SFO: Hivi ndivyo Chenge alihusika kashfa ya rada!

Naunga mkono kuwavalisha tairi kwani kiukweli hatuna vyombo vya sheria tena nchi hii!!!
 
Pia baba yake DR Hosea ndie aliemsomoshe Nimrod Mkono kupitia nafasi aliyekuwa nayo katika kanisa la kisabato ,kwa hiyo hawa wanasheria wa enzi hizo wanakamtandao kao akina Mkono,Hosea,Masaba,Chenge na mpwa Felesi.
mambo mengi sana yamejificha............tusipoangalia vizuri hizi background za viongozi wetu ndio chanzo cha mitandao michafu kama ya akina jk,lowasa,rostam
 
Pia baba yake DR Hosea ndie aliemsomoshe Nimrod Mkono kupitia nafasi aliyekuwa nayo katika kanisa la kisabato ,kwa hiyo hawa wanasheria wa enzi hizo wanakamtandao kao akina Mkono,Hosea,Masaba,Chenge na mpwa Felesi.
mambo mengi sana yamejificha............tusipoangalia vizuri hizi background za viongozi wetu ndio chanzo cha mitandao michafu kama ya akina jk,lowasa,rostam
 
Jamani, sijui Hosea anasema nini kufuatana na taarifa yake ya leo ya kummsafisha Chenge.
 
Mwenyewe kasema jalada lake la SFO na TAKUKURU yote yameshafungwa sasa hivi anasubiri ama kuapishwa au kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa Spika wa bunge la JMT
 
Mwenyewe kasema jalada lake la SFO na TAKUKURU yote yameshafungwa sasa hivi anasubiri ama kuapishwa au kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa Spika wa bunge la JMT


Tunataka nao SFO waseme -- maana hawajasema bado. Hata Takukuru walikuwa hawajasema bado. Mimi naona kuna uharaka unafanyika havya, yaani achaguliwe Uspika kabla SFO hawaja-confirm wanachodai Chenge na Hosea. SFO wakija na taarifa tofauti wakati Chenge kishakuwa spika ndiyo basi tena.
 
TAKUKURU wamesema Mh Chenge hahusiki-official statement from PCCB, ipo blog ya Michuzi
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA


Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.


TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.


Imetolewa na

Doreen J.
Kapwani,

Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010

S. L.P. 4865,

Dar Es Salaam.
http://www.wavuti.com/4/post/2010/1...ha-chenge-na-rada-takukuru.html#ixzz14hRxmHnW
 
Inasikitisha kuwa wtakuwa waandamizi wa serikali ya Tanzania. Labda ingefaa ya Albashir
 
Sasa hata kama alihusika mtafanya nini nyie watadanganyika? Kwanza hizo hela mbona kidogo tu ukilinganisha za kagoda?

Watanzania wengi hawahoji hizi tuhuma kwa nguvu. Watu walitakiwa waandamane nchi zima kushinikiza serikali isema ukweli kuhusu hizi hela. Lakini cha kushangaza watu kibao walikuwa wanachomwa na jua pale uwanja wa taifa jumamosi huku wakishangalia. Hawajuulizi hela za Kagoda alichukuwa nani na yuko wapi?

Wadanganyika bwana, kazi kweli.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI


YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA
RADA




Tunapenda
kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza
kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew
Chenge katika tuhuma hizo.

TAKUKURU inawaomba wananchi
waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale
wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja
wetu.

Imetolewa na
Doreen J.
Kapwani,

Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 ,
2010

S. L.P. 4865,
Dar Es
Salaam.

Simu: 2150043-6/2150360 |
Nukushi: (022) 2150047 | Barua pepe: dgeneral@pccb.go.tz | Mtandao
www.pccb.go.tz




from: Tumeshindwa kumhusisha Chenge na Rada - TAKUKURU -

Haya takukuru, mnajaribu lkutuchanganya makusudi au? Je hizo fedha ambazo serikali ya Uingereza imesema italipa kwa TZ na serikali yetu ikasema izipokee yenyewe nim za nini? Kama ni rushwa kwenye Rada nani alihusika kama siyo Chenge, Vithlan.Rashid na wenzao? Ebu tuwakumbushe taarifa ya SFO ambayo nyinyi takukuru mlikataa/mliogopa kuifanyia kazi:
 
Hosea's statement is unfair nonsense I tell you...:nono: What next? Lowassa and Aziz?
 
CHENGE KUWA SPIKA....NOOOOOOO!!
HOSEA KUMSAFISHA CHENGE ILI AWE SPIKA NOOOOOOOO!!
Ujanja-ujanja huu wananchi tusiupokee, tusiuafiki na tusiuvumile kamwe!
Hapa dawa ni wananchi kuandamana na kuupinga mpango huu wa kuikabidhi nchi kwa utawala unaotetea na kulinda mafisadi...
Hii haikubaliki, njama hapa ni kumuwezesha Chenge apite katika Uspika ili kuziba aina zote za kujadili haki za wananchi kuhusu ufisadi, ufilisi wa rasilimali na kulinda maslahi ya wanaotuhumiwa na watakaotuhumiwa kwa ufisadi...tutumbuke Richmond!

MUNGU IOKOE NCHI YETU INAYOPELEKWA KATIKA MAANGAMIZI....!
Nani hajui kuwa Richmond na Hosea alikuwepo? Rada nayo ina mikono ya vigogo? Hii ni hatari na haikubaliki...

Afadhali wananchi tulipinge lili kwa nguvu zote...hakuna cha Chenge kuwa Spika, na suala la Hosea kumsafisha ni ukiukwaji wa maslahi ya Taifa.
 
inasikitisha sana

yani ccm katika wale wabunge zaidi ya mia ndio wameona chenge anafaa?
 
TAKUKURU ni Chombo ambacho kinalinda maslahi ya Mafisadi wa Nchi hii. Taarifa zote na Ushahidi uliopo unajitosheleza hasa kuhusu jinsi Chenge na Rashid walipotajirika ghafula. TAKUKURU na Hosea wanataka kutuambia hawalioni hilo au ndiyo kuchakachua taaluma ili kulinda maslahi binafsi. Hosea awajibike. Lakini kama mtakumbuka wakati wa suala la RICHMOND, Bunge liliazimia Hosea awajibike lakini Ikulu ilimkingia kifua na hakujiuzulu. Tunahitaji wanasheria wa nchi hii waingilie kati kwa kuanzia pale SFO walipoishia ili watu aina ya hakina Chenge na Vikaragosi wao watendewe haki.
 
headline_bullet.jpg
Achunguzwa na vigogo wengine saba
headline_bullet.jpg
Makachero wadai ana kesi nzito ya kujibu


Chenge%283%29.jpg

Mheshimiwa, Andrew Chenge

Wakati kampuni ya kutengeneza zana za kijeshi ya Uingereza, BAE Systems, imekubali kulipa faini ya Dola za Marekani milioni 450 ili kumaliza kesi mbalimbali zilizokuwa inaikabili kutokana na udanganyifu wa kuuza zana za kujeshi kwa nchi kadhaa duniani Tanzania ikiwamo, suala hilo linamweka njia panda aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kutokana na suala la kuhusika kwake kwenye kashfa hiyo kurejeshwa mikononi mwa serikali.

BAE Systems imeamua kulipa kiasi hicho cha fedha ili kumaliza kesi zilizofunguliwa dhidi yake na Ofisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO) pamoja na Wizara ya Sheria ya Marekani.

Katika fedha hizo, Wizara ya Sheria ya Marekani italipwa Dola milioni 400, wakati SFO watalipwa Dola milioni 47.

Fedha za SFO zitakwenda kwa nchi ambazo zilikuwa zikiendesha uchunguzi kuhusu biashara zilizofanywa na BAE System ikiwamo Tanzania, Jamhuri ya Czech, Romania na Afrika Kusini.

Wakati BAE wanakiri kuboronga mambo kwa kuwasilisha taarifa za uongo kwa serikali ya Marekani kuhusu biashara ya zana za kijeshi na jinsi ya kuepukana na rushwa, kwa Tanzania inakiri kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi kuhusu biashara ya kuiuzia Tanzania rada mwaka 1999.

BAE Sytems inakiri kwamba kwa kuboronga mambo katika uuzaji wa rada kwa Tanzania, inaridhia kulipa fidia ya Pauni milioni 30, sehemu ya kiasi hicho kikiwa ni msaada kwa ajili ya Tanzania.

Hatua hizi mpya za BAE System sasa zinaacha mamlaka za Tanzania katika mtihani mgumu ambao hazikutarajia hasa kutokana na uchunguzi wake kuwagusa baadhi ya wakubwa nchini akiwamo Chenge na Dk. Idris Rashidi.

Katika uchunguzi wa SFO dhidi ya Chenge, yafuatayo ndiyo yaliwekwa bayana kuwa ni tuhuma mahususi kwa mbunge huyo wa Bariadi Magharibi ambaye alijiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu Aprili 2008 baada ya SFO kufichua kuwa amejihifadhia kitita cha zaidi ya Dola milioni moja (Sh. bilioni 1.2) katika akaunti kisiwani New Jersey kikihusishwa na rada hiyo.

Ripoti kamili ya uchunguzi
Barua ya Machi 21 mwaka 2008 iliyoandikwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa (SFO), kwenda Mwanasheria Mkuu wa Tanzania inasema.

Mpendwa Mwanasheria Mkuu wa serikali,
Yahusu: Bae Systems PLC, Red Diamond Trading Ltd & Merlin International Ltd, Envers Ltd, Tanil Kumar Chandulal, Somaiya, Shailish Pragji Vithlani, Andrew Chenge na wengineo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa (SFO) anawasilisha kwa Mamlaka za Kisheria za Tanzania na hususan Mwanasheria Mkuu, taarifa hii ili kupata msaada utakaowezesha uchunguzi zaidi wa tuhuma kuhusu makosa makubwa yaliyofanyika nchini Uingereza.

SFO iliundwa kutokana na Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 1987 (CJA 1987) na ikaanza kufanya kazi Aprili 6 mwaka 1988. Chini ya CJA 1987, mkurugenzi wa SFO anaweza kuchunguza na kufungua mashitaka ya jinai dhidi ya tuhuma atakazoona ni kubwa na nzito zilizofanywa nchini Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini. Mkurugenzi anafanya kazi chini ya uangalizi wa Mwanasheria Mkuu wa Uingereza na Wales.

Wanasheria katika taasisi hii (SFO) wana nguvu sawa kama wanavyopewa na mkurugenzi katika kuchunguza, kufungua na kuendesha mwenendo wa kesi. Mimi (Matthew Cowie) ni mwanasheria na nimeteuliwa na mkurugenzi kuwa msimamizi mkuu wa kesi hii ambayo kwayo tunaleta maombi haya ya kutaka msaada wako.


Watuhumiwa
SFO kwa kushirikiana na Wizara ya Polisi na Ulinzi (MDF) tunachunguza taasisi na watu wafuatao: Wa kwanza ni Bae System PLC, yenye makazi yake namba 6 Carlton Gardens, London, wa pili ni Michael Peter Rouse aliyezaliwa Januari 29, mwaka 1948. Anaishi nyumba namba 26 Badgers Hill, Virginia Water, Surrey.

Watatu ni Sir Richard Harry Evans (aliyezaliwa Julai 9 mwaka 1942). Yeye anaishi Hallcross Manor, Lancashire. Wa nne ni Michale John Turner aliyezaliwa Agosti 5 mwaka 1948 ambaye kwa sasa anaishi namba 79 Fairmile Lane, Cobham, Surrey wakati Julia Aldridge aliyezaliwa Machi 31, 1957 ni mtuhumiwa wa tano. Yeye anaishi nyumba namba 102, Barabara ya Forest, Liss, Hampshire, Uingereza.

Mtuhumiwa wa sita ni Andrew John Chenge (aliyezaliwa Desemba 24, mwaka 1946) mkazi wa nyumba namba 546 katika Barabara ya Ghuba, Oyster Bay, S.L.P 11 958 Dar es Salaam, Tanzania, wa saba ni Tanil Kumar Chandulal Somaiya (aliyezaliwa Julai 7 mwaka 1965) mwenye hati ya kusafiria namba A 0163862. Barua zake zinapitia Merlin International Limited, Ghorofa ya 1. Avalon House, Barabara ya Zanaki, S.L.P 4013, Dar es Salaam, Tanzania na tisa ni Shailesh Pragji Vithilan. Akiwa amezaliwa Oktoba 3, mwaka 1964 ana hati ya kusafiria namba B 404501 barua zake hupitia kwa Merlin International Limited, Ghorofa ya 1. Avalon House, Barabara ya Zanaki, S.L.P 4013, Dar es Salaam, Tanzania.

(Hata hivyo mtuhumiwa namba saba hatajwi)

Makosa ya Jinai wanayotuhumiwa
Uingereza ni moja ya nchi zilizotia saini Mkutano wa mwaka 1997 juu ya Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo katika Kudhibiti Rushwa inayofanywa na maofisa wa umma wa Kimataifa katika Biashara. Mwezi Desemba mwaka 2001, Uingereza ilianza kutekeleza azimio hilo kwa kuanzisha Sehemu ya 12 ya Sheria dhidi ya Ugaidi, Makosa na Usalama ya mwaka 2001 (2001 Act). Sheria hiyo ya mwaka 2001 iliifanyia marekebisho Sheria ya Uzuiaji Rushwa ya mwaka 1906 kwa malengo ya kuiwezesha serikali kupanua wigo hadi nje ya mipaka. Vifungu vya marekebisho ya sheria ya Kuzuia Rushwa ya mwaka 1906 vilianza kutumika rasmi nchini Uingereza Februari 14 mwaka 2002.

Kuna sababu kadhaa zinazotufanya tuamini kwamba watu wote waliotajwa hapo juu pamoja na makampuni wamefanya makosa ya kupokea ama kutoa rushwa kinyume cha kifungu namba 1 cha Sheria ya Kuzuia Rushwa ya mwaka 1906.

Kiwango cha juu cha adhabu ya mtu anayepatikana na makosa haya ya rushwa ni kifungo cha miaka saba jela.

SFO na Wizara ya Polisi na Ulinzi ilipata habari kwamba kulikuwa na uchunguzi wa ndani kuhusu tuhuma za rushwa katika mchakato wa Bae kuiuzia serikali ya Tanzania rada ya kuongezea ndege. SFO kwa upande mwingine, inaendelea kufanya kazi sambamba na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Ukweli kuhusu hili ‘dili’
Katika kujua nini hasa kilijiri katika mchakato mzima wa kuuziana rada hii, SFO iliomba maelezo kupitia barua zifuatazo:

Barua ya maombi ya Juni 13 mwaka 2006, Barua ya nyongeza ya maombi ya Machi 14 mwaka 2007 na Barua nyingine ya Nyongeza ya Maombi ya Oktoba 1, mwaka 2007.

Yaliyojulikana
Mwaka 1999 Bae iliingia katika mkataba wa kuuza rada na vifaa vyake kwa Serikali ya Tanzania. Rada hiyo ilitakiwa ifanye kazi katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam. Kadhalika rada hiyo ilikuwa na uwezo wa kuongoza ndege za kiraia na za kijeshi.

Bei ya ununuzi wa rada hiyo ilikuwa Dola za Marekani milioni 40. Kilichogundulika ni kwamba mpango wa kununua rada kwa ajili ya Tanzania ambao uliihusisha Bae ulianza mwaka 1992, lakini wakati huo ukifanywa na kampuni ya Siemens Plessey Systems (SPS). Katika kipindi hicho, serikali ya Tanzania ilikuwa inataka kununua vifaa vya kijeshi kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 88.

Bae iliichukua kazi za SPS Oktoba 1997 na kurithi mipango iliyokuwa ikiendelea ambayo sasa ilikuwa katika hatua ya juu. Hata baada ya bei ya rada kupunguzwa hadi dola milioni 40, mauzo haya yaliendelea kupingwa na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha Duniani (IMF) pamoja na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa na Ofisi ya Mambo ya Nje za Uingereza. Pamoja na pingamizi hilo, kwa mshangao wa wengi, Bae ilipewa leseni ya kusafirisha rada hiyo na mkataba huo wa mauziano ukaridhiwa.

Mawakala wa Tanzania: Envers na Shailesh Vithlan
Mwaka 1999, Bae kupitia kampuni ya Red Diamond Trading Limited, kampuni iliyosajiliwa katika kisiwa cha Virgin, Uingereza, iliingia katika makubaliano na kampuni iliyosajaliwa Panama ya Envers Trading Corporation. Envers ilijitambulisha kama wakala anayefanya kazi Tanzania. Mawakala hawa waliwahi pia kufanya kazi na SPS na waliendelea kufanya kazi hata baada ya shughuli za SPS kuchukuliwa na Bae. Nyaraka zilizotolewa kwa SFO zinaonyesha kwamba Envers ilikuwa inatakiwa kupata kamisheni (cha juu) ya asilimia 30 ya mauzo ya rada hiyo.

Katika uchunguzi wa SFO, imegundulika kwamba Tanil Jumar Chandulal Somaiya na Shailesh Pragji Vithlani, walikuwa na nguvu za kufanya maamuzi ya kisheria katika Envers na walifanya kazi kupitia anuani inayohusisha kampuni ya Merlin International Limited (Merlin) yenye makazi yake Dar es Salaam.

Kati ya Januari 2000 na Aprili 2005 zaidi ya Dola milioni 8 zililipwa na Bae kwa Envers kupitia Red Diamond. Malipo haya yaliendelea licha ya kuanza kwa kutumika kwa Sheria dhidi ya Ugaidi, Makosa ya Jinai na Usalama ya mwaka 2001 hadi pale makubaliano baina ya Red Diamond na Envers yalipositishwa rasmi Desemba mwaka 2005 baada ya kulipana Dola 3,362,250.

Inajulikana kutokana na nyaraka ambazo SFO ilipata kutoka Bae kwamba Vithlani alikuwa anahusika katika sakata hili kama wakala wa SPS katika hatua za mwanzo za mchakato wa ‘dili’ hili. Lakini hakuna maandishi yoyote kutoka kwa Vithlani yaliyopatikana kuonyesha malipo aliyolipwa, lakini taarifa kutoka kwa mtu aliye karibu na Vithlani zinaonyesha kwamba hakuwa mtaalamu wa rada wala mjuzi wa mambo ya biashara kuonyesha umuhimu wake katika suala hili kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Kwa sasa SFO inaona kwamba Vithlani alikuwa na kazi maalum ya kuwalipa ‘cha juu’ maofisa wa serikali ya Tanzania wenye maamuzi muhimu kuhusu ununuzi wa rada hii. SFO inaamini kutokana na nyaraka ilizo nazo kwamba Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Andrew Chenge, alikuwa ni mmoja wa watu muhimu kwa Vithlani kuwapa malipo kama mlungula kutokana na umuhimu wa maamuzi na mapendekezo yao kwa serikali.

Andrew John Chenge
Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania kati ya mwaka 1995–2006. Katika kipindi hiki, Bae na SPS walikuwa wanaendelea na mazungumzo kuhusu mauzo ya rada kwa ajili ya Uwanja wa Ndage wa Dar es Salaam na Serikali ya Tanzania. Chenge alihusika katika suala hili kwa namna mbalimbali, hususan kuhusu malipo ya ununuzi wa rada.

Kwa kifupi, ili kufikia makubaliano ya kulipia rada, ilikuwa ni lazima kuwepo na kujiridhisha kwamba mauzo hayo yalikuwa sahihi. Kwa mantiki hiyo, bila Mwanasheria Mkuu kukubali, malipo ya rada ambayo yalifanywa kupitia benki ya Barclays yasingeweza kufanyika. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilitakiwa kutoa maoni yake na kisha kukubali malipo yafanyike ama kukataa.

Umuhimu wa namna ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilivyoshughulikia sakata hili unaonekana pia katika barua ya Juni 16, mwaka 2005 kutoka kwa maneja mauzo wa SPS, Naqvi pale anaposema:

“Kile kinachoendelea kuwa muhimu, ni hitaji la Mwanasheria Mkuu kuhusu kuona mkataba halisi wa mauziano haya.”

Nyaraka ambazo SFO inazo zinaonyesha kwamba Juni 29, mwaka 1995 Mwanasheria Mkuu yeye mwenyewe (Chenge) alishiriki katika mazungumzo ya mauziano ya hii rada. Kutoka siku hiyo, ushiriki wa Mwanasheria Mkuu katika mchakato mzima wa malipo kuhusu rada hii unatajwa katika nyaraka nyingi za ndani ya SPS.

Kati ya mwaka 1996 na 1997 mchakato mzima wa kuuziana rada hii ulikuwa inaelekea ukingoni.

Taarifa zilizopatikana kwa mamlaka ya uongozi wa kisiwa cha Jersey kati ya Juni 19 mwaka 1997 na Aprili 17 mwaka 1998 zinaonyesha kwamba kupitia kampuni linayomilikiwa na Chenge ya Franton Investiment Ltd, Chenge alipokea dola za Marekani milioni 1.5 katika akaunti ya kampuni hiyo iliyoko katika benki ya Barclays, tawi la Jersey. Pesa hizi zinaonekana kwamba mapema zilihamishiwa huko kutoka tawi la Barclays la Frankfurt na kupitia nyaraka zingine zilizopatikana kutoka JO Hambro zinazoonyesha kuwa pesa hizo zilianzia benki ya LGT tawi la Liechtenstein. Nyaraka zinasema mlipwaji ni “mmoja wa wateja wetu”.

Nafasi ya Vithlani katika kufanikisha mchakato mzima unaonekana katika nyaraka zilizotolewa na wafanyakazi kadhaa wa SPS. Hakuna ubishi kwamba anayetajwa kama “rafiki” au “mtu mnene” katika waraka huu kwa mfano ni Vithlani.

Mark Simpkins wa SPS alisema katika barua iliyotumwa kwa faksi Agosti 30 mwaka 1997:

“Nilikuwa na mazungumzo marefu na rafiki yetu na nilikuwa na mkutano asubuhi hii na Mwanasheria Mkuu ili kupitia masuala muhumu… Tulijadili mpango mzima katika kufikia mkataba halisi. Tumekubaliana kwamba ni muhimu tuwe tumekamilisha mambo yote ifikapo wiki ijayo. Amesema atawajulisha watu wake kinachoendelea. Mtu mnene, kama ninavyosema sasa, alisema ni muhimu kusaini nyongeza katika makubaliano haya… Anasema kwamba ameingia ahadi na wahusika wa zamani na wapya katika mpango huu hasa ikizingatiwa kwamba mchakato mzima umechukua muda mwingi kukamilika…”

Moja ya jambo muhimu katika mpango mzima wa majadiliano ilikuwa uchambuzi wa sheria pale kunapotokea mtafaruku katika mkataba wa mauziano haya. Hili lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa jukumu la Mwanasheria Mkuu.

Septemba 8, mwaka 1997, Simpkins aliandika:
“Pia mwishoni mwa wiki, rafiki yetu mnene alikuwa akijitahidi kushughulikia mambo yote ya kibiashara yanayojitokeza. Asubuhi hii amenijulisha kwamba vikwazo vyote vilivyokuwa vinaonekana kujitokeza amevimaliza kama ifuatavyo (pamoja na mambo mengine):

Sheria: Wamekubali kutumia sheria za Uingereza na Upatanishi wa kisheria (kama utatokea mtafaruku kwenye mkataba) utafanyika Uingereza.

Kutokana na maelezo ya hapo juu inaonekana kwamba ushirika wa Chenge na Vithlani ulipelekea makubaliano hayo ya kisheria ambayo yanaipunguza Barclays hofu ya kupoteza fedha zake kwa kuikopesha Tanzania. Pia inaonekana maelezo kwamba Vithlani ameingia ‘ahadi mpya’ ni suala la kutoa rushwa. Na hii pia inaonekana kwenye nyaraka ambazo Vithlani alikuwa anafanya marekebisho mbalimbali ya uwakala wake.

Itaendelea kesho

CHANZO: NIPASHE

Kwa mtazamo wangu naona kesi hii inamizegwe kwani kuna watu mashuhuri ambao kwa namna fulani wanafununu za wizi huu kama wenyewe hawahusiki.

Jakaya Kikwete kama waziri wa mambo ya nje na sasa Rais
Bwana Othman Rashid kam afisa wa ubalozi uingereza na sasa mkurugenzi mkuu wa usalama
hawa nni watu mhimu sana katika kusaidia kupata mwafaka wa kesi hii lakini kama kwa namna fulani
walihusika au kuzembea wakati huo mnategemea mwenendo wa kesi uweje.
kama kampuni imekubali kulipa mamilioni hayo ni dhahili lisemwalo lipo.
Mwisho Hosea wa Tasisi ya kuzuia rushwa mnamtuma akazuie rushwa ipi?, hivi watanzania ni lini tutapata ufahamu ( Je utamtuma nyani kufukuza nyani wenzie kwenye shamba la mahindi mategemeo yako yatakuwa yepi?).
Lipo tazizo ambalo watanzania wengi bado tumelifumbia macho nalo ni la Uongozi bora,kama vile mwalimu Nyerere alivyowahi twambia kuwa tunahitaji Watu,Ardhi,siasa safi na uongozi bora, Watu tunao tena wavumilivu, Ardhi yetu imejaa neema ambayo haielezeki kiasi kuwa tuna hata madini yasiyopatikana kwingineko, vivutio k.m Kilimanjaro,Ngorongoro, Maziwa yetu makuu ambayo mengine ndo yanayochangia uhai wa baadhi ya nchi zingine kama Victoria inavyo watunza huko juu kwa mto Nile na n.k.Lakini uongozi bora haupo, hapo awali angalao tulikuwa na siasa safi sasa nayo imeyoyoma imebakia siasa ya samaki mkubwa kumla mdogo. Ndg zangu ni wakati wa kuamka na kuanza kupambana na uongozi huu dhaifu usio bora ambao una hatari ya kutusababishia janga na maafa yasiyo na sababu. Je tutakimbilia wapi maana nchi yetu ndo ya makimbilio sasa sisi tutakimbilia wapi.
 
Hivi wanasheria wa bongo inakuwaje mnakubali taaluma yenu inapakwa matope na ninyi mko kimya pride yenu iko wapi, jitokezeni basi tuone makali yenu, kila kitu ni magumashi kuanzia mikataba ya madini mpaka mienendo ya kesi, si mnamkumuka mlivyomuachia Zombe wakati ushahidi wa mazingira haukuwa na utata wowote, sasa mnataka tuwasifu kwa jema gani mlilolifanyia taifa lenu. kweli mnashangaza sana acheni upuuzi fanyeni kazi bwana, kama fani imewashinda nendeni mashambani mkaendeleze kilimo kwanza kwa power tilers za JK, mnaudhi sana kwa kweli, sijui mkoje? ???? :A S-baby: watu wengine bwana
 
zile pesa ni za watoto yatima na mimi ni mwanahisa tu.
full stop.
wenye wivu wajinyonge.
 
Wazungu nao siku hizi ni wasanii!mbona wamechelewa sana kutoa matokeo ya uchunguzi wao na hasa ukizingatia kwa sasa teknohama ipo juu sana ,hapa duniani!!
 
Back
Top Bottom