Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha!

Amoeba youv said it,sio lazima iwe buku tano halisi nadhani yeye ametumia hiyo kama mfano tu kwa yule ambaye anacho kiasi kidogo kwa kuanzia na sio wale wenzio wanaosemaga ana mil 100 afanye biashara gani?(who knows km kweli anayo mill mia kweli au ni maneno tu?) sasa hali halisi ya kibongo tunaifahamu tulio wengi tusikariri kisa kasema mill 100 ukapiga hesabu ya 100 chukua idea weka kwenye biashara/mazingira yako halafu uone.

Afadhali hata wewe umeliona hili ukafanya ndoto za AMOEBA za kutajirika kwa elfu tano ziwe za kufikirika AKA Hadithi.
 
Kuna mambo mnashindwa kuelewana, "wewe" hiyo elfu tano huwezi kufanyia biashara, kwa mtu anayeanzia chini huo ni mtaji tosha kwake. Kumbuka kwamba, hiyo mil50 ambayo wewe unaona inatosha kuanza biashara kuna mtu ukimpa hiyo pesa anaona unacheza, ni pesa ndogo sana kwa level yake na hataona biashara ya kuifanyia zaidi ya kula!

Amoeba

refer to my phrase "lets be realistic"

tuachane na nadharia hatutafika mbali, kila siku watanzania wanalia kuhusu mitaji halafu leo hii tunasupport kwamba TZS 5,000 inaweza kufanya biashara ? swali la msingi ni je unaweza ku "break even" ?
 
Mkuu, naona kuna kutoelewana "viswahili" hapa, labda tubadili Lugha kidogo; Hyo elfu tano kwa vijana wanatoka mlimani ni ndogo sana kwao kuanzia, lakn siyo jambo lisilowezekana! Amini nakwambia, kuna graduates wengi wanakaa mtaani hata mika miwili kulakulala hawana kazi wanasubiri keep change ya mama....na kuna FIV leavers wengi wanatumia mtaji wa el3 kwa siku kukodi troley la kubebe a mzigo na mwisho wa siku wanagawana mpaka elf20 take home!!! Haina haja ya kutajana majina humu, nina jamaa yangu wa karibu ambaye ana biashara za faida zaidi ya 400M/pm aliishia stdIV; amini nakwambia alianza kwa kufyatua tofali za kuchoma KWA MIKONO YAKE!! Huyu jamaa ratiba yake ni kuamka saa11 na kulala saaa6 usiku kila siku ispokuwa jumapili tu, huyu jamaa mpaka leo anaendesha CRESTA, vijana wa Bongofleva mnaweza?

Mimi naona tunajifungia sana ndani jamani mpaka tunakuwa na mawazo mgando, internet tumeifanya kuwa chanzo cha kila kitu bila kufahamu kuwa kuna tabaka flani la watu tunaoweza kuwachukulia kuwa mifano ya kuigwa hawaingii huku!! LET US BE REALISTIC!
 
Mimi nina mfano halisi wa mtu ninayemfahamu ambaye alianza biashara kwa kiwango chini ya hicho miaka minne iliyopita. Yeye alianza kufanya biashara ya kuuza vipande vya sukari guru, Yaani ananunua kilo moja ya sukari guru then anaikata kata vipande vidogo vidogo na kuiuza. Alianza na mtaji wa Tsh 4,000 na siku ya kwanza kuanza biashara alipata jumla ya mauzo ya tsh 11,200 hivyo faida ya shilingi 7,200. Leo hii ana mtaji mkubwa katika biashara zake, kwa hiyo siyo kweli kwamba huwezi kuanzisha biashara kwa kiwango kidogo sana cha mtaji. Binadamu wanatofautiana pengine wewe unadhani milioni mia tano ndio inatosha kufanyia biashara lakini kwa mwingine kiwango hicho ni kidogo sana na hakuna biashara yoyote anayoweza kuifanya kulingana na hadhi yake.
 
Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo

Unajua ndo maana nilisema hapo awali kuwa mie hapo ni kula kulala. kwa hiyo baadhi ya vianzio nadesa home hapo mkuu
 
Sasa hapa AMOEBA ndiyo umeliweka hili suala vizuri, hasa baada ya kusema kama mwingine hawezi kuanzisha biashara kwa hicho kiasi, yupo anayeweza. Lakini ni vyema tukikumbuka kwamba huyo mtu anayezungumziwa kwenye post ni Graduate (ingawa hajasema ni degree au certificate), yeye anasema "kumbuka hapo ndio numemaliza chuo" kwa huo msisitizo ni wangu.

