Shaka: Ni marufuku kwa hospitali za Serikali kumtoza Mama mjamzito kiasi chochote cha fedha wakati, kabla na baada ya kujifungua

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,986
4,083
IMG-20220819-WA0238.jpg

SHAKA "TUSIWATOZE FEDHA WAJAWAZITO"

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka amewataka watoa huduma kote nchini kuacha kuwatoza fedha wanawake wajawazito wakati wa kliniki na wanapofika kujifungua.

Shaka ametoa maelekezo hayo akiwa Jimbo la Bukene wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora alipopokea kilio cha wakina mama wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wakati wa ziara yake.

IMG-20220819-WA0237.jpg


"Naomba nitumie jukwa hili kuweka msisitizo kwenye maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa wizara ya afya pamoja na TAMISEMI juu ya kusimamia takwa la kisera la kutaka watoa huduma za afya kote nchini kutowatoza fedha wanawake wajawazito wakati wa kliniki na wanapofika kujifungua. Hapa Bukene DC na Mkurugenzi mmesikia kilio hiki naomba tusitishe tabia hiyo" Amesema Shaka.

IMG-20220819-WA0236.jpg

Shaka amewaeleza wananchi hao kuwa tayari Rais Samia ameshatoa maelekezo kwa wizara ya afya nchini kufanya mapitio ya gharama za matibabu ili kuja na muongozo utakaowapunguzia mzigo wananchi. Hivyo waendelee kumuunga mkono kwa kumuombea dua na sala pamoja na kutoa ushirikiano kwa serikali anayoiongoza kwa kuchapakazi na kulipa kodi.

IMG-20220819-WA0234.jpg

Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya CCM ya Umoja wa Wazazi Tanzania Ndg Gilbert Kalima ambaye ameambatana na Shaka katika ziara hiyo amewataka wananchi kujitokeza kuhesabiwa na kutoa ushirikiano kwa makarani siku ya sensa Agosti 23, 2022.

IMG-20220819-WA0235.jpg

'CCM Imara, Shiriki Uchaguzi Kwa Uadilifu na Jiandae Kuhesabiwa Agosti 23, 2022'

#CCMIMara
#KaziIendelee
 
Shaka Ni katibu wa itikadi na uenezi Bora kabisa kwa Sasa katika ukanda huu wa Afrika mashariki na Kati na kusini mwa Afrika, Anajuwa Nini anafanya, Amekuwa Ni mtu wa kusikiliza matatizo na kero za wananchi na kuagiza wahusika wayashughulikie matatizo ya wananchi, Shaka Ni kiongozi anayefikika licha ya ukubwa wa cheo chake,

Ndio maana unaona namna anavyo pokelewa na umati mkubwa wa watu, Namuona akifika mbali Sana kiuongozi, Sisi vijana Tuna kila sababu na mengi ya kujifunza kutoka kwake
 
Muda muafaka wa kumtafuta binti wa watu na kumpa mimba! 😆😆😆😂😂😂🤣🤣🤣🚬🚬🚬🏃🏾🏃🏾🏃🏾
 
Back
Top Bottom