Serikali yasitisha Uhamisho wa Walimu nchi nzima

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Serikali imezuia uhamisho wa walimu nchi nzima ikieleza kuwa sababu za kuomba hivyo nyingi ni za uongo.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Mwita Waitara amesema hayo bungeni leo Alhamisi Aprili 25, akieleza kuwa kuanzia sasa uhamisho utatolewa kwa kibali maalumu na masharti muhimu kutoka serikalini.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mrimba (Chadema), Suzan Kiwanga ambaye amehoji kuhusu upungufu wa walimu hasa wa kike katika wilaya ya Kilombero.

"Suala la kuhamisha walimu kwa uhamisho wa ndani liko chini ya mkurugenzi na hapa ninaagiza kufanyika marekebisho hayo mara moja tena ndani ya miezi miwili au wiki mbili ili kupata walimu kwa jinsia zote," amesema.

Waitara amesema Serikali imefikia hatua ya kuzuia uhamisho kutokana walimu wengi kusingizia kuwa wanawafuata wenza wao na kugundulika kuwa sbabu nyingi ni za uongo.

Katika swali la msingi, Mbunge Viti Maalum (CCM), Ferister Bura alitaka kujua ni lini Serikali itaajiri walimu 527 wa masomo ya sayansi katika mkoa wa Dodoma.

Akijibu, Waitara alisema ni kweli Dodoma ina upungufu wa walimu lakini Serikali imeshatoa kibali cha kuajiri walimu 4,549 wakiwamo walimu wa sayansi na hisabati.
 
Nasikitika kuuacha ualimu wakati bado ninaupenda ila sijutii was a right thing to do,tatizo jingine kubwa waalimu wengi nao ni kama tawi la chama dola,hawana uwezo wa kujisimamia ma kujiongoza,wakati wa kampeni kwa visenti ,vikanga,caps wananunuliwa na chama dola kikisha fikia malengo yake ,kinawatupa kama tunavyofanya kwa toilet papers,bado na mtapata tabu sana kwanza offer yenu ya kupanda daladala bure ndani ya jiji la DSM bado ipo!!!!
 
Hahhha uliacha mwaka gan mkuu
 
Si haki kuzuia haki ya watu wawili kwa kuwa wapo Elfu moja wasio waaminifu walidanganya

Jukumu la Serikal ni kujiridhisha uhalali wa maombi sio ku generalize
 
Safi waziri wamezidi kuhama na wakae kituo kimoja miaka 30 tena wasiruhusiwe kabisa kukutana na wenzi wao kwa kuwa itawafanya wasiganye kazi kwa weledi .
 
Nasikitika kuuacha ualimu wakati bado ninaupenda ila sijutii was a right thing to do,tatizo jingine kubwa waalimu wengi nao ni kama tawi la chama dola,hawana uwezo wa kujisimamia ma kujiongoza,wakati wa kampeni kwa visenti ,vikanga,caps wananunuliwa na chama dola kikisha fikia malengo yake ,kinawatupa kama tunavyofanya kwa toilet papers,bado na mtapata tabu sana kwanza offer yenu ya kupanda daladala bure ndani ya jiji la DSM bado ipo!!!!
Nafikir ni umasiki wa kutupwa ndio unaowasumbua, siku 1 nilipanga folen bank na walimu walikuwa wamelipwa madeni yao lkn hiyo furaha waliyokuwa nayo na matani wanayotaniana hadi nikasema hawa watumishi pengine wamelipwa mamilioni kuja kuangalia cheki zao ni kat ya laki 2 au 3, kimoyomoyo nikasema tz tunasafar ndefu sana ili tujikomboe, kwa siku hiyo sidhan kama ungeongelea ubaya wa serikali hao walimu wangekuelewa.
 
Hahhha uliacha mwaka gan mkuu
wakati nchi imeshaanza kupoteza heshima na adabu,ila nimesoma ualimu wakati tunalipwa kichele(100tshs),tunalipwa nauli wakati wa likizo(inategemeana na umbali unaosafiri),JKT tulikuwa tunalipwa (100tshs) sasa wewe jongo wakati paymaster analipa na kambi niliyokwenda paymaster wetu alikuwa analipa siku yeyote na muda wowote btn 23th hadi 30th ya kila mwezi!!but JKT LIMENIFANYA NIWE A DIFFERENT PERSON,na ninashukuru nimefanya mafunzo haya chini ya makamanda halisi wa JKT...kumbuka Col.Mtono,Col.Msilu,Col.Makame,na baba yao mmmmmmm COL.MLAY(mafinga jkt) JUST imaging unamaliza CTS Mafinga jkt unakatwa bogi kwenda Chita jkt ...... kwa LT.COL.Sanga mmmmmm,utakimbizana na nyati hadi uzimie but I enjoy my life.ninakokwenda ni kufupi kuliko nilikotoka!!!!
 
Back
Top Bottom