Infact hatusemi kwamba hiyo amount (Tsh.5000) haiwezi kuanza biashara, (kwani wauza karanga wanaanza na mtaji gani?) bali ni lazima uchanganye na advantage ya mazingira mtu aliyopo (ambayo kwa bahati mbaya wengi wanashindwa kuyaequate na fedha). Lakini kwa hawa graduate wetu!... (mimi nawaweka hapo kwenye blue)

Na amejiita mjasiriamali, kazi kweli kweli!
 
Watu wengi ni maskini, si kwa sababu hakuna biashara, LA HASHA, kwa sababu ya kukosa MAWAZO, UTHUBUTU na visingizio kama unavyotoa.

Watu wengi waliofanikiwa kwa kutegemea mitaji ya pesa midogo, ukumbuke wana mitaji mingine. Naona kuna umuhimu wa kufundishana maana ya mtaji.

Ukiwaeleza watu mtaji, wengi wanafikiria kwa kipesa peke yake, aah Sh. 5,000 tu itamtoa kivipi. Wanasahau, kuangalia ndani ya mtu. Ndani ya mtu , kumejaa mtaji mkubwa, Ok tuwe wahalisia hapa kwa kutaja vitu ambavyo ni mtaji.

1.Mtu mwenye ya dhati kufanikiwa katika biashara yake - Huo ni mtaji

2. Wazo - La biashara yako, namna ya kuanza, kukua na kupanuka - mtaji mwingine

3.Mazingira - Hapa Tz tunao uhuru wa kufanya biashara maeneo mengi tu bila vikwazo ,ikiwemo malipo

4. Watu - Idadi ya watu unaowajua kwenye eneo lako, ambao wanaweza kuwa wateja wako wa kwanza na hata kukusaidia kimawazo.

4. Uwezo wa kutokata tamaa na kujilinganisha na wengine isivyofaa-

5. Afya njema

Ukiangalia kuna mambo mengi yanaweza kuwa sehemu ya mtaji na kukuunga mkono. Lakini dunia na hasa Tanzania , imejaa.

a) Wakosoaji- aah mtu wa chuo kikuu aanze na sh. 5,000

b) Wakatisha tamaa- huwezi kufanikiwa kwa mtaji mdogo

c) Tanzania imejaa ufisadi, unafikiri watu wanafanikiwa bila ufisadi

d) Waangaliaji tu na kuahirisha kila jambo.
 
halafu huyu jamaa anataka kukwepa kulipa kodi, biashara gani hii?

Mkuu jaribu kufikiria nje ya sanduku mkuu! Umeshawahi kuuliza mtaji wa mama ntilie wewe! hebu funguka, nyie ndo wale ambao tukiwapa majukumu ya planning, wanaishia kuwaza mambo makubwa mabyao hayagusi maisha ya watanzania masikini wa nchi hii. Funguka akili ndugu hata kama umekulia posta mpya, yatambue maisha ya wengine, usiwe mbinafsi kiasi hicho na kudhani maisha yako ndiyo standard life!
 
Watu wengi ni maskini, si kwa sababu hakuna biashara, LA HASHA, kwa sababu ya kukosa MAWAZO, UTHUBUTU na visingizio kama unavyotoa.

Watu wengi waliofanikiwa kwa kutegemea mitaji ya pesa midogo, ukumbuke wana mitaji mingine. Naona kuna umuhimu wa kufundishana maana ya mtaji.

Ukiwaeleza watu mtaji, wengi wanafikiria kwa kipesa peke yake, aah Sh. 5,000 tu itamtoa kivipi. Wanasahau, kuangalia ndani ya mtu. Ndani ya mtu , kumejaa mtaji mkubwa, Ok tuwe wahalisia hapa kwa kutaja vitu ambavyo ni mtaji.

1.Mtu mwenye ya dhati kufanikiwa katika biashara yake - Huo ni mtaji

2. Wazo - La biashara yako, namna ya kuanza, kukua na kupanuka - mtaji mwingine

3.Mazingira - Hapa Tz tunao uhuru wa kufanya biashara maeneo mengi tu bila vikwazo ,ikiwemo malipo

4. Watu - Idadi ya watu unaowajua kwenye eneo lako, ambao wanaweza kuwa wateja wako wa kwanza na hata kukusaidia kimawazo.

4. Uwezo wa kutokata tamaa na kujilinganisha na wengine isivyofaa-

5. Afya njema

Ukiangalia kuna mambo mengi yanaweza kuwa sehemu ya mtaji na kukuunga mkono. Lakini dunia na hasa Tanzania , imejaa.

a) Wakosoaji- aah mtu wa chuo kikuu aanze na sh. 5,000

b) Wakatisha tamaa- huwezi kufanikiwa kwa mtaji mdogo

c) Tanzania imejaa ufisadi, unafikiri watu wanafanikiwa bila ufisadi

d) Waangaliaji tu na kuahirisha kila jambo.

Ufafanuzi wako umekaa vizuri mkuu.
 
leo nimeelewa almost 90% ya watanzania hawana uelewa wa mtaji wa biashara na biashara na ujasiriamali kwa ujumla.... tunahitaji kujielewa our inner selves ndio itakuwa rahisi kuelewa ujasiriamali na uthubutu wa kufanya chochote popote na kwa gharama yoyote no matter how little/small or big it takes..NIA YA DHATI na UJASIRI wa kuamini kuwa UNAWEZA hii ni silaha tosha ya mafanikio...

swali la kizushi...wakati dunia haina/ haitumii pesa kama means of exchange watu walikuwa hawafanyi biashara?... mtaji ulikuwa ni nini?...gold, diamond, slaves, mazao, mifugo etc.....TUJIONGEZEEE WATANZANIA TUKITHUBUTU TUNAWEZAAAA.
 
Asante Mkuu Amoeba.Hata hivyo, nimpe pongezi za dhati Mkuu Ndyoko kwa kuanzisha hii mada.Ukitaka kuona ukweli wa hili, angalia timu ya Zambia na ushindi wao juzi halafu uangalie Tanzania na watanzania walio wengi, inaelezea vizuri hali ya mjadala huu.Tutabaki kuwa washangiliaji kwenye maisha, badala ya kuwa wachezaji.Maishani, una uchaguzi mbili za kufanya, kuwa mshangiliaji/ shabiki asiyelipwa au kupewa medali yoyote au kuwa mchezaji ambaye hupata medali, kulipwa malipo nk.Wewe unachagua lipi?Mimi na familia yangu tumechagua kuwa wachezaji. Kila siku , tunauza kalimati nyumbani kwetu, mitumba ya bei ya mia tano tano na tunapata vichwa.
 
Mie nikiwa na tsh 5000 kama mtaji nitafanya yafuatayo
1- nitanunua kuku wa kienyeji firanga 2 @ 2000=4000/=
2- nitawafuga mpaka wakue na kuanza kutaga mayai na kutotoa vifaranga saya vifaranga 10
3-nitauza mayai ya kuku/mama wa vifaranga kila yai tsh 300/= nitapata tshs 20 x 300/= = 6000/=
4- baada ya mwaka mmoja nitakuwa na kuku kama 5 majike na majogoo sio chini ya 2.. Taratibu mwaka wa 2 nitaanza kupata mayai 60 na vifaranga vitaongezeka na lastly nitakuwa na kuku kama 100 ndani ya miaka mi-4

nisiulizwe kuhusu gharama za chakula...mind you ni kuku wa kienyeji wanajitafutia na mie ni mkaazi wa huko kiluvya, nisiulizwe kuhusu chanjo wala madawa ya kutibia mdondo maana mie nilimwona babu yangu kijijini akitibu magonjwa ya kuku kwa kuweka majani ya porini sikuhizi mwayaita aloevera kwenye maji ya kuku ya kunywa na hakuna aliyeugua...pia pilipili ni tiba ya ugonjwa wa kuku (waulizeni vijijini watawajibuni)

practically tshs 5000 inaweza kumtoa mtu ki-maisha as long as hana pressure ya mafanikio ya haraka na kutaka kutazamia maisha ya wenzake...awe focused and determined atatoka tuuu
 
Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo

nadhani yeye anapigia mahesabu kwamba vitendea kazi tayari anvyo ni hivyo tu..
 
Mimi nawapa KITU HALISI kwa mtaji wa TSh 5,000 zilizonifikisha hapa nilipo. Ilikuwa mwaka 2003.

Kwanza nilikopa sh 5,000 kwa Mwalimu Mkuu msaidizi Mwl. Komba, maana nilikuwa nakaa nyumba ya shule (Shule ya Msingi Mburahati) kwa ahadi ya kurudisha baada ya wiki.

hiyo 5,000 nikaenda sokoni Tandale nikanunua maembe, machungwa na kisu sikumbuki yalikuwa ya TSh ngapi ila ilitosha, nikarudi nyumbani nikachukua Meza yangu ya Ghetto nikaigongelea vibao pembezoni nikaanza biashara ya Maembe na Machungwa nje ya shule ya msingi Mburahati. Na pesa niliyokopa nilirudisha kabla ya wiki kiasi cha Mwl Komba kutoamini akijua haitarudi maana sikumwambia nitaifanyia nini ila aliona nilichokifanya kesho yake.

Baadae nikabadili nikaweka pipi na Biskuti nilipoona hainiendei vizuri nikabadili biashara, nikaanza kukaanga mihogo. Kwa mtaji ule ule ambao sasa ulishakuwa na kuwa na kiasi cha TSh 12,500 nikaenda Tandale nikanunua Mihogo ya Tsh 5,000 nyingine nikanunua sahani za Plastiki, kisu kingine, mkaa, karai, jalo, nyanya, vitunguu, na jiko dogo.

Siku ya kwanza nilipotumia mkaa nikaona unanigharimu kesho yake nikatumia kuni na nilianza kwa kuokota kuni kwanza jioni yake baada ya biashara. Kwa biashara hii ya mihogo ikanipandisha kwa kujiwekea kidogokidogo nikanunua Kitanda cha 5x6 mpodo, nikaendelea kujiwekea hadi nilipofikisha 180,000 niaacha biashara ya kukaanga mihogo nikaenda Tanga wilaya ya Handeni nikaanza biashara ya Maharage, nanunua kwa wakulima kwa kibaba nakuja sehemu moja wanaiita Songe naleta Handeni sokoni, nikaendelea na biashara hiyo mtaji ukakua kutoka gunia moja hadi gunia kumi.

Biashara ilipochanganya nikaungana na ndugu yangu nikawa napeleka Pangani - Handeni, nikajitanua zaidi nikawa napeleka Zanzibar kupijia Mkwaja au Kipumbwi kwa jahazi hadi Mkokotoni Zanzibar.

Hivyo msikatishwe tamaa na hiyo 5,000 bado inaweza kufanya jambo likawa kubwa kama ilivyokuwa kwangu. Mtaji wa 5,000 ndio ulionifikisha hapa nilipo leo kiasi namejenga nyumba hapa Kunduchi Mtongani, nimejiendeleza kielimu na sasa mimi ni Graphic Designer nikiwa nafanya kazi za Graphics, Video Production kwenye kampuni yangu inaitwa Creative Point nikijishughulisha na kazi hizo.

Na pia nafanya Matengenezo ya Computer, Web Designing pamoja na Installation (PC and Mac) na hii yote ni baada ya kutanua upeo wangu wa kufikili, Still ujasiliamali unaendelea.
 
leo nimeelewa almost 90% ya watanzania hawana uelewa wa mtaji wa biashara na biashara na ujasiriamali kwa ujumla.... tunahitaji kujielewa our inner selves ndio itakuwa rahisi kuelewa ujasiriamali na uthubutu wa kufanya chochote popote na kwa gharama yoyote no matter how little/small or big it takes..NIA YA DHATI na UJASIRI wa kuamini kuwa UNAWEZA hii ni silaha tosha ya mafanikio...

swali la kizushi...wakati dunia haina/ haitumii pesa kama means of exchange watu walikuwa hawafanyi biashara?... mtaji ulikuwa ni nini?...gold, diamond, slaves, mazao, mifugo etc.....TUJIONGEZEEE WATANZANIA TUKITHUBUTU TUNAWEZAAAA.

mbona mkuu ujatoa ushauri zaidi ya kuuliza maswali..
 
Back
Top Bottom