Sweden kusaidia gharama za ujenzi wa SGR Lot 3 (Makutupora - Tabora - Isaka)

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ambaye ameahidi kuwa nchi yake itashiriki kugharamia ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.

Katika mazungumzo yao Mhe. Nchemba ameishukuru Sweden kwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania, ikiwemo kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Lot 2, kipande kinachoanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida, ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 96 na kwa utayari wa nchi hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kujenga reli kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.

Ziara ya Balozi huyo wa Sweden Mhe. Charlotta Ozaki Macias, aliyeambatana na Balozi wa Biashara Endelevu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Bi. Cecilia Ekholm, ni ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba, aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden, mwezi Septemba, 2023
 
Jamhuri ya mbeleko na madeni mvururu mwaka bado tutaona mengi bado umeme wa hiyo reli maana treni bado na umeme unasumbua mbeleko zitawaua hawa watu hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutegemea kupewa.
 
Hakuna madeni tuna vijideni..
Sisi kukopa bado sana.
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ambaye ameahidi kuwa nchi yake itashiriki kugharamia ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.

Katika mazungumzo yao Mhe. Nchemba ameishukuru Sweden kwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania, ikiwemo kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Lot 2, kipande kinachoanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida, ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 96 na kwa utayari wa nchi hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kujenga reli kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.

Ziara ya Balozi huyo wa Sweden Mhe. Charlotta Ozaki Macias, aliyeambatana na Balozi wa Biashara Endelevu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Bi. Cecilia Ekholm, ni ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba, aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden,
Sweden kusaidia tz ujenzi wa SGR umeifurahisha nini andika Sweden yaikopesha tz!! Unajua maana ya msaada? Mjitahidi kuwa mnaandika ukweli kwanza.
 
Back
Top Bottom