Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sh 5,000 inaweza kabisa kunitoa kimaisha!

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by ndyoko, Feb 14, 2012.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Kuna mtu amependekeza kuanza biashara kwa sh 5000, kama kawaida waungawana humu jf wamedai apeleke huo uzi wake joke forum. Lakini mie nna mtazamo tofauti hapa. Kwamba bado hiyo elfu tano inaweza kukutoa kabisa kama kweli uko serious. kwa namna gani inaweza kukutoa, hebu fuatilia hapa chini:

  Nimeamua kufanya biashara ya kuuza juisi ya matunda.

  Mananasi 2 sh 2000
  Parachichi 2, sh 1500
  Sukari robo 1000
  Jumla 4,500

  Baada ya kuitengeneza zitatoka walau lita tano, ambazo kwa kiwango cha chini, ntapata jumla ya glass zisizopungua 15. Kwa bei ya gsh 500 kwa glass moja, ikiisha ntapata jumla ya sh 7500.

  Kumbuka hapo nimemaliza chuo, bado mie ni mtu wa kula kulala-yaani nakaa geto. Nimeshatengeneza faida ya shi 3000, kwa siku. Hii ina maana kama ni ajira basi nalipwa 90,000 kwa mwezi. Hivi ntalala njaa kweli nikiamua kuwa serious na hii bishara?

  Hivi kwa hesabu ndogo kama hii, kuna haja kweli ya mtu kulia njaa jamani. Mi nadhani kinachotusumbua wengi ni kale katabia kwamba hiyo kazi ni ya kufanywa na mtu ambaye hana shule, lakini hela haina shule, na sioni kama hapo kuna kudhalilika kwa aina yeyote. Jamani, let us start from the scratch kama hatuna mbadala wa aina yeyote ktk ajira zetu.

  Tanzania hii kila kitu kinawezekana, sio ufisadi pekee tu!
   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kweli unaweza ukafanikiwa but utachelewa sana. Lakini NDYOKO mbona umepigia mahesabu ya hizo raw materials tu na si vitendea kazi? Kwa mfano Blender? Kisu? Fridge/Ice Blocks?, Dumu?, Glass?, Usafiri (to/from Sokoni), Sufuria, Boiled water (mkaa, jiko, maji n.k). Hiyo 5000 labla itatosha kama utakuwa umeshajipanga, kwani hiyo biashara si rahisi namna hiyo
   
 3. u

  ureni JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hiyo juice utaiweka kwenye chombo gani uanze kusambaza?hiyo ndoo utaipata bure?glass je utaenda kukopa?Huko utakapoenda kununua mananasi hutatumia nauli au utatembea kwa mguu?Kwenye hiyo geto utakayoishi maji yanapatikana bure?
  Lakini nisikukatishe tamaa ni theory nzuri.
   
 4. +255

  +255 JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Labda ujaribu ule mchezo wa bahati nasibu wa kutabiri matokeo, ka una bahati utakutoa maana coupon moja sh 500, ambayo unaweza kupata 10,000+, ila kwa 5,000 kufanyia biashara itabaki kuwa joke mkuu manaake hy analysis yako ni ya kufirika sana.
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Labda iwe 5,000 ya jirani zetu Kenya na siyo cash ya Tanzania yetu ninayoijua!

  Utakaa sana!
   
 6. u

  ureni JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hata elfu tano ya jirani zetu kenya bado utakaa sana,labda iwe elfu tano ya wamarekani ndio mambo yatakua safi.
   
 7. L

  LAT JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  halafu huyu jamaa anataka kukwepa kulipa kodi, biashara gani hii?
   
 8. n

  newazz JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 60
  Sh. 5000 ni mtaji tosha wa kipesa.

  Kumbuka sehemu ya mitaji mingine utaipata hapo home.

  Kwa mfano jana, nimekutana na kijana anauza karanga za kukaanga, ninamfahamu akaniambia amechoka kukaa kijiweni. Basi, nilikuwa nimesimama barabarani karibu na kwangu , nikanunua za Sh. 500, jamaa yangu mmoja akapita akamnunulia mkewe za sh. 300. Unaona, ghafla akawa ameshauza kwetu na lakini ameshauza kwa wengine.

  Mambo yanawezekana, tatizo la watanzania ni visingizio. Hizo post nyingi ni visingizio, blenda zipo nyingi , hata nyumbani anapokaa, kama hakuna unaweza ukapata kwa jirani au ukatumia njia mbadala, kwani blenda zilikuwepo miaka yote.

  Unaweza kupika vitafunio, kwa mfano kwa sh. 5000 inatosha, kupika kalimati na nyumbani wanapika kila siku kwa mtaji huo.

