Serikali yasema haijarudisha walioghushi vyeti

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
SERIKALI YASISITIZA KUTOWAREJESHA KWENYE UTUMISHI WA UMMA WATUMISHI 15, 538 WALIOGHUSHI VYETI

Serikali imesisitiza kutowarejesha kwenye Utumishi wa Umma Watumishi 15,538 walioondolewa kazini kwa kughushi vyeti au kutoa taarifa za uongo katika kumbukumbu zao rasmi za kiutumishi kuwa wana elimu ya kidato cha nne.

Akizungumz na Waandishi wa Habari leo jijini Arusha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema, msimamo wa Serikali wa kutowarejesha watumishi hao waliobainika kughushi vyeti uko palepale.

“Ninasisitiza kuwa, hakuna msamaha wowote uliotolewa na Serikali kuwarejesha watumishi waliokosa uadilifu kwa kughushi vyeti au kutoa taarifa za kiutumishi zisizo sahihi,” Mhe. Mchengerwa amefafanua.

Aidha, Mhe. Mchengerwa ameuarifu umma kuwa, Serikali imewaondoa pia watumishi hewa 19,708, hivyo kuiwezesha Serikali kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 19 ambazo zinatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Akizungumzia watumishi waliorejeshwa kazini baada ya kuondolewa kwenye Orodha ya Malipo ya Mishahara, Mhe. Mchengerwa amesema, mwaka 2004 Serikali ilitoa Waraka uliobainisha kwamba watumishi wote watakaoajiriwa kuanzia tarehe 20 Mei, 2004 walitakiwa kuwa na elimu ya Kidato cha Nne ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya Sera ya Ajira na Menejimenti ya Utumishi wa Umma pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma.

Mhe. Mchengerwa ameongeza kuwa, katika utekelezaji wa matakwa hayo, mwaka 2017 wakati wa zoezi la uhakiki wa vyeti na watumishi hewa ilibainika baadhi ya watumishi wenye elimu ya Darasa la Saba waliajiriwa bila ya kuwa na cheti cha ufaulu wa elimu ya Kidato cha Nne. Hivyo, watumishi hawa waliondolewa kazini kutokana na kukosa sifa kwa mujibu wa Miundo ya Utumishi ya Kada zao.

Amesema katika zoezi hilo, baadhi ya Waajiri waliwaondoa kwenye Orodha ya Malipo ya Mishahara kimakosa watumishi wasiokuwa na elimu ya Kidato cha Nne walioajiriwa kabla ya tarehe 20 Mei, 2004. Kutokana na makosa hayo, mwaka 2018 Serikali kupitia Waajiri na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora iliwarejesha kazini na kuendelea kuwalipa mishahara jumla ya watu
 
Iko hivi, hilo zoezi lilikumba watumishi wengi, sio wenye kughushi vyeti tu, kuna walitupwa kwenye hewa kwa kukosa barua za ajira japo walimudu kazi zao na kupata mshahara usiopanda daraja. Labda serikali ingefanya usaili upya kwa wale wote waliondolewa kazini kwa sakata hilo, kuna walioajiriwa kwa kuwa na vyeti zaidi
 
Basi Kama Ni hivyo,
Milaard Ayo na wenzake waloripoti Iyo habari wachukuliwe hatua.
 
Back
Top Bottom