Hao SGS hamna nilichokiona cha maana kwenye ripoti yao.
SGS wajanja wanajichomoa na wanawapima watanzania akili zao.
Hata kama wanajisifu wapo karibu nchi zote, wakiongoza katika kufanya analysis, sampling n.k n.k Bado haijatengua ripoti ya Pr Mruma kuprove alichokiona kwenye makontena.
Nianze na mfano.
Umeenda hospital unahisi kichwa kinakuuma, umemueleza dr akupime uenda una malaria, Dr akakuchukua damu bahada ya matokeo akagundua kweli una malaria.
Tanzania ni kama mgonjwa pale tunasimamiwa na TMAA, tunategemea matokeo ya sampling kutoka SGS ambae ndio kama DR, akitoa matokeo ya sample aliyochukua na TMAA ndio wanafile hiyo hiyo.(kumbuka hapo tushamwabia atupe matokeo ya copper, silver na gold.
Hapo Dr wetu SGS kashamaliza kazi yake, hana lawama, lawama zitakuja kwa tofauti ya viwango tu.
Sasa kama umeenda hospital na ukamueleza Dr mie naumwa lakini chukua damu na upime magonjwa yote. Hapo dr atakuja na majibu yote una typhod, UTI, Kaswende, gono, malaria, kichaa n.k n.k (rejea uchunguzi wa pr Mruma mchanga kapima kila content iliomo mule)
Umeona kazi ya SGS ilivyo rahisi, kama watalazimika kuzipima upya sample za nyuma ni lazima zitaleta majibu tofauti na waliyonayo kwenye ripoti na hili si kosa lao ni makubaliano ya TMAA na Accacia wapime gold, silver na copper.
Hapo SGS hana makosa, makosa yapo kwa Accacia wanakijua wanachokifanya