Serikali yatangaza rasmi Mikoa mipya 4 na wilaya 19 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali yatangaza rasmi Mikoa mipya 4 na wilaya 19

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msanii, Mar 8, 2012.

 1. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI[/FONT]


  [FONT=&amp]SERIKALI YATANGAZA RASMI MIKOA MIPYA MINNE NA WILAYA 19[/FONT]  [FONT=&amp]SERIKALI imetoa matangazo rasmi ya Serikali (Government Notices) kuhusu uanzishaji wa mikoa mipya minne na wilaya mpya 19 ambayo yamechapishwa tangu Machi 2, mwaka huu.[/FONT]


  [FONT=&amp]Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema matangazo hayo ambayo yalisainiwa na Rais Jakaya Kikwete tangu Machi mosi, 2012, yanabainisha mikoa mipya kuwa ni Geita, Katavi, Njombe na Simiyu. Mikoa hii imechapishwa katika Tangazo la Serikali Na. 72.[/FONT]

  [FONT=&amp]Wilaya 19 ambazo zimeanzishwa na kuchapishwa katika Tangazo la Serikali Na.73 ni Buhigwe, Busega, Butiama, Chemba, Gairo, Ikungi na Itilima. Wilaya nyingine ni Kakonko, Kalambo, Kaliua, Kyerwa, Mbogwe, Mkalama na Mlele. Nyingine ni Momba, Nyang'hwale, Nyasa, Uvinza na Wanging'ombe.[/FONT]

  [FONT=&amp]Kwa mujibu wa matangazo hayo makao makuu ya mikoa hiyo mipya minne yatakuwa kama ifuatavyo: Geita (Geita), Simiyu (Bariadi) Njombe (Njombe) na Katavi (Mpanda).[/FONT]

  [FONT=&amp]Mikoa hiyo itakuwa na wilaya zifuatazo; Geita utakuwa na wilaya tano za Bukombe, Chato, Geita, Mbongwe na Nyang'hwale. Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda. Mkoa wa Njombe utakuwa na wilaya nne za Makete, Njombe, Ludewa na Wanging'ombe wakati mkoa wa Simiyu utakuwa na wilaya tano za Bariadi, Busega, Maswa, Meatu na Itilima.[/FONT]


  [FONT=&amp]Makao makuu ya wilaya mpya zilizoanzishwa ni kama ifuatavyo: Buhigwe (Buhigwe); Busega (Nyashimo); Butiama (Butiama); Chemba (Chemba); Gairo (Gairo); Ikungi (Ikungi) Itilima (Lagangabilili); Kakonko (Kakonko); Kalambo (Matai) na Kaliua (Kaliua).[/FONT]

  [FONT=&amp]Nyingine ni Kyerwa (Rubwera); Mbogwe (Mbogwe); Mkalama (Nduguti); Mlele (Inyonga); Momba (Chitete); Nyang'hwale (Kharumwa); Nyasa (Mbamba Bay); Uvinza (Lugufu) na Igwachanya (Wanging'ombe).[/FONT]

  [FONT=&amp]Julai 2010, kabla Rais Kikwete hajatoa hotuba ya kulivunja Bunge, Serikali ilitoa uamuzi wa kuunda mikoa mipya minne na wilaya mpya 21. Hata hivyo, baada ya [/FONT][FONT=&amp]kuhakiki mipaka ya maeneo hayo yote na kuandaa maelezo ya mipaka hiyo vizuri (boundary descriptions),[/FONT][FONT=&amp]wilaya zilipunguzwa na kubakia 19.[/FONT]


  [FONT=&amp](mwisho)[/FONT]

  [FONT=&amp]IMETOLEWA NA:[/FONT]
  [FONT=&amp]OFISI YA WAZIRI MKUU,[/FONT]
  [FONT=&amp]S. L. P. 3[/FONT][FONT=&amp]021,[/FONT]
  [FONT=&amp]DAR ES SALAAM.[/FONT]
  [FONT=&amp]ALHAMISI, MACHI 8, 2012[/FONT].

  [FONT=&amp] ==================================================

  [/FONT]
  [FONT=&amp]My Yake: Je kuna umuhimu wa lazima kuwa na mikoa mipya? [/FONT][FONT=&amp]
  [/FONT]
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Shangazi , mjomba , rafiki watapata ajira
   
 3. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  CHALINZE nje.....duh jamaa anaogopa lawama kupendelea home
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  wapuuzi sana hao, walifikiri watavuta tention zetu kwenye kugawa wilaya na mikoa, tuna matatizo mengi hatutaki takwimu za idadi ya wilaya au mikoa, tunataka maendeleo.
   
