Serikali yasitisha Uhamisho wa Walimu nchi nzima

Serikali yasitisha Uhamisho wa Walimu nchi nzima

Umaskini kitu kibaya sana.
Nafikir ni umasiki wa kutupwa ndio unaowasumbua, siku 1 nilipanga folen bank na walimu walikuwa wamelipwa madeni yao lkn hiyo furaha waliyokuwa nayo na matani wanayotaniana hadi nikasema hawa watumishi pengine wamelipwa mamilioni kuja kuangalia cheki zao ni kat ya laki 2 au 3, kimoyomoyo nikasema tz tunasafar ndefu sana ili tujikomboe, kwa siku hiyo sidhan kama ungeongelea ubaya wa serikali hao walimu wangekuelewa.
 
Wenye sababu za ukweli wanadhulumiwa haki zao kwa upumbavu wa wenye dhamana!!

Mnatarajia watoto wetu watapona kutiwa mimba!!?
Suala la kuwatia mimba wanafunzi sio la walimu au wenye dhamana tu, jamii nzima inahusika kwa sababu ya mmomonyoko wa maadili!
 
Kwani hakuna vigezo vya kizingatiwa?ina maana wote wanaoomba uhamisho ni waongo,kweli haya ni maamuzi ya mtu mwenye akili?
Unaweza kuzingatia vigezo lakini sababu ikawa sio ya msingi!
 
Si haki kuzuia haki ya watu wawili kwa kuwa wapo Elfu moja wasio waaminifu walidanganya

Jukumu la Serikal ni kujiridhisha uhalali wa maombi sio ku generalize
Ndiyo maana tumesema maombi yao yaletwe wizarani ili tujirizishe kama sababu zao ni za msingi!
 
Kwahio wote wanaomba kwa sababu zisizo na msingi?
"Waitara amesema Serikali imefikia hatua ya kuzuia uhamisho kutokana walimu wengi kusingizia kuwa wanawafuata wenza wao na kugundulika kuwa sbabu nyingi ni za uongo"
Walimu wengi haimanishi "WALIMU WOTE"
 
Ndiyo maana tumesema maombi yao yaletwe wizarani ili tujirizishe kama sababu zao ni za msingi!

Wizarani kuna Watumishi sawa na Halmashauri?

Au Huko Wizarani mnatumia Microscope kugundua madai halali?
 
Hapa waitara kachemka,atajuaje kuwa sababu Fulani ya msingi ama lah? Nimewahi kufanya Nazi mkoani Lindi ilifika kipindi nikataka kuacha kazi kulingana na mazingira kutokuwa rafiki kwangu,Mungu saidia nikapata uhamisho.waitara atambue kuwa kuhama ni haki ya mtumishi kama yeye alivyohama toka Chadema na kuja CCM,naona ameanza kuharibu chama chetu.
 
Back
Top Bottom