SGR Dar-Moro yafikia asilimia 98, Moro-Makutopora 93%

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema maendeleo ya Ujenzi reli ya kisasa (SGR) kwa vipande vyote vitano unaendelea vizuri ambapo kwa kipande cha Dares Salaam hadi Morogoro ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 98

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TRC, Jamila Mbarouk, alipozungumza na gazeti la
HabariLEO jana.

Jamila alisema kuwa ujenzi wa SGR kwa kipande cha kwanza cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ume-fikia asilimia 98.14 wakati ujenzi kwa kipande cha kutoka Morogoro hadi Makutupora umefikia asilimia 93.83.

Alisema ujenzi katika vipande vingine nao unaendelea vizuri ambapo kipande cha kutoka Makutupora hadi
Tabora ujenzi wake umefikia asilimia saba. Kwa mujibu wa Jamila, kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka ujenzi wake umefikia asilimia 2.39 wakati kipande cha kutoka Isaka hadi Mwanza ujenzi wake umefikia asilimia 31.07.
 
Mbona walianza hadi kupendekeza bei za kutoka Dar hadi Dom tangu mwaka 2022?

Mbona wanacheza na akili zetu?

Mchi hii ni mazoba daima wa kudanganywa kila siku?
 
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema maendeleo ya Ujenzi reli ya kisasa (SGR) kwa vipande vyote vitano unaendelea vizuri ambapo kwa kipande cha Dares Salaam hadi Morogoro ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 98
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa TRC, Jamila Mbarouk, alipozungumza na gazeti la
HabariLEO jana.
Jamila alisema kuwa ujenzi wa SGR kwa kipande cha kwanza cha kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ume-fikia asilimia 98.14 wakati ujenzi kwa kipande cha kutoka Morogoro hadi Makutupora umefikia asilimia 93.83.

Alisema ujenzi katika vipande vingine nao unaendelea vizuri ambapo kipande cha kutoka Makutupora hadi
Tabora ujenzi wake umefikia asilimia saba. Kwa mujibu wa Jamila, kipande cha kutoka Tabora hadi Isaka ujenzi wake umefikia asilimia 2.39 wakati kipande cha kutoka Isaka hadi Mwanza ujenzi wake umefikia asilimia 31.07.
Tanzania. Miaka michache ijayo Inshallah tutaanza kupanda SGR
 
Back
Top Bottom