Trust me, CCM ikidondoka haitakuja kusimama tena!Kwa maoni yangu ni kuwa CCM haiwezi kujiongeza upendo kwa wananchi hata kifanye mazuri mengi kiasi gani. Hata kilipe jobless mishahara lakini bado upendo kwao utaendelea kupungua.
Na sababu kubwa ni kwamba watu wameichoka tu, wengine hata hawana sababu za msingi zaidi ya kukichoka tu.
Njia pekee ya kurudisha upendo ni kustep down. kikae pembeni, kwani hii njia itawapunguza wengi wale wa ccm chumia tumbo, na kubakia na ccm-imani, ccm itikadi.
Chama kitakachotawala kwa umasikini wetu huu kitafanya fyongo tu, na hivyo kitalalamikiwa pia kama ccm. - Huu utakuwa wakati muafaka kwa ccm kujisafisha na kutengeneza upendo kwa wananchi. - Baada ya hapo uchaguzi utakaofuata (ulio fair) ccm inaingia madarakani bila makando yoyote.
Angalizo: jaribio hili lifanywe tu baada ya kuwa kimeweka misingi imara ya utawala bora nchini.