  Wengine, wanasema itakuchukua muda mrefu, swala si muda ila, unahitaji nia ambayo ndio mtaji mkubwa. Eti wengine wanasema, labda ingekuwa dollar 5000 ya USA, unafikiri mambo ni rahisi kwa vile una hela nyingi, waulize waliofilisika biashara za maduka ya nguo kariakoo.

  Unachohitaji ni wazo, nia isiyoyumba na wapi unataka ufike hakika utafika.
   
 9. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hujui kuwa mbuyu ulianza kama mchicha? vijana songeni mbele heshimu kile ulicho nacho (They say negative thinker see's difficulty in every opportunity ,positive thinker see opportunity in every difficulty) guys lets think positive

   
 10. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ndyoko, heshima mbele!
  Naomba nitofautiane kiasi na wakuu waliotangulia hapo juu, lakini pia nitofautiane kidogo na wewe, hasa katika ukokotozi wako ulioufanya hapo juu; kuna mambo ya msingi kabisa ambayo haujayaweka katika bajeti yako (labda haujawahi kutengeneza juisi ya aina yoyote!). Wakuu hapo juu wamepotoka kwa kusema elfu 5 haikupeleki popote, tukumbuke kuwa kila hesabu huanza na sifuri, hauna kitu then moja.

  Kimtazamo nadhani Bwana Ndyoko alikuwa anamaanisha kuwa unaweza ukaanza na kiasi kidogo kabisa ulichonacho na baadae ukafikia mafanikio makubwa kabisa ya kushangaza, tatizo ni kuwka ujumbe huu ameuleta kwa watu ambao si kiwango chao, watu ambao elfu tano haiwatoshi kwa kifungua kinywa!

  Vijana wengi hatuheshimu pesa hata kidogo, tunaangalia sana watu waliofika juu na kutamani kufika juu haraka iwezekanavyo bila kutambua kuwa hao walio juu kwa asilimia kubwa walianzia chini. Ongea na watu wenye mafanikio kibiashara, ukiondoa wale ambao kwa namna moja au nyingine walikuta njia imesafishwa na ndugu waliowatangulia, amini nakuambia wengi watakuambia walianza na sifuri, hiyo elfu tano ambayo wewe leo unaweza kumwomba hata jamaa yako na akakupa bure; yeye aliitafuta kwa jasho lake! Ninayo mifano mingi sana ya watu wa namna hiyo (ni mingi), wapo waliolima na kupata mitaji ya kuuza miwa, mitumba nk.

  Tunachokosa sana Watanzania ni mipango endelevu. Utakuta mtu anafanya kazi na kupata kiasi kizuri tu cha pesa, lakn anaona ni kidogo sana kufanyia kazi ya maana, na badala ya kuweka akiba anaidharau hiyo pesa na kuitumia katika anasa. Chukulia mfano wa muuza mitumba mwenye mtaji wa elf10, anadaka mashati matanio mnadani kwa sh elfu2 kila shati; mashati hayo akizungusha mtaani na kuuza shati moja wastani wa shilingi elfu sana atakuwa na jumla ya Tsh35,000 (faida sh 25,000/day!, siku hazifanani fanya wastani wa faida ni Tsh 15000/=), Kwa mtu mwenye kuona mbali kipato cha sh elfu kumi baada ya mwaka mmoja utamkuta na kijiduka somewhere, na baada ya miaka mitano atakuwa anaingiza faida angalau laki moja kwa siku. Lakini kwa wenzangu na mimi akiingiza elf15 kwa siku akala elf tano atabakiza elfu kumi, mwisho wa wiki atakuwa na kama elf50 Jumapili utamkuta anasumbua Bar za Uswahilini na Malaya!!!!! Tuige wenzetu Wachagga, Wakinga, Wasukuma wa Kule bariadi, na vijana kutoka maeneo mengine walio na akili za kusonga na kuacha kulalama hatukopeshwi na hali hatukopesheki!!
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Ulishawahi kuanzisha biashara yoyote? Unapozungumzia kukaa sana, wewe unataka kutajirika ndani ya muda gani, kwa biashara gani, mtaji gani? Mtaji toka wapi? Weka mchanganuo wako hapa!
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ni hii elfu tano ya Tz inaweza kukutoa kabisa, suala la muda ni suala lingine, inaweza kukutoa kwa sababu, moja tayari umehama kwenye nadharia na umeingia ktk kutenda/kuthubutu kwa silaha uliyo nayo, pili upungufu utakaoupata kupitia hiyo buku tano ndio utakaofanya ubongo wako upanuke zaidi ili kuikabili changamoto hiyo mpya.
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu, lets be realistic bana, kwa dunia ya sasa hivi, unafanyaje biashara na mtaji wa 5,000 halafu uka break even?

  labda ufanye "biashara"
   
 14. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Kuna mambo mnashindwa kuelewana, "wewe" hiyo elfu tano huwezi kufanyia biashara, kwa mtu anayeanzia chini huo ni mtaji tosha kwake. Kumbuka kwamba, hiyo mil50 ambayo wewe unaona inatosha kuanza biashara kuna mtu ukimpa hiyo pesa anaona unacheza, ni pesa ndogo sana kwa level yake na hataona biashara ya kuifanyia zaidi ya kula!
   
 15. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbona hujamalizia hapo kwenye red? Nilichokiona mimi haya mawazo ya Mkuu NDYOKO yapo ki idealist zaidi. Kwanza ametolea mfano wa Graduate. Mtu umetoka chuo (unapata 10,000 per diem = 300,000) ambayo ni zaidi ya kima cha chini cha mshahara, ukashindwa hata kufanya saving (sorry najua wengine hawapati mkopo). Leo unaongelea elfu 5 kama mtaji wa biashara?

  Kwanza mwanachuo aliyekuwa na mkopo chuoni, akirudi huku uraian kuswitch life (hakuna boom) anaathirika kisaikolojia kabisa (hasa kama hajapata Diploma kutoka University of Life), sasa ndio uje kumpa mtaji wa elfu 5 (yaan kiingilio cha disko kwa usiku 1) kwa ajili ya Biashara. Ndyoko kuwa muwazi kama kweli yupo huyo Graduate aliyeanza na hyo elfu 5, nipe details zake kwenye inbox yangu (Ni PM) nami nitamuongezea mtaji
   
 16. u

  ureni JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160

  AMOEBA elfu tano haiwezi kufanyia biashara hizo zinaitwa ni ndoto za abunuasi,huyo machinga unayesema itokee gafla augue hilo jina lako hiyo hela nahuakika haitamtosha kwa matibabu,tatizo wewe amoeba unatetea kitu ambacho hakiwezekani unataka kulazimisha kiwezekana,ni sawasawa na kulazimisha madaktari warudi kazini bila kuwaboreshea maslai yao utaua watu wewe.
  Kwa tz ya sasa huwezi kufanya biashara kwa mtaji huo ikakutoa.
   
 17. +255

  +255 JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Kama biashara zingekuwa rahisi kwa mtindo huo sidhani kama kungekuwa na "MASIKINI"
   
 18. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Amoeba youv said it,sio lazima iwe buku tano halisi nadhani yeye ametumia hiyo kama mfano tu kwa yule ambaye anacho kiasi kidogo kwa kuanzia na sio wale wenzio wanaosemaga ana mil 100 afanye biashara gani?(who knows km kweli anayo mill mia kweli au ni maneno tu?) sasa hali halisi ya kibongo tunaifahamu tulio wengi tusikariri kisa kasema mill 100 ukapiga hesabu ya 100 chukua idea weka kwenye biashara/mazingira yako halafu uone.
   
 19. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sasa hapa AMOEBA ndiyo umeliweka hili suala vizuri, hasa baada ya kusema kama mwingine hawezi kuanzisha biashara kwa hicho kiasi, yupo anayeweza. Lakini ni vyema tukikumbuka kwamba huyo mtu anayezungumziwa kwenye post ni Graduate (ingawa hajasema ni degree au certificate), yeye anasema "kumbuka hapo ndio numemaliza chuo" kwa huo msisitizo ni wangu.

  Infact hatusemi kwamba hiyo amount (Tsh.5000) haiwezi kuanza biashara, (kwani wauza karanga wanaanza na mtaji gani?) bali ni lazima uchanganye na advantage ya mazingira mtu aliyopo (ambayo kwa bahati mbaya wengi wanashindwa kuyaequate na fedha). Lakini kwa hawa graduate wetu!... (mimi nawaweka hapo kwenye blue)
   
 20. M

  Malila JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Siku moja nilikuwa naongea na Mbunge mmoja, wote tuna wazo moja lakini scale tofauti. yeye alianza na eka 500 kwa sh 15,000/ kila eka na mimi nilianza na eka 5 kwa Tsh 15,000/. Msimu ulipofika mimi nilianza na yy akasema ni aibu akiendeleza kidogo kidogo kama mimi. Baada ya miaka mitatu tangu tuanze, mimi nikamtembelea pale Dar ofisini kwake ( sasa sio mbunge),akasema namnukuu " unajua ningefanya kama wewe ningekuwa mbali sana".

  Red marked part is very important to you kama mjasiriamali.
   
Loading...