Sex...

Lizzy soma shule umalize halafu nijulishe umemaliza vizuri baada ya hapo nikumbushe juu ya hii mada yako ambayo ni nyeti sana halafu nitakuelekeza cha kufanya kama kweli wataka majibu ya maswali yako yaliyojaa hekima kibao................lol
Mbona nimeshamaliza?!Ndo nakukumbusha rasmi kunipa majibu...
 
Lizzy umesema vyema tendo ni kwa ajili ya kuzaana (tuijaze dunia) ila kuna mengineyo 'msinyimane msijeingia majaribuni, mfurahie mwenzi wa ujana wako nk' hapo kuna habari ya kutoshana.., kwa habari ya kutoka nje ya ndoa nionavyo mimi kuna vitu 2 vinatafutwa 1;tamaa 2;kutafuta upendo bandia
 
Kuna nadharia kadhaa ya kwanini biological sex imeweza kuwepo. Moja ni kwamba viumbe wanazaliana kwa njia ya 'sex' ili kuongeza uwezekano wa vizazi vyao kupambana na vimelea halifu (parasites). Kuna viumbe wanaozaliana kwa kwanjia ya kuji'clone wenyewe (yaani kuji'photocopy) - aina hii ya kuzaliana haitumii 'energy' kama kupitia sex na viumbe wanazaliana kwa haraka zaidi. Tatizo ni kwamba, vimelea halifu wanaweza kuleta maafa kiurahisi kwa kushambulia vizazi vinavyotokana na aina hii ya kuzaliana, kwani wote wanakuwa 'wanafanana' katika chembechembe za vinasaba (DNA).

Ila kupitia 'sex' kunakuwa na mchanganyiko wa DNA kutoka kwa mzazi wa kike na kiume hivyo kuongeza uwezekano wa kusaidia vizazi kupambana na hao vimelea halifu. Majuzi kuna wanasayansi wameweza kuonyesha haya kwenye maabara. Soma hapa: Science Magazine: Sign In
 
Back
Top Bottom