Serikali yavunja Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yavunja Katiba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Mar 21, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,490
  Likes Received: 19,888
  Trophy Points: 280
  Elias Msuya
  SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imevunja Katiba kwa kutoteua makamishna wapya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora baada ya makamishna wa awali kumaliza muda wao.

  Mpaka sasa haijulikani ni lini Serikali itateua makamishna wengine wa Tume hiyo ingawa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe alikiri makamishna wa Tume hiyo wameliza muda wao.

  Kutokuwapo Tume hiyo, Serikali imevunja Katiba Ibara ya 129 (1) katika Sura ya Sita, sehemu ya kwanza inayoeleza kuwa "Kutakuwa na Tume itakayoitwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora" ambayo majukumu yake yameelezwa katika Ibara ya 130 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kwa mujibu wa Katiba hiyo kazi za Tume ni nane ambazo zimeahinishwa katika mtiririko wa alfabeti A hadi H, baadhi zikiwa ni kupokea malalamiko ya uvunjaji wa haki za binadamu na wajibu kwa jamii kufungua kesi mahakamani ili kuzuia vitendo vya uvunjaji haki za binadamu au kurekebisha haki inayotokana na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.

  Tume hiyo haipo kwa zaidi ya wiki moja sasa baada ya waliokuwa makamishna kumaliza muda wao Machi 13,mwaka huu huku.Kaimu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Joaquine De Mello amekiri kuwapo kwa hali hiyo akieleza kuwa serikali ndiyo mwamuzi, lakini alifafanua kuwa makamishna wote walituma tena maombi kuendelea na kazi hiyo.

  “Taarifa hizo ni za kweli,na makamishna wote wamemaliza muda wao. Sheria ya Tume inasema kuwa, mkataba wa makamishna ni miaka mitatu, ikiisha pande mbili zina ridhaa ya kuamua kuendelea au kusimamisha mkataba huo, ” alisema De Mello.

  De Mello alisema kuchelewa kuteuliwa kwa makamishna wa Tume hiyo siyo jambo geni, kwani hata Tume iliyopita ilicheleweshwa hivyo hivyo.

  Alipoulizwa kwa kufanya hivyo serikali haitakuwa inawanyima haki wananchi ambao sasa hawana pa kupeleka malalamiko yao, De Mello alijibu huku akihoji: “Wewe unaulizia wananchi, mbona huulizi sisi makamishina hadi sasa hatuna ajira, Au sisi hatuna haki? Kwanza siyo Tume hii tu, mbona hata mikoa mipya iliyoundwa haina wakuu wake? alihoji

  Akirejea sheria ya Tume hiyo ibara ya 8(1) alisema kuwa, kamishna akimaliza muda wake atakoma kuwa kamishna, ila atakuwa anastahili kuteuliwa tena kwa miaka mingine mitatu. Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema kitendo cha serikali kuchelewa kuteua makamishna siyo tu kuvunja Katiba, bali pia kinainyima nguvu Tume hiyo.

  “Kutoteua makamishna kwa wakati ni kuinyima nguvu ya kikatiba tume hiyo na ya kimaamuzi, na ni uvunjivu wa haki za binadamu,” alisema.

  Sungusia alifichua kwamba, Serikali imekuwa ikiinyima bajeti ya kutosha tume hiyo ili tu ishindwe kufanya kazi yake ipasavyo. “Kila mwaka serikali imekuwa ikiipunguzia bajeti tume hiyo ili ishindwe kufanya kazi zake,” alisema.


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mathias Chikawe alipoulizwa alikiri Tume hiyo kumaliza muda wake, lakini alisema suala hilo linafanyiwa kazi.Alifafanua kwamba tayari taarifa kuhusu kumalizika kwa muda wa Tume hiyo zimefikishwa kwa waziri husika na kwamba zinafanyiwa kazi.

  Alisema mbali na kufahamu hilo, amekuwa akipigiwa simu na watu mbalimbali waliotaka kujua kuhusu uteuzi wa makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na kusisitiza kuwa amemjulisha Waziri wa Sheria, Celina Kombani.

  "Najua muda wao umepita, hilo linafanyiwa kazi. Tayari tumewafahamisha wahusika, Waziri wa Sheria ana taarifa na analifanyia kazi," alisema Chikawe.Waziri wa Sheria na Katiba Celina Kombani alisema siyo jambo la ajabu kwa makamishna wa Tume hiyo kuchelewa kuteuliwa upya.

  “Uteuzi ni suala la serikali, sasa kama hawajateuliwa hadi sasa, ‘is it news?' (Hiyo ni habari?). Lakini, uteuzi ni mchakato na serikali ndiyo inayojua. Ikitokea leo kamishna mmoja amefariki, kazi zitasimama? Si kuna watendaji wengine wanaendelea?” alisema Waziri Kombani.

  Hata alipoulizwa kuwa uteuzi huo utachukua muda gani, alisema:“Wewe andika tu lolote, kama itachukua wiki, mwezi, mwaka wee andika tu,” alisema Kombani na kukata simu.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kombani maskini!
   
Loading...