Sh. 2000/=

Sh. 2000/=

pata picha:

Mtu anakuomba hela ya bia au soda, unampatia tsh 2000/=

alafu huyo huyo uliyempa hela anakwambia "yaani unanipa elfu mbili?? Dharau hiyo!"

wewe unasemaje hapo?

Hapo hajakwambia umpe hela ya kiasi gani!
mtu akiomba bia mpe bia ukimpa pesa atakuzalau tu hatatosheka na hiyo pesa
 
Yaani Papa mopao kila ukijibu unalalamika "hana shukurani", akiwa na shukrani utampa nyingi eehe?

Ha ha ha! Alzadawi...siyo kwamba nimelalamika, kinachonipa shida ni pale mtu hata kile unachokitoa kidogo ulichonacho anaona unamdharau wakati moyoni mwako ile dharau haipo!!
 
Pata picha:

Mtu anakuomba hela ya bia au soda, unampatia Tsh 2000/=

Alafu huyo huyo uliyempa hela anakwambia "Yaani unanipa elfu mbili?? dharau hiyo!"

Wewe unasemaje hapo?

hapo hajakwambia umpe hela ya kiasi gani!

mkuu mbona hesabu simple tu...hapo unamwambia hebu nirudishie hiyo buku 2. akirudisha unageuka kuondoka zako au unauchuna. akiuliza mbona hunipi..unamwambia naitunza hii buku 2 siku zikiwa nyingi nitakupa! hapo ndo forever...
 
Haaaa! Mkuu kweli una majibu ya kutosheleza, bravo bana...!
 
Kwa mtu anayetoa mshangao "Yaani unanipa buku 2???" Huyo hata ukimpa buku 10 hatakushukuru?

Utampaje mwanamke buku teni jamani, si bora umwambie sina.....
Teh! papa naomba ubadili jina asee, jina na matendo ni vitu viwili tofauti!!!!
 
malipo ya kuwalegezea mademu macho.... mwanaume usiwe laini. kama huna sema si kujigamba gamba kama una hela kumbe povu
 
Nilifungua hapa kwa matumaini ya kukuta michango yako maridhawa, 'Mkatoliki' uliyetukuka. Haya ndio mambo saizi ya akili yako

Babu pumu tena ukapumulie mbali, unipishe na ukome kunifatilia!!!!
nyie mnaojifanya mnazijua dini huwa wanafiki sana!!!!
 
Kwa kazi ipi aliyofanya? uvivu hadi mfukoni. Mi sitoi hata bati

Pole sana, wapo wengine wanatumia hela yako kwa mambo mengine ambayo si muhimu, hela zao wanazitunza za kununua sofa, kiwanja na gari na mengineyo kama hayo!!!
 
Utampaje mwanamke buku teni jamani, si bora umwambie sina.....
Teh! papa naomba ubadili jina asee, jina na matendo ni vitu viwili tofauti!!!!

Kuhusu buku kumi...hii haina shida chochote ulichonacho unampa moyo ukikusukuma utoe kiasi gani siyo yote bana.

Jina siyo tatizo bana Evelyn Salt...
 
Kongosho ndugu yangu, ngoja nikupe hii picha:

Wewe una sh elf 3 kwa mfano, anakuja mtu anaomba bia tu, sasa kwa vile una elf tatu ukachomoa buku 2 umpe ili akajinunulie zake huko ukabakiwa na buku moja za kukusaidia hapa na pale kwenye shughuli zako, bado huyo mtu anakwambia, "Yaani umenipa elf 2??? hii dharau!" Ingekuwa ni wewe unaombwa ofa ya bia utafanyaje na mfukoni una elf tatu tu?

Nadhan umenipata mtani wangu!!!
Hiyo ilinikuta mimi nikiwa na elfu mbili tu mfukoni nikakutana na ticha wangu ile kuniona tu kaanza kuchecheka afadhali nimekuona mwanafunzi wangu twende unipe soda, mimi nikajua itakuwa soda kweli ile tumefika ticha kaagiza bia kipindi hicho bia ilikuwa buku, baada ya kulipa nikaona hapa hapanifai nimkamuaga ile kuaga tu akaniambia sasa inabidi ununue na nyingine ili hii ikiisha niendelee, masikini mwanafunzi mie nikajitutumua nikamwachia na buku iliyobaki na mimi nikabaki mifuko tupu halafu mtu kama huyo aniambie dharau, lazima nimtukane na kumnyang'anya hicho kidogo nilichompa.
 
Ha ha ha ha ha nimecheka sana hapo kweli red...kuna wengine hawajui kwenye mfuko wako kuna sh ngapi bana...please language ni mbovu alaf hata shukrani hakuna!
 
Back
Top Bottom