Shaka: Sasa wapigaji wote uwe CCM au Mpinzani siku zenu zinahesabika kwa vidole

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,448
1,003

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema kutokana na kasi ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini, Rais Samia Suluhu Hassan ni pumzi mpya kwa maendeleo ya nchi.

Shaka amesema hayo leo Oktoba 15, 2022 katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Samia ukiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Geita, Shaka akitoa salamu za CCM alitumia fursa hiyo kueleza kuwa tangu Rais Samia alipoingia madarakani mambo makubwa yamefanyika.

"Sisi ambao tumekuwa na wewe leo tangu asubuhi ni mashahidi, tumekwenda pale katika Hospitali ya Kanda ya Chato. Hospitali ile ni ukombozi mkubwa kwa wananchi kwa kuwa itatibu hata magonjwa sugu," amesema.

Shaka amesema mbali na Hospitali ya Kanda ya Chato, katika eneo la Kanda ya Ziwa pia kuna hospitali nyingine kubwa ikiwemo ya Bugando ambayo inashiriknai na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutoa matibabu ya saratani na Hospitali ya Nyerere iliyopo Musoma mkoani Mara ambayo inashirikiana na Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) kutibu matatizo ya mifupa.

Mbali na sekta ya afya, Shaka amesema Rais Samia ameendelea kutekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili ya kuleta maendeleo

"Sasa ni wakati wa kwenda bega kwa bega na Rais Samia kuleta maendeleo. Rais Samia ni pumzi mpya ya maendeleo kwa nchi yetu," amesema.

Shaka ametumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia katika kuleta maendeleo kwa kuwa tangu ameingia madarakani hakuna kilichosimama.

Aidha, ametahadharisha na kuonya kuhusu rushwa katika kusimamia miradi ya maendeleo na kusema Chama kitaendelea kuwa karibu katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
=== ===
 
Wapigaji wakubwa walishamiri Sana awamu iliyopita na tatizo kubwa lilikuwa uhuru wa habari,

Nampungeza Sana Rais Samia kwa kupunguza kiwango cha Rushwa nchini,

Najaribu kupima nani zaidi kati ya nyie chawa wa Samia, na wale chawa wa enzi za Magufuli.
 
View attachment 2388770
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema kutokana na kasi ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini, Rais Samia Suluhu Hassan ni pumzi mpya kwa maendeleo ya nchi.

Shaka amesema hayo leo Oktoba 15, 2022 katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Samia ukiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Geita, Shaka akitoa salamu za CCM alitumia fursa hiyo kueleza kuwa tangu Rais Samia alipoingia madarakani mambo makubwa yamefanyika.

"Sisi ambao tumekuwa na wewe leo tangu asubuhi ni mashahidi, tumekwenda pale katika Hospitali ya Kanda ya Chato. Hospitali ile ni ukombozi mkubwa kwa wananchi kwa kuwa itatibu hata magonjwa sugu," amesema.

Shaka amesema mbali na Hospitali ya Kanda ya Chato, katika eneo la Kanda ya Ziwa pia kuna hospitali nyingine kubwa ikiwemo ya Bugando ambayo inashiriknai na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutoa matibabu ya saratani na Hospitali ya Nyerere iliyopo Musoma mkoani Mara ambayo inashirikiana na Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) kutibu matatizo ya mifupa.

Mbali na sekta ya afya, Shaka amesema Rais Samia ameendelea kutekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili ya kuleta maendeleo

"Sasa ni wakati wa kwenda bega kwa bega na Rais Samia kuleta maendeleo. Rais Samia ni pumzi mpya ya maendeleo kwa nchi yetu," amesema.

Shaka ametumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia katika kuleta maendeleo kwa kuwa tangu ameingia madarakani hakuna kilichosimama.

Aidha, ametahadharisha na kuonya kuhusu rushwa katika kusimamia miradi ya maendeleo na kusema Chama kitaendelea kuwa karibu katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
=== ===
WAPIGAJI WOTE TOKA NCHI INAPATA UHURU WAPO CCM
 
Kuongea sana na kusifia ni njia pekee na sahihi ya kuendelea kujipimia urefu wa kamba yako na kubaki katika eneo zuri la malisho.
Kwani kusifia na kujitoa ufahamu ni shilingi ngapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom