Shaffih Dauda ajirekebishe

liwaya

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
1,331
2,000
Nashindwa kumwelewa huyu shaffi dauda amekuwa na tabia ya kubeza tu na kushadidia vya nje bila ya kuwa na ulinganifu na kwa kuwa amepewa forum ya kusema tu anaitumia vibaya sana kukandia wengine bila sababu mfano jana akiwa clouds tv alikataa kutambua uwezo wa kipekee alioonyesha Manjyika Jr kwa kudai ndio wajibu wake hapo hapo anamsiru Nyiyonzima na Twite kwa kiwango bora kwa wanga na mkude. Ana sahau hata man u juzi tu de gear aliibuka man of the match na everton na kuingizwa top eleven ya week kwa kuokoa michomo mikali na hadi madrid wakaonyesha nia ya kumtaka. Kaponda mfumo wa malipo wschezaji wa kigeni wa tz na kusifia wa ulaya si ukweli kwani hata huko wanalipa kulingana na uwezo wa mchezaji na wengine ni mvuto wao kibiashara tu
 
Sumu

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
6,930
2,000
Achana na huyo kanjanja. Utakuwa mpumbavu wa mwisho kama utamchukulia kwa umakini huyo poyoyo.

Huyo Shafii ndo wale wachambuzi ambao wiki hii Man U akishinda anakwambia Man U ndo imeanza league. Wiki inayofuata Man U akifungwa anakwambia beki yao ni mbovu. Mchambuzi makini atakwambia Man U inamatatizo kwenye safu ya ulinzi hata ikishinda 5 - 0. Hao makanjanja wao wanachambua kufuatana na upepo unapoelekea.

Achana nao. Kama huna cha kufanya tafuta novel usome kuliko kumsikiliza huyo kanjanja.
 
Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,224
2,000
!
!
wachambuzi mavi hao wanaoshinda bbc, google na kwenye social media. Ndio hao wanajifanya wanaijua man utd viziri kuliko hata Van Gaal. Mchambuzi wa soka la ukweli kibongobongo bado mno, kwa dk Liki Abdalah watasubiri sana.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,844
2,000
Huyu hamna kitu. Anafuata upepo, anajifanya kulinganisha kila kitu cha hapa bongo upande wa mpira na ulaya bila kuangalia uhalisia. Ni fisi kabisa huyu. Sijui nani kampendelea kuwa mchambuzi wa soka. Nilimsikiliza jana na pia huwa nasikiliza clouds kama komedi tuu. Wote wanaokuwa pale isipokuwa yule mwenzao sijui Kibwana angalau anajitahidi, hatumii common sense, mi huwa naangalia show yao kama komedi tu. Luambano na shaffih ni kuponda tuu, wanatumia kupindi chote kuongea umbea. Si ajabu alipigwaga chini TFF.
 
Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,021
2,000
Roho za majungu
Roho za fitna
Roho za umbea
ndizo zilozo wajaa,DAUDA anatoa uchambuzi kwa mtazamo wake kwani amekulazimisha uamini kile unachoamini wewe?

HATA mimi naweza kumchambua C.Ronaldo na nikakuambia hana kikubwa sana ila mabeki wanaomkaba ndo wazembe.
 
SirChief

JF-Expert Member
Jun 23, 2014
3,215

mkuu soka la bongo limejaa magumash sana..hii kitu ata dr likey abdallah huwa anaisema sana..ni kweli hatuwez lingana na ulaya sawa..lakin hata kujarib kwa robo tushindwa!?...shafi huwa anaongea ukwel panapostaili..kwenye soka hakuna njia ya mkato, lazima tukubal kufa ili twende peponi na si vinginevyo..
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,844
2,000
Shaffih anaweza kuwa yuko sahihi kwa huyu manyika jr,sbb hakuna foward wa Yanga walichokifanya siku ile,huyo sijui hata km alipiga shuti hata moja!

Sawa! Lakini kwa dogo wa miaka 17-19, alikuwa na composure ya hali ya juu kwa mipira mwepesi michache iliyomkuta. Kwa mtu ka Shaffih ilitakiwa atambue hilo. Na sio mara ya kwanza, asilimia kubwa huwa anaponda tu, anasifiaga sana vya Ulaya. Pia ana tabia ya kujisifia kuwa hubashiri matokeo yatakuwa vipi ya mechi kadhaa. Kama ni mtaalamu awe anabet tuone kama mkeka hauchaniki.
 
Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,817
2,000
Duh, huyu jamaa ni mbishi tu..hana uchambuzi makini kabisa..yeye amekalia ubishi cku zote! Kuna kijana alikuwa naitwa Jeffy Leah, alikuwa hatari kwenye uchambuzi....anafanya comparative Analysis anajua historia, anafuatilia michezo yote! Huyu Dauda, hana lolote, nadhani apewe kazi ingine sio hii ya uchambuzi wa soka!
 
Mungu Mweusi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
1,471
2,000
Hiyo ni tabia ya kizandiki; kuna watu ambao huwa hawakibali wengine isipokuwa wao wenyewe na wakati mwingine huwa na nia ya kumuangusha mtu kwa roho ya husda. Shaffii anajiita mchambuzi wa soccer je ni chuo gani alichosomea uchambuzi wa soccer na kama ana Astashahada, stashahada, shahada,shahada ya juu au uzamivu basi aiweke hadharani kinyume na hapo ni ukanjanja tu wa njaa zinazomsumbua.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,844
2,000
Duh, huyu jamaa ni mbishi tu..hana uchambuzi makini kabisa..yeye amekalia ubishi cku zote! Kuna kijana alikuwa naitwa Jeffy Leah, alikuwa hatari kwenye uchambuzi....anafanya comparative Analysis anajua historia, anafuatilia michezo yote! Huyu Dauda, hana lolote, nadhani apewe kazi ingine sio hii ya uchambuzi wa soka!

Jeff Lea yupo Azam Tv siku hizi kila siku saa mbili usiku. Jeff Lea, ally Mayay na Edo wako juu sana. Hawa wengine umbea na mahaba.
 
makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,047
1,195
Kuna kitu kinaintwa daemokrasia wanayo haki ya kusuta na kusifia na kila mtu ana elimuyake na akili yake na kama yeye kaponda basina wewe usiache kusifia
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
31,844
2,000
Roho za majungu
Roho za fitna
Roho za umbea
ndizo zilozo wajaa,DAUDA anatoa uchambuzi kwa mtazamo wake kwani amekulazimisha uamini kile unachoamini wewe?

HATA mimi naweza kumchambua C.Ronaldo na nikakuambia hana kikubwa sana ila mabeki wanaomkaba ndo wazembe.

Basi kubali kuwa yaliyoandikwa na watu hapa ni mitazamo yao pia. Povu la nini?
 
Mar 2, 2011
86
70
Shaffi yuko sahihi kama mlienda mpirani hebu tuambieni ni mpira gani ambao ulikua ni dhahiri utakua goli manyika akaokoa hakuna hata shuti moja lilopigwa na fowadi yoyote wa yanga acheni hizo
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,864
2,000
Nashindwa kumwelewa huyu shaffi dauda amekuwa na tabia ya kubeza tu na kushadidia vya nje bila ya kuwa na ulinganifu na kwa kuwa amepewa forum ya kusema tu anaitumia vibaya sana kukandia wengine bila sababu mfano jana akiwa clouds tv alikataa kutambua uwezo wa kipekee alioonyesha Manjyika Jr kwa kudai ndio wajibu wake hapo hapo anamsiru Nyiyonzima na Twite kwa kiwango bora kwa wanga na mkude. Ana sahau hata man u juzi tu de gear aliibuka man of the match na everton na kuingizwa top eleven ya week kwa kuokoa michomo mikali na hadi madrid wakaonyesha nia ya kumtaka. Kaponda mfumo wa malipo wschezaji wa kigeni wa tz na kusifia wa ulaya si ukweli kwani hata huko wanalipa kulingana na uwezo wa mchezaji na wengine ni mvuto wao kibiashara tu

Huyo Jamaa Amenishangaza Sana Jana Na Ni Dhahiri Kuwa Ana Chuki Na Uongozi Huu Wa Simba Kwani Nimeambiwa Kuna Dili Alikuwa Analifukuzia Na Anataka Kulifanya Na Simba Na MNYAMA Wamemtolea MBAVUNI Na Pia Anatumika Na Ibrahim Masoud " Maestro " Kueneza Chuki Kwa Simba Kwani Maestro Alitegemea Naye Kupewa Cheo MNYAMANI ila Na Yeye Pia Kapigwa DOCHI LA MBALI. Nina Mengi Msiyoyajua Ya Kumhusu Huyo MITEGE Safiiii Na BINGWA WA USHIRIKINA na MAJUNGU Akiwa REDIONI na MICHEZONI Maksudi! Na NIMEMTOA RASMI KTK LISTI YA WADAU WA MICHEZO NILIOKUWA NAWAHESHIMU HAPA TANZANIA na SASA ANAINGIA Moja Kwa Moja ktk Kikosi Cha " MAPOPOMA ".
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom