VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
- Thread starter
- #21
Sasa sijui nisemeje?Anwani na jina lake chini haimaanishi kaandika yeye, hata mie naweza kuandika kitu nikaweka anwani na jina lake chini.
Sasa sijui nisemeje?Anwani na jina lake chini haimaanishi kaandika yeye, hata mie naweza kuandika kitu nikaweka anwani na jina lake chini.
Sasa sijui nisemeje?
unakijua kitu kinaitwa leseni ya kisanaa?
leseni ya sanaa,fasihi haina matusi ndugu yangu!Hapana hiki sikijui. Lakini leseni hiyo unaweza kuitumia mbele ya watoto wako. I am trying to imagine a case unasema hivyo mbele ya watoto halafu unawaambia ni leseni ya sanaa! Tuwe na kauficho kidogo1
leseni ya sanaa,fasihi haina matusi ndugu yangu!
Nakutafuta ngabu
Nyege ni kunyegezana. Karibuni tunyegezane....
Jamaa umepotea kabisa jukwaa la siasa umewatelekeza kina jingalao. Nyege nyegezi nyumbani hapo nkoi.
Una nyege tunyegezane?
Maana yake ni nini?
Nimeshindwa kukaribia
Ndioo
Kwanzaa tuambie Siri ya kupotea jukwaani maana Leo ni Siku ya mwisho "kuhama" kisha tuendeleePeni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana,
Hufaidika malenga, huvurugika akina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana,
Maana yaki kamili, wema ni kutendeana,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna,
Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona,
Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena,
Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana,
Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
(Mshairi Bora)
Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)
SLP 4775,
Kinondoni Shamba
Dar es salaam.
Njoo tunyegezane basi...