Shairi: Nyege ni kunyegezana by Andanenga

unakijua kitu kinaitwa leseni ya kisanaa?

Hapana hiki sikijui. Lakini leseni hiyo unaweza kuitumia mbele ya watoto wako. I am trying to imagine a case unasema hivyo mbele ya watoto halafu unawaambia ni leseni ya sanaa! Tuwe na kauficho kidogo1
 
leseni ya sanaa,fasihi haina matusi ndugu yangu!
 
leseni ya sanaa,fasihi haina matusi ndugu yangu!

Naomba kujua, kama sanaa haina matusi mbona nyimbo zingine, maigizo mengine ya ngono zinazovuka mipaka huwa yanapigwa marufuku na serikali? Mbona tanzania ilikataa kumtambua mshindi wa Tanzania big brother kuwa anayoyafanya hayaendani na utamaduni wetu? Mbona Miss tanzania haiungwi mkono ki-hivyo?
 
Haiyaa haiyaa!

Wimbo wa Raymond/ Rayvany akimshirikisha Diamond Platnumz umezua tahanani na kuwafanya BASATA waingilie kati na kuupiga marufuku kwa kutumia kisingizio cha maadili.

Sungusungu wa maadili Tanzania hii hawaeshi kustaajabisha.

Sasa mimi Ngabu, nisiye na hili wala lile, nauliza tu hapa.

Shairi la yule gwiji mshairi, si mwingine yule bali Amiri Abdalah Sudi almaaruf kama Andanega, lijulikanalo kama ‘Nyege ni Kunyegezana, nalo liliwahi fungiwa na hawa mgambo wetu wa maadili ya Kitanzania?

Kama hujawahi lisikia au kulisoma hilo shairi, nakuwekea hapa.

Furahia utunzi murua kabisa wa gwiji Andanenga:

Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana,
Hufaidika malenga, huvurugika akina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana,
Maana yaki kamili, wema ni kutendeana,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna,
Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona,
Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena,
Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana,
Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
(Mshairi Bora)

Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)
SLP 4775,
Kinondoni Shamba
Dar es salaam.
 
Jamaa umepotea kabisa jukwaa la siasa umewatelekeza kina jingalao. Nyege nyegezi nyumbani hapo nkoi.
 
Kwanzaa tuambie Siri ya kupotea jukwaani maana Leo ni Siku ya mwisho "kuhama" kisha tuendelee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom