hapo kuna mkoa wa magufuli,pinda,makinda,huo wa simiyu sababu za kisiasa!mkoloni alikua na majimbo tukaendelea kuliko
Jamani mbona haya maajabu mi katika maisha yangu sijawai kusikia mkoa wenye wilaya mbili
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19
My Yake: Je kuna umuhimu wa lazima kuwa na mikoa mipya?
SERIKALI imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72.
Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyanghwale, Nyasa, Uvinza na Wangingombe.
Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe (Njombe) na Katavi (Mpanda).
Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyanghwale. Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wangingombe wakati mkoa wa Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na Itilima.
Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe (Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba); Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko (Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).
Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti); Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyanghwale (Kharumwa); Nyasa (Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wangingombe).
Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge, Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21. Hata hivyo, baada ya kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions),wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
ALHAMISI, MACHI 8, 2012.
==================================================
Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda.......hii sasa ndio nini mkoa kuwa na wilaya mbili tu?.......halafu mikoa yote mipya ni kama kuwapendelea viongozi fulani....Geita(Magufuli).....Simiyu(Chenge).....Katavi(Pinda)......Njombe(Makinda)...
Naona Katavi unaweza kuwa ni mkoa wa kwanza kuwa na wilaya 2. S angalau wangemega wilaya za Kigoma?.
hapa sasa ukuu wa wilaya ingekuwa unagombea ningesema nikachukue fomu japo nijiliwaze na ukuu wa wilaya,
lakini ndo yale yale, mahawara na watoto wao waliowazaa nje ya ndoa zao ndo watapewa nafasi za uongozi ambao hakuna wanachokifanya, me sielewi hii serikali inachofanya ni nini?
its about time tuigawe hii nchi, maana itoshe sasa kugawa mikoa na kuongeza mzigo kwa serikali moja ambayo haina uwezo wa kuihudumia si tu mikoa iliyopo, achilia mbali mikoa mitatu tu.
Suluhisho la pekee sasa ni kuigawa hii nchi zitoke nchi tatu kila mmoja kivyake au tuwe na serikali ya majimbo japo manne ambayo kila mmoja ata manage jimbo lake kama usa.
Aaaaah me nimechoka sasa jamani.