Serikali yatangaza upya zoezi la uhakiki wa Vyeti feki laanza June 2017

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
27,900
2,000
Habarini wanaJF!
Uhakiki umechosha kwa watumishi wa umma umechosha sasa loooh!

Tutatakiwa kuwa na vitu vifuatavyo:
1. Kitambulisho cha NIDA
2. Kitambulisho cha kazi
3. Salary slip

Imechosha sasa, si kwa uhakiki huo!!!:(:(:(
Re : Zoezi la Uhakiki Watumishi wa Umma kwa Kutumia Taarifa za Kitambulisho
cha Taifa Pamoja na Ukaguzi wa Uingizwaji wa Taarifa katika Mfumo wa HCMIS
Tafadhali husika na somo tajwa hapo juu.

Tumepokea maelekezo ya Serikali kupitia barua toka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa

Umma na Utawala Bora yenye Kumb. Na.CFC.26/205/01”Y”/56 ya tarehe 06 Juni, 2017 kuhusu mada tajwa hapo juu. Kama mtakumbuka Mamalaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ilifanya zoezi la

Kuwasajili watumishi wa Umma kwa ajili ya kuwapatia Namba ya Utambulisho na Kitambulisho cha Kitaifa cha Taifa kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi mwezi Machi, 2017. Aidha, hatua inayofuata ni kufanya uhakiki wa taarifa za watumishi wote wa Umma kwa kutumia

Taarifa za NIDA zilizoingizwa kwenye Mfumo wa HCMIS. Ili kufanikisha zoezi hili uhakiki wa watumishi litaanza kuanzia tarehe 16 Juni, 2017 kwa watumishi walio Mikoani watahakikiwa katika Wilaya mliopo chini yaWakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambako zoezi hili litafanyika.

Aidha, ili kufanikisha zoezi hili kila mtumishi anapaswa na kutakiwa kuwa na nyaraka zifuatazo

wakati wa uhakiki;-
a) Kitambulisho cha kazi chenye picha ya mtumishi husika,
b) Hati ya malipo ya mshahara (Salary slip) na,
c) Kitambulisho cha Taifa au Namba ya Utambulisho wa Taifa

Ni matumaini yangu kwamba mtashiriki na kusimamia ipasavyo utekelezaji uweze kukamilika katika muda uliopangwa.

cad6100d9f105633e3380809d8681967.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom