Shairi: Swala la Umeme na Bunge wahenga wanasema "Mwerevu akivuliwa Nguo hasimami Huchutama"

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,611
17,843
Mwerevu akivuliwa Nguo hasimami Huchutama"(Mmetupunguza Ubongo,Mnatuchuza Hadharani)
Achutama zivukapo, mwerevu zake 'zo Nguo,
Kuinama aketipo, soniye ndio chaguo,
Tena hata aitwapo, huitika kwa rudio,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza Hadharani.

Mwatuchuza Hadharani, mmetupunguza Bongo,
Wengine si yetu fani, kuuzoea Uongo,
Twayanywa ya kisimani, hayatoki kwa miongo,
Mmetupunguza Bongo mwatuchuza Hadharani.

Juzi yeye katamka, itaanza Mwezi mosi,
Tena ni kasi kufika, dakika Mbili ni Nkasi,
Tena kaja Kugeuka, la Moshi gari majonzi,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

kama hatuna Dereva, safari yetu twendavyo,
Ya Abiria yatwezwa, gari limechoka Hivyo,
Na kasi mwatukimbiza, kelele zetu pambio,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza Hadharani.

sababuzo kuwa Giza, hazijawekwa bayana,
Wengine wadai Nguzo, ukarabati hakuna,
Kutoka na kuingiza, maji bwawani na kina,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Hakuna sababu Mpya, toka enzi za uhuru,
Zimeshindwaje kutoka, mbona wengi zatudhuru,
Mbona kodi twazipata, na mapato bullbull
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Maskini wanazidi, tabaka laongezeka,
Ajira mpaka Akidi, shilingi yaporomoka,
KIla Wakijitahidi, kodi shati yawashika,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Waziri Ananasimama, kutetea Zake chuuzo,
Arudia kudanganya, na kuongeza puuzo,
Wabunge wapongezana, kwa majina na tukuzo
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Mama kakamatwa swala, miongo miwili kenda,
Mkaguzi kataarifu, tirioni zimeenda,
Siwaoni waarifu, imefifia Ajenda,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Sifa kote zakithiri, kuliko matendo chanya,
Mwasema ni pilipili, kumbe ni hoho na nyanya,
Vizuri mngefikiri, bure mnatuchanganya,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Mengine Nayachelea, kuyaeleza kwa kina,
Nina Vijana Nalea, wadogo wwaso dhahama,
Na hofu nikiongea, nitawaacha na mama,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Uzuru Si udhaifu, ukiona Hutoshei,
Walisemaga machifu, alama haipotei,
Wapo wale wakusifu, na wengine kukebei,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.

Sisemi Bunge dhaifu, hoja njema hazisemwi,
Wengine kutwa kusifu, jimboni kwake Madeni,
Wengine wataka sarafu, iwekwe sura ya nani?
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani

NIweke kalamu chini, nisije kupigwa Bao,
pasipo Hofu ya nini, nguvu kuipa kikao,
Wallahi nilikathini, masikini hana kwao,
Mmetupunguza Bongo, mwatuchuza hadharani.
 
Back
Top Bottom