali aliyeshambuliwa tunamwona kwenye tv lakin dereva yupo wapi yeye ndio shahidi wa pekee
Kama CDM wanaweza kumficha mtu na serikali ishindwe kumpata, kama nchi hatupo salama.
 
Ana point, kumficha dereva kunaisaidia vp ? Chadema kwenye mikakati yake ?, ahojiwe tu,
CCTV camera hazikuwa na ushahd wa kutosha???
Na Polisi wa lindo walikuwa wapi? Wamehojiwa?? Tulipewa mrejesho wowote juu ya Tukio??
Yaani mnajitekenya alafu mnajilazimisha kucheka!!
Mhaza fhakhazzzzz[emoji48][emoji48][emoji48]
 
polepole.jpg

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenenzi, Humphrey Polepole amefunguka na kuhoji kuhusu kitendo cha Chadema kumficha dereva aliyeshuhudia tukio zima la shambulio la risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na amewataka wananchi wa jimbo la Siha kumhoji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aeleze sababu za kufanya hivyo.

Ametaka kuhoji siri iliyopo inayowafanya Chadema wamfiche dereva huyo wakati anahitajika kuisaidia Serikali kufumbua ukweli na kumjua aliyehusika katika shambulio hilo

Hivi huyu polepole yupo timamu kweli? Akipatikana dereva wa lissu hao watu wasiojulikana watapatikana baada ya kuhojiwa? Vipi dereva wa lissu angekufa ktk shambulio lile ina maana intelijensia ya jeshi la polisi ingekuwa nayo imekwisha?

Siasa za ccm kupitia huyu jamaa ni mufilisi kabisa.

Pole pole amekuwa msemaji wa serikali? Biashara ya kununua watumwa imekwisha? Siwezi kumwuliz akitu kwa sababu naona ana matatizo makubwa.
 
Hebu wacheni kupayuka payuka, hilo ni la ukweli, uchunguzi wa tukio lolote lile kwanza linaanza na waliokaribu na tukio, na kufuatia na wahasimu wake.

Hakuna anayefurahia tendo alilofanyiwa Lissu, sio haki ni dhulma. Kuhojiwa wa dereva na kutoa msaada ni wajib. Anaweza toa maelezo ya muonekano wa mmoja wa hao majangili na mchora akafanya kazi yake.

By law this has to happen na huyu mwanasheria maarufu ameingizwa mwenye.
 
Albadir iliyosomwa Tanga itakuwa imeshaanza kufanya kazi.
 
H. Polepole anatetea tumbo tu. Siasa haijui!!
Mm nadhani Dereva angekuwa shahidi namba moja, na kwa bahati nzuri sana mlengwa amesalimika awe shahidi wa pili ikifuatia sasa na vielelezo vya CCTV, majrani walinzi wa zamu wa eneo husika.
Katika upelelezi huo ndio ungefuatwa
 
Kwa sababu hakufa aje ahojiwe na vyombo vya dola. Kama alikufa asijitokeze!

Very stupid argument,ndiyo sababu vifo vyote vinavyotokea na havipewi uzito unaostahili inasukumiziwa Serikali wakati wahusika wakuu wanajulikana.

Hakuna kesi iliyoisha ikaleta matumaini kwa wahanga,Mauaji ya Dr.Mvungi mpaka leo hakuna kilichojulikana,Mawazo Alphonce ni yale yale na bado mnajitutumua kusema ati Dereva acheni upumbavu sote tunatakiwa kuitaka taasisi inayohusika kufanya kazi yake na si kurukaruka kama maharage yanayochemka.

Mnadhani kuutetea uovu ni sifa ila kuna siku mtajutia haya,maana kwenye hili kama watanzania tulitakiwa tuwe wamoja ili tutokomeze haya mauaji yanayoletwa na watu wasiojulikana ,hili kabila la watu wasiojulikana halipaswi kuendelea kuishi.

Ila Muda ndiyo msema kweli,yatakapowakuta mtajua wapi wasiojulikana wanaishi.Hata Imran Kombe aliuawa na watuwasiojulikana.Anyway poleni
 
Dereva wa Lisu anajua kila kitu lakini amefichwa.

Tukio lolote shahidi wa kwanza ni yule aliyekuwepo eneo la tukio
Mliwakataza wtz ƙumchangia damu na kumuomɓea sasa mnawashwa washwa nini?
 
Hivi Chakubanga anakumbuka kumeza ARV zake jamani? Maana naona wadudu wameshachanganya na dish linayumba sana.
 
Hahahahahah bavicha kweli vichwa maji.Yani lisu asimame kama wakili wa dereva hahahahahah wakati yy mwenyewe na dereva wake wanatakiwa kuhojiwa.Polepole anajua mengi na ndio hoja ya mcng.mleteni dereva

Pole pole hajui lolote mpuuzi kama wapuuzi wenzake wanaodhani mtawadanganya watanzania kirahisi hivyo.Mnamjua kwa uhakika muhusika ni mwanaccm mwenzenu ila akijakuwarudi mtamtaja tu.Jinai huwa haiishi.

For your information Dereva wa Lissu ni shahidi tu,pole sana mmeshikwa pabaya sana.

Haya yule aliyechukua CCTV anamaana gani?Kuuficha ukweli??Mpaka sasa mmeshawahoji wale polisi wanalinda eneo husika?MMeshawauliza kwanini hawakuwepo lindoni??Poor you and shame on you,hamna hata haya mnadhani kuua mtu ni kitu kidogo??

Mdogo wangu chuki hazijengi zinabomoa,unayedhani adui yako leo kesho anaweza kuwa rafiki na msaada kwako,lakini unayedhani ni rafiki yako hujui kama kesho ndiyo adui yako.

Mnapiga kelele ili kumfurahisha MJUMBE,kuna siku huyo MJUMBE atakumbwa na maji ndipo itakuwa mwisho.Kwa Polepole anamatatizo ya akili hivyo kwangu namuonea huruma sana.
 
Only in tz Badala ya kuongeza cctv camera eneo la tukio zinaondolewa.
 
Hebu tujiulize maswali,
Tufanye anafichwa sawa!
Anafiichwa kwa nini?
Nani anamficha,
Tufanye cdm wanamficha,inakuaje lissu na ndugu za lisu ambao hata siyo cdm wanashindwa kuwabana cdm wamtoe?
Inakuaje afichwe pamoja na mgonjwa sehemu mojo,
Km ni lissu ndo anamficha,kwa nini,
NB kuna muda ndugu za lisu waliwahi sema hawana uhakika na usalama wa dereva
 
Da, inaonekana bado tu wana hasira na huyo dereva kwani nakumbuka kuna time aliwahi kugusia kuwatambua waliyomshambulia Lissu.

Ila all in all, wahalifu lazima tu watapatikana, kwa sasa wanachoweza kufanya ni kuchelewesha tu mambo ila watajulikana na sheria itachukua tu mkondo.
Vipi mwisho wa uchunguzi wa gari tajwa
 
Hahahahahah bavicha kweli vichwa maji.Yani lisu asimame kama wakili wa dereva hahahahahah wakati yy mwenyewe na dereva wake wanatakiwa kuhojiwa.Polepole anajua mengi na ndio hoja ya mcng.mleteni dereva

Ukifanya jambo la kijinga, nawe unajua ni la kijinga, halafu watu na hadhi zao, elimu zao kubwa tu na uelewa wao mpana kabisa, wakasimama kukutea, sijui unawaonaje watu hao wewe unayetetewa.Hii pia inakufaa
 
Hebu tujiulize maswali,
Tufanye anafichwa sawa!
Anafiichwa kwa nini?
Nani anamficha,
Tufanye cdm wanamficha,inakuaje lissu na ndugu za lisu ambao hata siyo cdm wanashindwa kuwabana cdm wamtoe?
Inakuaje afichwe pamoja na mgonjwa sehemu mojo,
Km ni lissu ndo anamficha,kwa nini,
NB kuna muda ndugu za lisu waliwahi sema hawana uhakika na usalama wa dereva

Ndugu yangu JKN alisema hivi"Ukifanya jambo la kijinga, nawe unajua ni la kijinga...................", halafu watu na hadhi zao, elimu zao kubwa tu na uelewa wao mpana kabisa, wakasimama kukutea, sijui unawaonaje watu hao wewe unayetetewa.Usiwashangae
 
Back
Top Bottom