Kugoma ni wajibu kama diplomasia haitambuliki. Kelele za chura hazimzuii ngombe kunywa maji. Wewe ulisomeshwa bure! bure Waziri! Ndo maana hauelewi chochote! Na wanao wanasoma nje!. Sasa mmeubidilisha mfumo umekuwa wa mikopo. Na mikopo yenyewe hamtuoi!. Hela zote mmepeleka EPA, RICHMOND, Kwenye chaguzi, Kugawana, CCM na katika 'Maufisadi' lukuki usiohesabika, sasa Taifa litegemee nini?
Vitisho havifui Dafu kwenye Akili ya 'intellectuals' pole waziri. Mtawaonga wachache, lakini wenye uchungu wa kweli hamtawaweza. Elimu ndiyo Maendeleo, Uchumi na Maisha bora. Mawaziri mmesafiri mno kwenda nchi za wenzetu mmeona maajabu ya nguvu ya elimu. Hata hamuoni haya mkijilinganisha nao?. Eti mnaimba tu kila siku nchi changa. Unahitaji profesa wa Oxford au wa Havard aje akwambie kuwa tatizo Ni uongozi mbovu? Mungu Ibariki Tanzania