Shaka: Rais Samia pumzi mpya kwa maendeleo ya nchi

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
302
518
RAIS SAMIA NI PUMZI MPYA YA MAENDELEO

Shaka asema Kasi yake katika kutekeleza miradi ya maendeleo inatoa matumaini makubwa

Amesisitiza kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya sita huku akionya vitendo vya rushwa

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema kutokana na kasi ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini, Rais Samia Suluhu Hassan ni pumzi mpya kwa maendeleo ya nchi.

Shaka amesema hayo leo Oktoba 15, 2022 katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Samia ukiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Geita, Shaka akitoa salamu za CCM alitumia fursa hiyo kueleza kuwa tangu Rais Samia alipoingia madarakani mambo makubwa yamefanyika.

"Sisi ambao tumekuwa na wewe leo tangu asubuhi ni mashahidi, tumekwenda pale katika Hospitali ya Kanda ya Chato. Hospitali ile ni ukombozi mkubwa kwa wananchi kwa kuwa itatibu hata magonjwa sugu," amesema.

Shaka amesema mbali na Hospitali ya Kanda ya Chato, katika eneo la Kanda ya Ziwa pia kuna hospitali nyingine kubwa ikiwemo ya Bugando ambayo inashiriknai na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutoa matibabu ya saratani na Hospitali ya Nyerere iliyopo Musoma mkoani Mara ambayo inashirikiana na Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) kutibu matatizo ya mifupa.

Mbali na sekta ya afya, Shaka amesema Rais Samia ameendelea kutekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili ya kuleta maendeleo

"Sasa ni wakati wa kwenda bega kwa bega na Rais Samia kuleta maendeleo. Rais Samia ni pumzi mpya ya maendeleo kwa nchi yetu," amesema.

Shaka ametumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia katika kuleta maendeleo kwa kuwa tangu ameingia madarakani hakuna kilichosimama.

Aidha, ametahadharisha na kuonya kuhusu rushwa katika kusimamia miradi ya maendeleo na kusema Chama kitaendelea kuwa karibu katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
 
HHuyu

View attachment 2388681
Huyu dogo sio mwenezi wa chama bali ni wa Samia, kila siku anazunguka nchi akiimba Samia, Samia..... Hana kingine cha kusema zaidi ya Samia, Samia......
 
Back
Top Bottom