Serikali yatoa msimamo ujenzi bomba la mafuta la EACOP

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Serikali ya Tanzania imesema hakutakuwa na athari zozote za kiamzingira wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chomgoleani Tanga, kwani tahadhari zote zilizingatiwa kitaalamu.

Waziri wa Nishati, January Makamba alitoa kauli hiyo jana, ikiwa ni sehemu ya ufafanuzi wa maazimo yaliyotolewa siku tatu zilizopita katika Bunge la Ulaya (EU) kuhusu utekelezaji wa mradi huo.

Kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanaharakati wamekuwa wakidai kuwa utekelezaji huo utasababisha athari kimazingira, zikiwemo kuongezeka kina cha bahari, uharibifu kwenye chanzo cha ziwa Victoria, bonde la mto Nile na utolewaji wa hewa chafu ya ukaa zaidi ya tani milioni 37 kwa mwaka.

"Wito kwa EU na jumuiya ya kimataifa kutoa shinikizo kubwa kwa mamlaka za Uganda na Tanzania, pamoja na waendelezaji wa mradi na wadau, kulinda mazingira na kukomesha shughuli za uchimbaji katika mazingira yaliyohifadhiwa na nyeti, ikiwa ni pamoja na Ziwa Albert," ilinukuu taarifa ya Waziri Makamba.

Endapo mradi huu utakamilika utaenda kutunufaisha wananchi wote wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo basi tupuuze taarifa za uongo zinazosambazwa na baadhi ya wanaharakati kwenye mitandao ya kijamii.
 
Aisee! Ninachojua mzungu huwa hashindwi kitu. Kama amekataza mkilazimisha mradi hautafika mbali.

Ikifika wakati wa uuzaji wa hayo mafuta kuna kasoro zitapandikizwa kwenye hayo mafuta na yatawadodea.
 
athari kimazingira, zikiwemo kuongezeka kina cha bahari, uharibifu kwenye chanzo cha ziwa Victoria, bonde la mto Nile na utolewaji wa hewa chafu ya ukaa zaidi ya tani milioni 37 kwa mwaka.
Sasa hapa jamaa anajiona ana iq kubwa mno kuwa tutafaidika wote. Mbona hatujafaidika na Ile software ya iliyokodiwa kwa 69Bilioni kufuatilia umeme unapokatika nchini
 
Aisee! Ninachojua mzungu huwa hashindwi kitu. Kama amekataza mkilazimisha mradi hautafika mbali.

Ikifika wakati wa uuzaji wa hayo mafuta kuna kasoro zitapandikizwa kwenye hayo mafuta na yatawadodea.
Walishtuka baada ya wanaharaki kusambza taarifa kwamba kuna uharibifu wa mazingira which is not true kwani tahadhari zote zilichukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom