MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,591
Dunia haijawahi kuchoka kupokea elimu mpya kutoka katika hazina ya Fikra za wakazi wake. Yawezekana Ikawa kweli au mbinu za werevu wachache kutia hofu wakazi wa dunia lakini Gonjwa hili linasadikiwa kukua kwa kazi ya ajabu kwa mujibu ya watu waliozama katika mlengo huo wa maarifa.
SEXUALLY TRANSMITTED DEMONS NI NINI?
Kwa uhalisia Tendo la ndoa lilihifadhiwa kwa ajili ya Mtu mme na mke. Nje ya hapo utakutana na Uzinifu,Uasherati,Usagaji,Ushoga na kila uchafu kwa wa kingono kwa aina zake. Hapa inaelezwa kwamba Mtu mwenye majini (Kwa waislamu MAJINI WACHAFU) au Mashetani/Mapepo akifanya tendo la ndoa na mtu asiyenayo, Ule muunganiko Unatoa fursa ya kushea Majini hayo kati ya pande mbili.
Maelezo yanaenda mbali zaidi kwamba Sio majini tu ya kawaida haya bali hadi mizimu ya mmoja wa washiriki inafunguliwa milango inaingia kwa upande wa pili. Ukifikiri sana uhalisia wa Elimu hii basi unamfikiria mtu ambaye ameshafanya ngono na watu zaidi ya 500 atakuwa amejizolea Mashetani kiasi gani kama wapenzi walikuwa wabebaji wa Mashetani.
ELIMU HII
Imetapakaa katika imani ka kiprotestanti, na baadhi ya mielekeo michache ya kiimani na changamoto ni uhalisia wa haya mambo maana yako katika Frequency/Mawimbi yaliyo nje ya uwezo wa Macho na Darubini.
MASWALI YANAOYOBAKI KWETU
1:Je Majini/Mapepo/Maraika wachafu na Mashetani wanawezaje kuhama kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine Kupitia ngono.
2:Je Ni nini Dalili ya mtu anayesumbuliwa na SSexually Transmitted Demons?
3:Tiba yake ni nini?
4:Je watu wote wasio wasiamini katika uwepo wa Mungu,Mapepo na dhana ya Dhambi ni wahanga wa hii janga au wao wanakaa kwenye kundi lipi?
5:Je kunauwezekano wa kukwaa janga hili kwa njia ya Masturbation?
6:Je hizi ni story za kutisha waumini ili waachane na ngono nje na kabla ya ndoa na ni njia ya wajanja wachache kupiga pesa kwa kuwatibu kiimani wahanga huku sadaka zikitiririka kwa pembeni?
7:Watafiti wa Jambo hili wanasema karibu 70% wa watu wanaoshiriki tendo la ndoa nje ya ndoa wanamashetani, Je huu ni Ushahidi wa kutosha kuamini uwepo wa janga hili?
karibu useme chochote katika upande huu wa fikra, Dunia ina mambo.
Note:Mada hii haina uhusiano na mwanadamu kufanya mapenzi na Mashetani.
LENGO: Lengo kuu la bandiko hili sio kutisha watu kama ilivyoibuka kwenye maelezo bali ni kujua UHALALI AU UBATILI WA IMANI hii Kwa USHAHIDI WA VYANZO VYA BIBILIA/QURAN AU CHOCHOTE KATIKA IMANI ZA KIAFRIKA