 5. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hayo ya kuongeza mzigo wa viongozi na gharama za uendeshaji ndio wanaweza mambo muhimu kama kuinua uchumi na kuongeza ajira ni ndoto ukija masuala ya kushughulikia na kutatua migogoro kama ya madaktari, waalimu na migogoro ya ardhi na madini wanafyata mkia na kuingia mitini
   
 6. only83

  only83 JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Njia ya kupeana kula tu...mamikoa yote hayo na mawilaya hayo ni zigo kwa mtanzania masikini.
   
 7. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 9,953
  Likes Received: 10,096
  Trophy Points: 280
  Unaongeza ukubwa wa serekali wakati hata hzo zilizopo ni ngumu kuzihudumia. Au ndio yale yale ya kuongeza ukubwa wa serekali ili kila mtu aweze kupata fadhila?
   
 8. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Hizi pesa za kuhudumia hii Mikoa sijui zitatoka wapi? Kama za kuhudumia Mikoa iliyopo ni shida . Pesa za madakitari ni shida ! Za walimu ni shida ! Du Kweli ukiongozwa na boga lolote linawezekana
   
 9. tindo

  tindo JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 9,953
  Likes Received: 10,096
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa ukiwauliza nini kitaendelea wenyewe wanahamaki na kukushangaa eti wewe mtu wa ajabu sana, wakati tunapata uhuru tulikuwa na mikoa mingapi na wilaya ngapi ukilinganisha na sasa. Kumbe hawajua watu wenye akili wanaangalia ubora na sio wingi
   
 10. s

  sawabho JF-Expert Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Kuongeza tu ukubwa na gharama za kuendesha Serikali
   
 11. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana
   
 12. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Jamani mbona haya maajabu mi katika maisha yangu sijawai kusikia mkoa wenye wilaya mbili
   
 13. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Badala ya kutoa taarifa kuhusu mgomo wa madaktari wanatoa taarifa kuhusu mikoa na wilaya mpya. Prioritization!!!
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  upuuuzi wa serikali yetu
   
 15. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  vipi hii itapunguza matatizo yetu au ndio itaongeza???? Poor tanzania
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna mikoa mpaka tunavyoongea wamesha exhaust bajeti zao yaani now till July ni mwendo wa tia maji tia maji.
  Sasa iyo mipya labda ingoje bajeti ijayo!
   
 17. m

  mob JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  wakati tunajaribu kuungana kuwa kitu kimoja wengine wanapambana kutugawa kwa kuanzisha maeneo mengine ya kiutawala kwa manufaa yao wenyewe ya kisiasa.

  ndugu zangu kiukweli mie sikubaliani na hili jambo la kugawa mikoa mipya nawilaya mpya.ni kwa nini wanaongeza sehemu za kitawala ili hali wameshindwa kutawala maeneo yaliyopo.madhalani ukienda moshi kuna wilaya ya moshi mjini na moshi vijijini ila hakuna makao makuu ya wilaya ya moshi v na hivyo hivyo hakuna mkuu wa wilaya ya moshi vijijini acha hizo nenda dodoma kuna wilaya za bahi chamwino na dodoma mjini zote makao makuu yake yako dodoma mjini ndo hapo unajiuliza wanaofanya hivyo wanaangalia nini cha zaidi.
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280

  Mkoa wa Katavi utakuwa na wilaya mbili za Mlele na Mpanda.......hii sasa ndio nini mkoa kuwa na wilaya mbili tu?.......halafu mikoa yote mipya ni kama kuwapendelea viongozi fulani....Geita(Magufuli).....Simiyu(Chenge).....Katavi(Pinda)......Njombe(Makinda)...
   
 19. Kaka mwisho

  Kaka mwisho JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Tuache umbumbu jamani. Mbona mnakuwa kama watoto kwa michango yenu ya ajabuajabu. Kama huna hoja kaa kimya sio kila kitu uchangie
   
 20. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  hapa sasa ukuu wa wilaya ingekuwa unagombea ningesema nikachukue fomu japo nijiliwaze na ukuu wa wilaya,

  lakini ndo yale yale, mahawara na watoto wao waliowazaa nje ya ndoa zao ndo watapewa nafasi za uongozi ambao hakuna wanachokifanya, me sielewi hii serikali inachofanya ni nini?

  its about time tuigawe hii nchi, maana itoshe sasa kugawa mikoa na kuongeza mzigo kwa serikali moja ambayo haina uwezo wa kuihudumia si tu mikoa iliyopo, achilia mbali mikoa mitatu tu.

  Suluhisho la pekee sasa ni kuigawa hii nchi zitoke nchi tatu kila mmoja kivyake au tuwe na serikali ya majimbo japo manne ambayo kila mmoja ata manage jimbo lake kama usa.

  Aaaaah me nimechoka sasa jamani.
   
Loading...