Shaka Hamdu Shaka msumari wa moto kwa Upinzani Tanzania

Mafiningo

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
4,405
2,000
Kwa maoni yangu ni kuwa CCM haiwezi kujiongeza upendo kwa wananchi hata kifanye mazuri mengi kiasi gani. Hata kilipe jobless mishahara lakini bado upendo kwao utaendelea kupungua.

Na sababu kubwa ni kwamba watu wameichoka tu, wengine hata hawana sababu za msingi zaidi ya kukichoka tu.

Njia pekee ya kurudisha upendo ni kustep down. kikae pembeni, kwani hii njia itawapunguza wengi wale wa ccm chumia tumbo, na kubakia na ccm-imani, ccm itikadi.

Chama kitakachotawala kwa umasikini wetu huu kitafanya fyongo tu, na hivyo kitalalamikiwa pia kama ccm. - Huu utakuwa wakati muafaka kwa ccm kujisafisha na kutengeneza upendo kwa wananchi. - Baada ya hapo uchaguzi utakaofuata (ulio fair) ccm inaingia madarakani bila makando yoyote.

Angalizo: jaribio hili lifanywe tu baada ya kuwa kimeweka misingi imara ya utawala bora nchini.
 

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
1,670
2,000
Kwa maoni yangu ni kuwa ccm haiwezi kujiongeza upendo kwa wananchi hata kifanye mazuri mengi kiasi gani. Hata kilipe jobless mishahara lakini bado upendo kwao utaendelea kupungua...
Wakina nani wamechoka?

Nilini walikufanya kuwa msemaji wao?
 

Jesusie

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
1,021
1,500
Sijawahi ona kiongozi mnyenyekevu kama Shaka, Kama mnamfahamu nitajieni
 

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
10,568
2,000
Msingi wake ukiwa ni aina ya Siasa anazozifanya kijana huyu Mzalendo wa kweli wa Taifa hili zimekizolea umaarufu na heshima kubwa ndani na nje ya nje Chama cha Mapinduzi kwa kipindi hiki kifupi tangu kuteuliwa kwake...
Hana lolote huyu dogo!

Anatakiwa amsaidie Mama Samia ili sera za uchumi ziwe dhahiri ndani ya chama.

Awe na lugha ya kuelezea msimamo wa chama juu ya uchumi, kitu ambacho hajakifanyia uenezi.

Siyo siri, upeo wake bado mchanga mno.
 

Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
986
1,000
Msingi wake ukiwa ni aina ya Siasa anazozifanya kijana huyu Mzalendo wa kweli wa Taifa hili zimekizolea umaarufu na heshima kubwa ndani na nje ya nje Chama cha Mapinduzi kwa kipindi hiki kifupi tangu kuteuliwa kwake,

Siasa zake za msimamo wa wastani na kuegemea zaidi kwenye kusikiliza na kutatua matatizo na shida za watu bila kujali itikadi wala hali yoyote zimemfanya Shaka Hamdu Shaka awavute watu wengi hasa vijana kujuinga na Chama Cha Mapinduzi,

Shaka pamoja na fitina na figisu nyingi alizofanyiwa huko nyuma kamwe hazijawahi kumfanya alege kwenye kukitetea na kukipigania Chama Cha Mapinduzi zaidi sana kijana huyu alisamehe na kusahau leo Shaka amegeuka kuwa darasa la Uongozi na viongozi kwa vijana wengi wa CCM na hata kwawale wasiokuwa na vyama au wavyama vingine,

Wakasema Shaka Hamdu Shaka anakula rushwa wakamsimamisha uongozi kijana huyu mwenye hulka ya Upole na Unyenyekevu hakujali wala kukata tamaa zaidi sana akaendelea kuchapa kazi kwa weledi na bidii zaidi kuliko mwanzo,

Vijana wa Tanzania tunachakujifunza toka kwa kijana huyu Mzalendo wakutiliwa mfano, Pamoja na Vita kubwa kubwa na nzito alizopigwa leo hii Shaka amegeuka lulu ndani ya Chama Cha Mapinduzi,Leo ndio mtu anayerudisha imani kwa Watanzania kuendelea kuiamini CCM-Tanzania

#Vijana Uvumilivu Unalipa sana,

View attachment 2019626

View attachment 2019627

View attachment 2019629View attachment 2019631

View attachment 2019632

View attachment 2019636

View attachment 2019686

View attachment 2019687

View attachment 2019688

View attachment 2019689 View attachment 2019706
Ni kijana gani anaweza kujiunga na ccm kwa hiari? Vijana wamepigika mtaani hawana hamu kabisa na ccm labda kipindi Cha jk ambacho ajira zilikuwa bwerere Kila Kona. Sasa hivi mwenye masters anaendesha bodabida au Ni shoeshiner halafu aipende ccm? Kwa lipo!!
 

AGGGOT TZ

JF-Expert Member
Sep 14, 2018
1,061
1,500
Tanzania inawatu wasiopenda kuwatia moyo Wale wanaofanya kazi kwa bidii,

Tanzania tunaishi kwa gubu katika kila jambo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom